Machapisho

Mjadala wa dini na sayansi unaendelea...

Najaribu kupangilia mambo yangu niweze kujadili masuala ya dini wakati wowote kuanzia sasa. Wadau wa masuala haya ninawakaribisha nyote. Jana nilianza kwa kujiuliza swali kuu: Je, ni dini inaiogopa sayansi ama sayansi ndiyo inayoiogopa dini? Mdau wa mjadala huo, Profesa Matondo alikuwa na mchango huu wa kusisimua: ' ''Hili ni suala zito ambalo limehangaisha mafilosofa kwa muda mrefu sana. Kuna mambo ambayo sayansi haijaweza kuyaeleza. Dini kwa upande wake, kwa vile haihitaji vithibitisho kama vile sayansi, inaweza kujibu kila kitu kwa mwenye imani. Kuna mzozo mkubwa sana unaendelea hapa Marekani kuhusu ufundishaji wa nadharia ya Evolution ya Charles Darwin. Walokole wa hapa Marekani wanataka ama ifutiliwe mbali kufundishwa mashuleni au uumbaji (creationism) wa Mungu pia nao ufundishwe kama nadharia mbadala (alternative theory). Wanasayansi wanabisha kwamba uumbaji hauwezi kuthibitishwa kisayansi kama kweli ulitokea na kwa hivyo hauwezi kufundishwa mashuleni. Sij...

Dini inaiogopa sayansi?

Nilitegemea kwamba dini na sayansi vingeenda pamoja. Kwa sababu nionavyo mimi, upo uhusiano mkubwa kati ya vitu hivyo viwili. Kwanza, vyote vinahusu maisha ya watu japo kwa namna tofauti. Lakini pili si lazima viwili hivyo vitengane ili kujenga heshima yake. Lakini ajabu, karibu mara zote tangu maendeleo ya sayansi maumbile yanaanza inaonekana wazi kuwa dini imekuwa kinyume nayo. Je, ni hali hii ni halisi au ni hisia? Je, ni dini inaiogopa sayansi ama sayansi ndiyo inayoiogopa dini? Nitafafanua nikirudi

Blogu mpya nyingine

Picha
Sogea karibu usome blogu ya Ndugu Renatus Kiluvia . Yeye ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kituo cha redio cha 87.8 Ebony fm cha Iringa lakini kwa sasa yuko kwenye studio ndogo ya Dar. Kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe, blog hiyo inahusu muziki na maisha katika nyanja tofauti-tofauti. Pia itahusika kuzungumzia burudani zingine kama filamu n.k. Bonyeza hapa upate kila kitu .

Stella mwanablogu mpya

Kila siku jamii ya wanablogu wa kiswahili inazidi kupanuka. Hivi sasa zipo blogu za kiswahili zaidi ya mia mbili na zinaendelea kuongezeka. Dada yetu Stella naye kajiunga na jamii yatu. Bofya hapa kumkaribisha , kuona maudhui ya blogu yake na pia kuendelea kumsoma. Dada stella, karibu sana.

Kutoka Maktaba: Ndesanjo unaombwa kurudi kundini

Picha
Katika safari ya kupitia kilichomo kwenye maktaba yetu, niliyoisemea kidogo jana, nilimfuma mdogo wangu anayenifuata, akirejea makala za mwandishi Ndesanjo Macha. Makala hizi ni zile alizoziandika kati ya mwaka 2005 mpaka 2007 katika magazeti ya Mwananchi Jumapili. Wakati huo mdogo wangu akiwa kidato cha tano na sita alianza kuzifuatilia kama matokeo ya mkumbo tu (pengine) lakini baadae ukawa ndio ugonjwa wake mpaka zilipotoweka ghafla zaidi ya miaka miwili iliyopita. Sasa akiwa anamaliza Chuo Kikuu mwaka 2010, makala hizo anazisoma kwa kupitia 'hifadhi' ya magazeti yale ya chumbani kwetu. Nimeshawahi kumkuta mwaka jana akiwa na vipisi vya safu ya "Rai ya Jenerali" vyenye tarehe za mwaka 1995 mpaka 2005 vikiwa vimeungamanishwa kwa pamoja na kufanya kitu kama kitabu fulani hivi ambacho alikuwa akitembea nacho kwenye begi lake. Kwa hiyo sikushangaa kukutana na shughuli hii ya kukusanya makala za Ndesanjo hivi majuzi. Picha hizi ni ombi maalumu kwa Ndesanjo M...

Amana ya ‘nguvu zangu’

Picha
Hivi majuzi, nilipata fursa ya kula pasaka nyumbani kwetu, Singida. Katika niliyoyafanya, ni pamoja na kukagua ‘maktaba’ ambayo mzee wangu alitutengenezea chumbani kwetu. Ni kijishelfu kidogo ambacho alikitumia enzi hizo kutuwekea vitabu kadhaa kila mara na kutuhimiza kuvisoma. Pamoja na vitabu, humo aliweka nakala za magazeti ya Rai ile ya zamani na mengineyo. Na kweli tuliyasoma, mimi na mdogo wangu. Namshukuru baba yangu kwa hilo. Maana nakumbuka alinifanya nianze kugharamia nakala za magazeti tangu nikiwa kijana wa darasa la sita na saba. Niliweza kubana matumizi ili kumudu kununua gazeti hilo kila wiki. Ndio ulikuwa ulevi wangu. Pia nimshukuru kwa sababu alinijengea ari ya kuiba vitabu kila nilikopita. Ujue kila mtu hukumbuka siku zile za ‘adolesensi’ kwa jinsi yake. Wengine kwa idadi ya wasichana aliowatongoza. Wengine kwa michezo ya ‘baba na mama’. Na kadhalika. Mimi huzikumbuka zaidi kwa wizi wa vitabu. Sikuwa na uwezo wa kumudu kununua vitabu nilivyovipenda. Kwa hiyo ...

Arusha warembo ni majasiri wa kibiashara

Picha
Nimewapenda akina dada hawa wanaojishughulisha na biashara halali kama hizi. Ni majasiri wasiosita kufanya shughuli kama hizi kujipatia kipato licha ya urembo wao. Hapa niliwafuma wakimsubiri mwenzao. Then wakaendelea na shughuli zao. Pongezi kwao.

Padre Karugendo ndani ya Blogu

Kama ulizoea kusubiri siku ya Jumatano kusoma mawazo ya Padre Karugendo kwenye gazeti la Raia mwema au labda Jumapili kwenye Tanzania Daima, jua enzi hizo zimepita. Sasa utaweza kupata kila unachotaka kwa wakati wowote kupitia blogu yake. Bonyeza hapa kumkaribisha , halafu uendelee kumtembelea. Karibu sana Padre Karugendo. Umechagua fungu jema kufungua blogu.

Tangazo la Mkutano Mkuu wa Uanahabari wa Kiraia wa Global Voices 2010

Picha
Mkutano wa wanablogu wa Global Voices, utafanyika Mjini Santiago mwezi Mei tarehe 6 na 7 mwaka huu. Nimezipata habari hizo kupitia ukurasa wa kiswahili wa mradi wa Lingua Swahili . Nimetamani kama na sisi tungekuwa tunapanga kukutana siku fulani mwaka huu! Inawezekana! Ni muhimu tuanze kufikiri kukutana uso kwa uso hata kama matanga ya ile Jumuiya yetu hajapita bado.

Upweke wa kutokublogu

BAADA ya kimya cha muda mrefu kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu, namshukuru Mungu wa Israeli nimerejea tena. Sijaja na kipya. Ila nimekuja kusoma mengi ya mtandaoni. Ukweli ni kwamba mtandao ni moja ya burudani zangu muhimu sana kama ilivyo mpira kwa wenzangu fulani. Kwa wenzangu na mimi tusiopenda kujua hata matokeo ya mechi za Uefa, wapi zaidi ya kwenye blogu? Nilikosa kusoma posti na maoni ya wanablogu. Nimekuwa kwenye kipindi cha upweke fulani hivi nisioweza kuueleza. Kila siku nijakosa kujiuliza: hivi Baba Mtakatifu Simon kasemaje leo? Da! Watu kama akina Mubelwa, Subira, John Mwaipopo, Yasinta, Maprofesa Mbele (bora hata ninakisoma kitabu chake kwa kukirudia na kukirudia) Matondo, akina Evarist, Kamala, Mbilinyi, Dada Vukani, Kisima, Lundu Nyasa (msee jibu lako nakuja nalo), akina Shabani Kaluse (pole na shule), wazee wa Strictly gospel (hee yale majadiliano nitayarudia mapema sana), na wengine wengi ambao nimebaki nao kichwani mwangu. Nilikosa kusoma mawazo motomo...

Posti bora ya mwaka 2009

Kabla sijapotea kwenye blogu (kwa siku mbili tatu nne)nitakushirikisha posti bora kabisa nilizozisoma kwa mwaka mzima 2009 ambazo kwa hakika zilinipa mtazamo mpya wa mambo. Nitarudi kama Shaka Ssali anavyosema-ga "Don't go away!", naja.

Blogu bora kwa mwaka 2009!

Mwaka jana umepita kwa namna yake. Namshukuru Mwenyezi Mungu amenifikisha mwaka huu salama. Japo sikuwa hewani mwishoni mwa mwaka, lakini nimekuwa nikitafakari kidogo namna mwaka ule ulivyoenda katika maeneo kadhaa ya maisha yangu. Mafanikio kwa Matatizo. Furaha kwa huzuni. Kupanda na Kushuka. Kupiga hatua mbele katika eneo moja na kurudi nyuma kwingineko. Yote yamekuwa sehemu yangu kwa mwaka uliopita. Nimekuwa msomaji wa blogu karibu zote zilizo hai. Na kwa kweli nimejifunza maarifa mengi makubwa bila kuyagharimia. Waandishi wake waliyagawa bure na uone ilivyo ajabu, maana waliweza kujibizana na wasomaji wao kwa lengo la kupanua mjadala. Na ni hakika kwamba hivi sasa blogu zimeanza kuchukua nafasi ya magazeti na televisheni, au angalau kupambana na vyombo hivyo vikongwe. Umaarufu wa magazeti ya kununua taratibu unaanza kupotea. Katika blogu za Kiswahili jambo la tofauti hivi sasa ni maudhui aina aina yanayoandikwa. Nakumbuka miaka mitatu au minne iliyopita, karibu kila blogu ilik...

Mwisho wa mwaka Singida

Picha
Hapa ni sehemu ya mji wa Singida kama ilivyokuwa Krismas ya mwaka huu. Wengine ni Bw. Albert William, mhadhiri msaidizi DUCE (huyu aliwahi kublogu hapa miaka kadhaa iliyopita, bila shaka atarejea tena. Mwingine ni mkewe Krissie, mtafiti wa bayoteknolojia, Mlimani aliyewahi kublogu hapa na kuitelekeza blogu hiyo kwa muda. Na huyo mwingine (mwenye kaki) ni kilaza, mimi.

Je, tunafikiri kwa kutumia lugha?

Kuna changamoto zimejitokeza kwenye ule mjadala wa tasnifu ya msomi wetu ambayo kwa maoni yaliyotolewa huenda ingekuwa bora kama ingekuwa katika kiswahili. Changamoto kubwa zaidi ni ile iliyoletwa na msomaji Godwin Habib Meghji akihoji ikiwa mwanadamu hufikiri kwa kutumia lugha. Hapa anasema: "Mimi sina uhakika kama binadamu anafikiria kwa kutumia lugha fulani. Viziwi na bubu pia hufikiri". Hii ni changamoto nyingine. Una maoni gani katika hili? Je, tunawezaje kufikiri? Fikra zinauhusiano wowote na lugha? Je, bubu ama kiziwi hana lugha kwa sababu tu hawezi kutamka ama kusikia?

Tembelea Website mpya

Pole na shuguli za kutupasha habari mbali mbali zinazotokea ndani na nje ya Tanzania. Naomba nafasi katika blog yako ili niwajulishe ndugu zangu watanzania kwamba nimetengeneza website www.rusumo.com ambapo wataweza kusikiliza nyimbo mbali mbali za Tanzania kama vile taarab,segere,dance,bongo flava,gospel na nyimbo za kigeni kama vile raggae,za kihindi,pop na nyengine nyingi tu. Pia kuna dictionary ya kisasa kabisa ambayo ina lugha zote za Ulaya na baadhi ya lugha za Asia,katika dictionary hii baada ya kupata tafsiri ya neno pia unaweza kuona picha za neno hilo kwa kubofya upande wa pili wa Ukurasa. Kadhalika wadau wataweza kuona hali ya hewa na wakati wa sehem mbali mbali za dunia. Karibuni sana wadau, ni mimi MSAFIRI ISMAIL RUSUMO. www.rusumo.com