Kuwa mwaminifu na mkweli - Dr. Benjamin Carson











Daktari Ben Carson ni kati ya watu ambao walinisisimua tangu nikiwa kinda. Nimesoma vitabu vyake Gifted Hands, Think Big na the Big Picture.

Katika mambo muhimu ambayo huwa nayakumbuka kupitia vitabu vyake ni suala la uaminifu. Kwamba ni muhimu kusema ukweli. Ukisema ukweli hautalazimika kukumbuka ulichosema kabla!

Ukweli hata katika mambo madogo kama wakati unapoulizwa ulipo kwenye simu. Uaminifu unalipa. Na kweli nimethibitisha kuwa uaminifu unalipa.

Kama unapenda kusoma vitabu hivyo, jaribu kwenye maduka ya vitabu katika mji uliko.

DSM - Christian Bookshop, Mtaa wa Mkwepu makabala na Billicanas, au Mlimani city, Barabara ya Sam Nujoma.

Arusha- Book Point, Kimahama ama Kase Store.

Bonyeza hapa kupata picha ya falsafa yake.

Maoni

  1. wewe inaelekea unadili la kusambaza vitabu vya huyo daktari ebu niunganishie na mimi basi, yaani unatangaza hadi maduka yanakouzwa,,haya ntakitafuta nikuunge mkono

    JibuFuta
  2. Katika Nchi ya Bongo ukitangaza chochote, kinachokuja akilini mwa baadhi ya waungwana ni 'dili' la pesa. Sishangai.

    Kuelekeza kinakopatikana kitu ninachodhani ni chema kwa faida ya wasomaji, sidhani kama hili haliwezi kuwa jukumu la blogu hii.

    Nitafurahi kama utaniunga mkono kwa kuvisoma vitabu vya mwandishi niliyemtaja. Itakuwa ni dili lenye maslahi ya muda mrefu.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia

Pay $900? I quit blogging