Kuwa halisi, ufe halisi

Kila binadamu anazaliwa halisi/origino. Uwezo halisi. Akili halisi. Mtazamo halisi. Maono halisi. Sura halisi. Machache kwa kutaja. Uhalisi huu una maana ya kuwa na uwezo wa kipekee katika uasili wake ili kutimiza jukumu halisi na la kipekee katika jamii.

Bahati mbaya idadi kubwa ya wanadamu hawa waliozaliwa origino, wanakufa wakiwa "fotokopi" za watu fulani. Wanaiga kila kitu. Mtizamo bandia. Fikra bandia. Akili bandia. Uwezo bandia. Sura bandia. kazi bandia. Na kadhalika. Bandia hapa ina maana ya kuwa ama kujaribu kuwa mtu mwingine tofauti na yule halisi aliyezaliwa akiwa wewe. Bandia ina maana ya kutafuta kufanya jambo lisilo lako. Kuiga. Kupoteza muda kufanya kitu ambacho si halisi yako.

Vipi, u halisi wewe? Au umekuwa fotokopi ndugu yangu? Rudi kwenye mstari utafute uhalisi wako. Hapo utakuwa umejielewa.

Maoni

 1. Bwaya unanifurahisha sana.Mi bado niaelekeza kwenye mfumo mzima wa malezi yetu.Tumefanya kujikataa sisi wenyewe ni wachache sana ambao huamini kuwa wao ni tofauti sana na wazazi wao.Wengi huwa tunaamini katika maumbo ya nje,mfano mtu akiwa anafanana sura na moja kati ya wazazi wake hupenda kujitahidi kufanya kama afanyavyo mzazi wake matokeo yake ni kujifotokopi na wala sio kubaki yeye origino.
  Laiti kama tungeweza kujielewa uhalisi wetu hii dunia ingekuwa ni mahali pazuri sana.Mtu yuko tayari kuamini kupitia kwa wazazi wake pale alipoambiwa kabila fulani ni wabaya naye akaamini bila hata kufikiri.
  Bwaya endelea kutupa shule,ninakukubali.

  JibuFuta
 2. Nuru nakubaliana na wewe kabisa. Nadhani wazazi wanapaswa kuelewa kuwa wanao uwezo mkubwa wa kuwafanya wanao wawe vyovyote wapendavyo.

  Nakushukuru kwa michango yako muhimu. Unanipa changamoto sana.

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Fumbo mfumbie mwerevu

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3