Dini inaiogopa sayansi?

Nilitegemea kwamba dini na sayansi vingeenda pamoja. Kwa sababu nionavyo mimi, upo uhusiano mkubwa kati ya vitu hivyo viwili. Kwanza, vyote vinahusu maisha ya watu japo kwa namna tofauti. Lakini pili si lazima viwili hivyo vitengane ili kujenga heshima yake.

Lakini ajabu, karibu mara zote tangu maendeleo ya sayansi maumbile yanaanza inaonekana wazi kuwa dini imekuwa kinyume nayo.

Je, ni hali hii ni halisi au ni hisia? Je, ni dini inaiogopa sayansi ama sayansi ndiyo inayoiogopa dini?


Nitafafanua nikirudi

Maoni

  1. Hili ni suala zito ambalo limehangaisha mafilosofa kwa muda mrefu sana. Kuna mambo ambayo sayansi haijaweza kuyaeleza. Dini kwa upande wake, kwa vile haihitaji vithibitisho kama vile sayansi, inaweza kujibu kila kitu kwa mwenye imani.

    Kuna mzozo mkubwa sana unaendelea hapa Marekani kuhusu ufundishaji wa nadharia ya Evolution ya Charles Darwin. Walokole wa hapa Marekani wanataka ama ifutiliwe mbali kufundishwa mashuleni au uumbaji (creationism) wa Mungu pia nao ufundishwe kama nadharia mbadala (alternative theory). Wanasayansi wanabisha kwamba uumbaji hauwezi kuthibitishwa kisayansi kama kweli ulitokea na kwa hivyo hauwezi kufundishwa mashuleni. Sijui ni nani atashinda.

    Vituo vya televisheni vya History na Discovery Channel hapa Marekani huwa vinarusha vipindi vya kina sana kuhusu baadhi ya mambo yanayojadiliwa katika dini. Wao wanadai kwa mfano kwamba miujiza mingi iliyofanywa na Yesu na mingine mingi iliyomo katika Biblia inaweza kuelezeka kisayansi. Hata yale mapigo ya Musa kwa Wamisri pia si miujiza. Lakini pia wanafika mahali wanakwama na wanaishia kusema kwamba mambo mengi ni fasihi simulizi tu ambazo zilikuwa zimetapakaa katika tamaduni mbali enzi zile za kale. Kwa mfano ile hadithi ya Adamu na Eva bustanini Eden wanasema kwamba imeibwa kama ilivyo kutoka katika hadithi za kale kutoka Mesopotamia na Babiloni na kubadilishwa kidogo tu.

    Kuna mkondo wa mawazo (ambao nakubaliana nao) unaodai kwamba sayansi na dini kimsingi zinakamilishana na upinzani uliopo ni wa juu juu tu unaosababishwa na wahafidhina wa pande zote mbili kuvutia upande wao. Sote tunakumbuka ukiritimba na upuuzi wa kanisa katoliki lililokuwa linajiona kama ndilo linamiliki maarifa japo baadaye ilikuja kugundulika kwamba baadhi ya mambo yake ya msingi yalikuwa ni uwongo mf. nadharia kwamba eti jua huzunguka dunia. Hata Galileo Galilei alipomkaribisha Papa achungulie kwenye teleskopu ili ajionee mwenyewe alikataa kwani hiyo ilikuwa kinyume na dogma ya wakati ule.

    Kwa sasa wanasayansi wapo wanajaribu kugonganisha "particles" chini ya milima ya Uswizi wakitumia "The Large Hadron Collider" - mashine iliyowagharimu dola billioni 9. Eti wanajaribu kutafuta particle moja ya siri isiyoonekana ambayo ndiyo inaunda karibu kila kitu. Particle hii wameibatiza jina la "God's particle" Wakifanikiwa basi watakuwa wameonyesha kwa ukaribu sana hali ilivyokuwa mara tu baada ya Big Bang - ambayo kwao ndiyo tokeo mbadala la uumbaji ingawa hawasemi vitu vilivyogongana na kuripuka wakati wa Big Bang, kupoa na baadaye kuunda vitu vyote tuvionavyo na tusivyoviona vilitoka wapi.

    Nitaendelea baadaye ukifafanua...japo nina wasiwasi kama utarudi mapema.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia

Uislamu ulianza lini?