Tofautisha dini yako na utamaduni wa "wenye dini"

Wakati umefika wa kuchukua juhudi binafsi za kutenganisha dini na utamaduni wetu kama vitu viwili tofauti. Tuweze kupambanua mambo ambayo ni ya kidini na yale ya utamaduni wa nje, ambayo kwa kujua ama kutokujua tunadhani kwa kuyafanya maana yake tunashika dini.

Kuvaa kanzu na baibui si utamaduni wetu. Kuitwa Mathayo hakuhalalishi ukristo wako. Kukaa chini katika ibada, wakati kuna uwezekano wa kupata viti, ni kujaribu kuwaiga wenye dini na mazingira yao.

Na bahati mbaya twayafanya hayo tukiamini kuwa tunashika dini kumbe ni ulevi tu wa utamaduni wa watu fulani fulani. Tujielewe.

Maoni

  1. Huu ni wakati kweli wa kuamka kifikra hasa haya masula ya Dini. Nimekuwa kwa muda mrefu nikifuatilia mambo hayo lakini ukweli kuna mambo yamekuwa magumu sana kuyaelewa. Nikiwafuata hao viongozi wa dini na kuwadadisi wengi husema ninaelekea kuchanganyikiwa au wengine nina pepo na wengine nina kufulu.
    Ni kweli Bwaya kuvaa kanzu au baibui sio utamaduni wetu, huu utamaduni tumelazimishwa na hao walioleta hizi dini.Manake unaambiwa usipovaa hivi we sio ktk dini yetu jamani hebu tujiulize swali huyu atakuwa ni mungu wa aina gani anayeangalia mavazi ya mtu na sio kuangalia mtu kama mtu mawazo yake na matendo yake?Wengine wanaambiwa usipoitwa jina la mtakatifu fulani sio miongoni mwetu.Kwa Mungu ndugu zangu hakuna suala la majina kama tutadhania hivyo tutakuwa tumepotea sana.Katika uislam kuna watu kabla hawajawa waislam walikuwa na majina yao na baada ya kuwa waislam walibakia na majina yao iweje leo hapa kwetu mtu ukitaka kuingia kwenye uislamu inabidi ubadili jina lako ndiyo utakuwa muislamu safi?Vivyo hivyo katika ukristo historia inaonyesha watu waliomkubali kristo waliingia katika ukristo na kubakia na majina yao.SWALI:Abubakari swahaba mkubwa sana wa Mtume Muhamad kabla hajawa muislam aliitwa nani na Petro mwanafunzi wa Yesu kabla ya kumpokea krist aliitwa nani?
    Jamani huo ulikuwa ni utumwa wa kifikra na kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa katika hilo manake huwezi kuamini watu ni wengi ambao tuko katika kuamini dini ya mtu iko kwenye jina!Hayo majina huo ni utamaduni wa waliyo yaleta hayo majina,kila jina ambalo tunaamini ni la kidini sio kweli TUMEDANGANYWA. Ninavyojua mimi kila jamii huwa ina utaratibu wake w kuwapa watu wajina.

    JibuFuta
  2. Mkuu wengi wanakesha makarisani,wengi wanajiita walokole eti watakwenda mbinguni,nawaluteri au wakatoliki je?bado tuko katika giza,bado tumetekwa na imani kali ya utamaduni wa watu wengine.babu zetu waliaabudu mizimu lakini leo!

    JibuFuta
  3. Nuru na Luihamu, nadhani kuna umuhimu wa kuziruhusu fahamu zetu kuchunguza na kutafakari masuala ambayo hapo mwanzo hatukuweza.

    Ni kucharibu kuchunguza miwani tunayoitumia kuyatazama masuala hayo. Hiyo ndiyo hatua ya kwanza.

    Asanteni kwa ushirikiano mnaouonyesha katika harakati hizi za kujielewa.

    JibuFuta
  4. Mkristo umechokoza mada nzuri!! kwamtazamo wangu kutengamanisha dini na utamaduni ni kitu kigumu saana. kwasababu unapoongelea utamduni ndani yake kuna vitu vingi ikiwemo dini. kwahiyo unapotaja dini fulani tayari unautaja utamaduni wa watu fulani. Dini, sanaa na vitu vngingine vingi ndio pakacha moja linalounda utamaduni fulani.
    Lakini ni mwanzo mzuri kama tumeanza kufikiri namna ya kutofautisha dini na utamaduni. tutafika mahali tutaanza kuangali namna ya kutenganisha dini na "political interests" za hao walioleta hizo dini zilizojificha ndani yake!
    Lakini kwa maoni yangu suala sio kupembua na kutangamanisha bali, ama kuzipiga chini kabisa au kuzitohoa ziendane na mukhtadha wa utamaduni wetu tulionao (kama tunao)

    JibuFuta
  5. inawezekana vipi kutofautisha dini na utamaduni wa wenye dini wakati hao ndo waliotuletea dini hizo wakiwa na tamaduni walizonazo!.kama tunataka kutafuta ukweli kisayansi ni kuwa huwezi kuitwa mkristo au muislamu bila kushikwa na tamaduni za hao waliotuletea dini na kutupotosha kuwa ukiitwa MICHAEL ni jina la kikristo wakati kiukweli jina hilo linatambulisha utamaduni wa waingereza wakati yesu hajawahi kuwa muingereza!.hivyo basi haiwezekani kutofautisha dini za kigeni na tamaduni zao labda kama tutaanzisha dini zetu na kuingiza tamaduni zetu humo ikiwemo na kujiita majina ya tamaduni zetu kama "kubalunga".

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia

Uislamu ulianza lini?