UKIMWI una tiba kumbe?


Sikuandika siku kadhaa zilizopita, kipingamizi kikiwa ni uvamizi wa kirusi. Nafurahi kwamba "tabibu" alipatikana, na tiba sahihi ilifanyika, UKIMWI ukasalimu amri.


Shukrani za pekee zimwendee Bwana Minja, msomaji wa blogu (yeye anadai inatosha kuzisoma) na fundi mwanafunzi katika sayansi ya kompyuta. Kwa hakika tunawahitaji sana watu kama hawa katika jamii zetu, watusaidie "kugawana" umasikini wetu.
Minja. Minja kaozea katika teknolojia. Minja. Minja na spana. Minja. Ukienda kwa Minja hutathubutu kuongea siasa. Si tu kwamba hatakusiliza, lakini pia mazingira hayatakuruhusu. Bush kafanyeje, wala hajui na hataki kujua. Ongea teknolojia. Ndugu yangu utakoma. Huo ndio mgawanyo wa kazi unaotutofautisha wenyewe kwa wenyewe.
Ndugu Minja nakushukuru sana.


Nitajaribu kuchukua hatua za dharura, tatizo lisijirudie. Wanasema tubadili tabia ili kuepuka gonjwa lile. Basi huenda tabia yangu ya kunyonya blogu mtandaoni na kuzihamishia kwenye kimeo changu inaniponza.
Muhimu, niweze kuandika.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Pay $900? I quit blogging

Kama sio utumwa ni nini hiki?

Kikao cha tathmini na mipango ya familia

Padre Karugendo kakosea kipi hasa?

Aprili: Utasoma vitabu vingapi?

Huu si udhaifu wa kiume?

Strictly gospel na mijadala ya kiimani