Padre Karugendo ndani ya Blogu

Kama ulizoea kusubiri siku ya Jumatano kusoma mawazo ya Padre Karugendo kwenye gazeti la Raia mwema au labda Jumapili kwenye Tanzania Daima, jua enzi hizo zimepita.

Sasa utaweza kupata kila unachotaka kwa wakati wowote kupitia blogu yake. Bonyeza hapa kumkaribisha, halafu uendelee kumtembelea.

Karibu sana Padre Karugendo. Umechagua fungu jema kufungua blogu.

Maoni

 1. Karibu sana Padre Privatus Karugendo katika ulimwengu wa kublog. Nimekuwa nikikusoma katika Rai ya enzi hizo tangu nikiwa High School. Leo naona fahari kukusoma humu mjengoni kwenye uhuru wa kuongea pasipo kuhofu 'topic' inaweza kutobeba maslahi ya mhariri na mmiliki.
  Karibu sana fadha.

  JibuFuta
 2. Ni habari njema hizi,nami nimekuwa mfuatiliaji mzuri saaaana wa makala za Padre Karugendo ktk gazeti la Raia mwema. Nami nafurahia sana ujio wa Padre ktk ulimwengu huu wa kublog. Karibu sana Padre Karugendo.

  JibuFuta
 3. Kaka Bwaya asante kwa taarifa hii ngoja niende kumtembelea.

  JibuFuta
 4. ngoja nijikumbushe dhambi zangu tayari kwa kitubio kwa padre karugendo. ngoja nikamsabahi.

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mbinu za Kumfundisha Mtoto Kusoma Akiwa Nyumbani

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Fumbo mfumbie mwerevu

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)