Kamwe usikate tamaa
Haya tena. Siku zinakimbia kama nini vile. Ni juzi tu mwezi umeanza. Leo eti masaa machache yajayo mwezi unakatika hivi hivi. Mwaka ndio usiseme. Mwezi wa kumi na moja huu. Bado mwezi tu na mwaka ukatikie mbali. Sijui kinachosababisha siku kukimbia namna hii. Muda ni mfupi kuliko matarajio. Mambo mengi kuliko dakika zilizopo. Kazi kweli kweli. Binafsi mwezi huu umepita vizuri pamoja na changamoto za hapa na pale. Nafurahi nimeweza kuzitazama changamoto hizo kwa jicho la kujisahihisha. Nawe ndugu msomaji bila shaka mwezi umekuendea vyema. Hata kama inawezekana umekumbana na changamoto mbili tatu hakuna haja ya kukata tamaa. Usikate tamaa. Kuna mtu aliwahi kuniambia picha nzuri kusafishwa kwenye chumba cha giza. Giza ni muhimu ili kusafisha picha. Maana yake yake unapojikuta kwenye hali inayofanana na giza vile, kwa maana ya changamoto, kukatishwa tamaa, chukulia hiyo kama mchakato wa kukutengenezea picha nzuri mbeleni. Usikate tamaa. Pigana kiume. Songa mbele. Anza mwezi wa kumi...