Yapo mambo mengi katika jamii zetu yaliyofanyika zamani ambayo tukiyatazama twaweza kujifunza mengi. Mengi ya hayo, si sehemu ya jamii za kisasa hivi leo, lakini yalekuwa na msaada wa namna Fulani kwa jamii. Katika jamii ya asili ya wanyaturu, kabila dogo linalopatika katika wilaya ya Singida (na kidogo manyoni), mahusiano kati ya baba na mama yalikuwa na sura tofauti sana na ilivyo leo. Wakati leo hii, wazazi kulala vyumba tofauti huchukuliwa kama ishara ya kufifia kwa mahusiano baina ya wawili hao, kwa Wanyaturu hiyo ilikuwa na maana tofauti. Kikawaida, wazazi wa Kinyaturu hawakupaswa kukaa nyumba moja (sio chumba kimoja, nyumba moja) ndani ya boma. Katika boma analojenga mwanaume kama himaya ya familia yake, alipaswa kuzingatia uwepo wa nyumba mbili ndnai ya boma moja. Baba ambaye ndiye mkuu wa boma, alilala na wanawe wa kiume katika sehemu maalumu ya nyumba inayojulikana kama "Idemu/Ikumbu". Nyumba hiyo ilijitenga pembeni na nyumba kuu alikoishi mama na wanawe wa...