Wewe ni nani?

"Wewe ni nani?" Uliza swali hili kwa kila unayekutana naye na sikiliza majibu yao:
"Mimi ni Idi"
"Mimi ni Mashaka" Tena kwa kujiamini kabisa.
"Mimi ni Masumbuko" Huku akikushangaa kwa kumuuliza swali la kitoto.

Ukionesha kutokuridhika na majibu hayo mepesi, ukaongeza swali jingine, sana sana utaonekana mtu wa ajabu unayeuliza kitu kinachoeleweka. Utaonekana huna kazi.

"Unaulizaje swali kama hilo? Ina maana unataka kunifanya mimi sijijui?"

Lakini ukweli ni kwamba pasipo kujibu swali hilo, kila unachokifanya kitakuwa ni kupotea njia. Sababu wewe ulikuwa wewe kabla hujapewa hilo jina ulilonalo. Yaani wewe ulikuwa wewe kabla hujaambiwa ni wewe.

Jitahidi usipotee njia. Anza leo. Jijibu swali hilo. Nakutakia siku njema ambayo inaweza kuwa mwanzo wa kujua wewe ni nani hasa wakati unazaliwa.

Maoni

 1. Swali gumu sana hili ingawa watu hawalichukulii umaanani.Naamini watu kibao tutakufa hatutajijua wala kujiuliza hili swali kwa kisingizio tunajua majina yetu.

  JibuFuta
 2. Kazi ipo. Ni kweli hadi tutakufa hatutajijua sisi ni nani na kwa sababu tumeshindwa kujijua sisi ni nani hata sababu ya kuwepo duniani hatutaijua. Ndio maana wengi tunakufa bila ya kuwa na mchango wowote kwenye jamii sababu hatujiui sisi ni NANI?

  JibuFuta
 3. Sio tu kujua sisi ni nani lakini hata kujiuliza swali hili ni kazi kwa wengi wetu.

  Ndio maana watu tumekuwa tuhangaika kufanya mambo mengi ambayo hayaakisi taswira yetu halisi. Tunafanya mambo kwa kisingizio kwamba yanafanywa na wengine. Tunasahau kuwa kila mmoja anachokitu cha pekee cha kufanya ambacho hakijawahi kufanywa na mwingine yeyote duniani. Hilo linawezekana kama tutajibu swali hilo alilouliza Bwaya.

  Mjada huu ni mpana na mzuri.

  Bwaya hongera kurudi ukumbini. Ile sehemu ya dini mbona imekuwa kimya?

  JibuFuta
 4. Usiwe na shaka Kulaba. Sehemu hiyo ipo kama kawa. Nashukuru kwa kutembelea kibaraza hiki.

  JibuFuta
 5. Mhuu yaani swali nzuri,ila hadi sasa sina jibu lolote,nisaidieni kulipata jibu.

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Fumbo mfumbie mwerevu

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3