Unahusianaje na nafsi yako?
Huwa unajisikiaje ukijitazama kwenye kioo? Unaridhika na sura unayoiona? Vipi ukiangalia picha zako za hivi karibuni? Unaridhika na ulivyo? Umbo lako? Mtindo wa nywele zako? Rangi ya ngozi yako? Unajionaje? Watu wengi tunapata shida sana kujikubali. Hatujipendi. Kila tunapojitazama, tunaona kasoro. Wachache wetu huziona kasoro hizo kama vitu vidogo visivyotupa tabu sana. Mtu aweza kujiangalia kwenye kioo, akaona kasoro ndogo, lakini akajipa moyo: "Ngoja nichane, nitapendeza". " Ngoja niende saluni, nikabadili mtindo". Akaziona kasoro na zisimsumbue. Lakini wengi wetu huvunjika moyo kwa kudhani/amini kuwa kasoro hizo hazirekebishiki. Pengine rangi ya ngozi si nyeupe vya kutosha. Ama umbo letu halivutii, na mambo kama hayo. Kuvunjika moyo kwa namna hiyo, husababisha kujengeka kwa hisia hasi kuhusu nafsi ya mtu mwenyewe. Jambo moja kabla hatujaendelea: Mahusiano mema na nafsi zetu hutokana na vile tujichukuliavyo. Mahusiano mabaya na nafsi zetu husababisha kujidh...