Hitilafu ndogo

Kutokana na sababu ambazo ni za wazi, ili kublogu huwa natumia tarakilishi-paja kuandikia na kisha kuja mtandaoni kupesti maandiko yangu. Kufanya hivyo hunipunguzia gharama za muda wa kukaa mtandaoni ambao kwa nchi tajiri kama yetu, unagharimu sana.

Kwa bahati mbaya sana, tarakilishi hiyo imepata UKIMWI siku kadhaa zilizopita! Kuna kirusi kaivamia na ananizuia kufanya chochote. Jitihada za kumtafuta daktari wake zinaendelea.

Maoni

  1. Hawa wadudu wamekuwa hatari kweli,namimi tarakishi yangu imevamiwa,hope leo nitamtoa nina nafasi

    JibuFuta
  2. Pole sana kwa kirusi hiki. Tutaendelea kukusoma kama 'utapona'

    JibuFuta
  3. pole kaka mimi mpia nina jamaa anaitwa trajon horse na adware wananila mwezi sasa nimejaribu program tatu tofauti naona zinamshindwa ninakomaa nao hivyo hivyo nikijaribu kuhamisha mafail muhimu ili nishushe injini. jamaa wamekuwa hatari sana natumia viprogram vya kutuliza maumivu kwa sasa ant vir na avast.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?