Nimeikumbuka hii hapa...


Nimekuwa nikiamini kuwa tofauti ya mawazo ndiyo msingi wa majadiliano. Tofauti hizi ni pamoja na mitazamo na uelewa, namna tunavyo'react' tukiguswa kwenye maeneo tunadhani hayajadiliki, namna tunavyoheshimu mawazo ya wasemaji wengine wanaoamini tofauti na sisi, namna tunavyoweza kuvumiliana na bado tukajadiliana (hata kama inakuwa kama vurugu fulani vile) lakini mwishowe mnajifunza: Hakuna anayejua. Wote mnahitaji kujifunza kwa wengine.

Nimefurahi kusoma maoni ya mchangiaji aliyeamua kujificha kwenye kichaka cha jina la 'Natiakasi.' Ni bahati mbaya kwamba alidhani mimi nina chuki na dini yake anayoitetea kwa nguvu zote. Nimeona pengine itafaa nikimwonyesha chuki yangu hasa ni ipi kwa kumpeleka kwenye makala hii, niliyoiandika miaka mitatu iliyopita.

Enzi hizo nilikuwa bado naandika makala ndefu ndefu (kwa sasa huwa sioni ulazima wa kurefusha ninachotaka kukisema) kwa hiyo naomba msamaha kwa makala ndefu inayochosha.

Pamoja na kwamba wachangiaji wa wakati huo wengi wako kimya sasa, nadhani, itamfaa kujua kuwa hata Ukristo tulishawahi kuuhoji.


Saturday, September 9, 2006
Dan Vinci Code: Ukweli unaouma?



Dan Brown mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina la Da Vinci Code, kafanya kile ambacho binadamu wengine hatuthubutu hata kukijadili. Kaamua kuchokonoa mambo ya kiimani ambayo watu tunakwepa kuyahoji, kwamba hayajadiliki. Ni dogma. Trela ya filamu yake hii hapa.

Katika Da Vinci code, Dan Brown anajaribu kuchimbua “kweli” zilizojificha nyuma ya ukristo, “kweli” ambacho zimefunikwa na kanisa ili kuwapumbaza watu waamini kwamba Jeshua alikuwa mwana wa Mungu.

Kwa kadiri ya Da Vinci Code, ukweli wenyewe ni kwamba Ukristo ulianzishwa na “nabii wa kawaida” ambaye hastahili kujidai kwamba ana uungu (divinity) wowote. Nabii mwenyewe ni Yesu Kristo. Kwa hakika, alimwoa Mariam Magdalena, ambaye baadaye ndiye aliyemchagua kuliongoza kanisa baada ya kifo chake.

Suala hili, kwa mujibu wa Da Vinci Code, liliwakasirisha sana wanafunzi wake na baada ya kusulubishwa kwake, Mariam Magadalena ilibidi atimuliwe, ndipo akakimbilia Ufaransa na mtoto wao waliomzaa na Yeshua “mume” wake.

Mwandishi anasema kwamba habari hizi hazifahamiki na wengi leo hii, kwa sababu vitabu ya injili ambavyo kwavyo pekee ndiko tunakopata simulizi za Yesu zilihaririwa kwa makini sana ili kuondoa maelezo yoyote yaliyojikita katika maisha ya “kawaida” ya Bwana Yesu. (Rejea uk. 244).

Vilevile kwa kadiri ya Da Vinci Code, biblia tuijuayo leo hii, iliwekwa sawa na Mfalme wa Rumi Constantine ambaye alikuwa ni mpagani. (Rejea uk. 231). Tafsiri yake ni kwamba wakristo wanamekubali kudanganywa na mtu amabye hata hakuwahi kuwa Mkristo.

Katika ukurasa wa 231, Leonardo Da Vinci ametoa maoni yafuatayo kuhusiana na Kitabu cha agano jipya:
“Many have made a trade of delusions and false miracles, deceiving the stupid multitude”. Halafu anaendelea, “Blinding does mislead us. O! Wretched mortals, open your eyes”. Sijathubutu kutafsiri, nikihofia kupoteza maana halisi.

Nimekisoma kitabu miezi kadhaa iliyopita, wakati tayari nimekuwa msomaji wa vitabu vingi vya Theolojia, nikijaribu kutafuta majibu ya maswali yangu mengi kuhusu imani yenyewe ya Ukristo.

Kuna suala linaitwa canonization katika Theolojia, yaani utaratibu wa kuyatambua maandiko ili kuyafanya yawe sehemu ya Biblia. Katika kitabu cha Jensen’s Survey of the New Testament, utaratibu huu ulifanyika kwa maongozi ya ziada, yaani Mungu mwenyewe. Katika ukurasa wa 22 anasema “…God gave to His people (japo hawataji) in collective sense, the spiritual perception to recognize in each of these books genuine marks of divine inspiration and authority. With the Holy Spirit’s guidance, they knew what spurious writings to reject, as well as what genuine writings to accept”.

Tatizo la masuala haya ya kidini yanapojadiliwa anatangulizwa Mungu kabla ya hoja. Matokeo yake unakuta maswali mengi yanamezwa kirahisi na majibu kwamba ni Mungu. Hivyo unakuta hofu kwamba tunajaribu kujadili mambo ya Mungu, inatutia woga wa kuendelea mbele.


Suala la kujiuliza ni kwamba ilikuwaje maandiko mengine yaonekane yanafaa na mengine yakaonekana ni ya kutupa? Tutapuuza suala hili tukienda haraka kwa kufanya kama ilivyo ada ya majadiliano ya kidini: Kutangulize imani! Pengine yanayosemwa na Dan Brown ni ukweli ambao hao tunaoambiwa waliongozwa na Mungu waliuficha! Tutajuaje kama wana-theolojia wenyewe wanatuambia hivyo?

Kwa mujibu wa Bruce, F.F katika kitabu chake cha “The books and Parchments” uk. 104-13, tunaambiwa kuwa wakati hawa jamaa wanaongozwa na Mungu (Dan Brown anasema ni pamoja na pagani Constantine) wanakubaliana kitabu kipi kiingie kwenye orodha na kipi kitupwe kapuni, kukawepo mabishano mazito kuhusu vitabu vinavyoitwa Antilegomena yaani Waebrania, Yakobo, Waraka wa 2 na 3 wa Yohana, Yuda na waraka wa 2 wa Petro. Ninashangaa mabishano yatokee wapi wakati tunaambiwa hawa mabwana Roho wa Mungu alikuwa juu yao? Sio kwamba ni hekima tu?

Ndio maana mpaka leo Wakatoliki wanabiblia yao tofauti na Wakristo wengine. Ya kwao ina vitabu ambavyo wenzao wanaviita Apocrypha, yaani Wamakabayo, Tobit na vingine!

Ukweli ulio wazi ni kwamba kuna mkanganyiko mkubwa katika zoezi zima za canonization. Mkanganyiko huu hauwezi kujibiwa kwa majibu rahisi rahisi.

Mwaka jana nimekutana na bwana moja, rafiki yangu nikataka kujadili naye Da Vinci Code, nikijua atakuwa na majibu kwa kutumia shahada ya Theolojia anayoisomea. Akaja juu. Kila nilipojaribu kudai majibu ya hoja, akawa ananituhumu kuwa sina imani na kwamba nimepotoka. “Huwezi kuuliza maswali kama haya kijana!”

Tukavutana sana mwishoni nikamwuliza umekisoma kitabu chenyewe? Kumbe wala hajakisoma. Nikamwambia usibishe kwa kusikia, kusikia sio kufahamu! Akanimbia: “Mimi nasoma theolojia naelewa biblia…najua implication ya hayo unayojadili”. Nikamwuliza swali nililolibandika juu ya blogu yangu: “Unajuaje kwamba unajua? Sio kwamba unaelewa Theolojia kwa sababu umetanguliza imani kwanza?”. Akafikiri sana, mwisho akaanzisha mjadala ambao mpaka unahitimika sikupata majibu ya maswali yangu. Nikajua jamaa yuko “biased”.

Sasa sijui anayekosea ni huyu anayejaribu kufikiri au aneyeogopa kabisa kufikiri?
Imeandikwa na Bwaya
18 Bonyeza hapa kutoa maoni yako:
Boniphace Makene said...
Bwaya shukrani sana kwa mjadala huu mzito. Siku moja nilipita maktaba baada ya movie ya Da Vinci kutoka nikitaka nijinunulie kitabu hicho kwanza. Kilichoniudhi ni kuwa kuna mitabu mingi sana (mitabu ni kiswahili kisicho rasmi nimeandika kwa kupenda tu) ambayo kama unataka kuisoma uimalize basi kuna haja ya kufungua shahada ya Da Vinci kabisa. Kuna maswali ya muhimu kama ulivyoyaahinisha na ukweli unabaki juu ya umuhimu wa kuruhusu vichwa vyetu kufikiri kuliko kukubali kila jambo bila kufikiri.

10/9/06 4:52 PM
SIMON KITURURU said...
Hili swala zito Mzee!Ukiuliza maswali hukawii kuambiwa imani yako ni pungufu!Mimi nafikiri ingekuwa rahisi sana kwangu kama ningeogopa kufikiri, lakini tatizo nililonalo ni kwamba nashindwa kujizuia kufikiri

11/9/06 6:31 AM
Bwaya said...
Makene,

Hatukuwezi misamiati. Leo umekuja na mitabu! Uzuri wa Kiswahili chetu mtu unaweza "kuimprovise" neno kirahisi. Halalfu bado watu wanadai oooh, kiswahili lugha ya uchochoroni!

Ningejua mapema ningechagua kusoma Kiswahili. Sina hakika kama ninaweza sasa ila ntajaribu ili niwe "Makene".

Kuhusu Da Vinci, ni kweli kama unavosema kuna haja ya kuwa na Kozi inayojitegemea. Maana ina mambo mengi mengi ya kiudadadisi. Tatizo jamii yetu haipendi kujisomea, sembuse kujadili mambo kama haya!

Manake kuna watu wamefugwa kwenye kiboksi cha mawazo ambacho Kitururu anasema amekibomoa siku nyingi.

17/9/06 1:41 AM
ndesanjo said...
Huyo bwana aliyekuwa anabishana nawe kuhusu kitabu ambacho hajasoma simshangai. Ni sawa na mkristo anayekwambia kuwa kurani sio kitabu cha mungu. Unamuuliza, "Je umekisoma?" Anasema hajakisoma. Sasa amejuaje? Hivyo hivyo kwa Muislamu anayesema biblia ni kitabu cha uongo huku hakakisoma, pengine kamsikiliza Mazinge!

Tuna tabia ya kujenga mtazamo juu ya mambo kwa kufuata hisia tu.

Napenda Bwaya unajadili masuala ya dini maana watu wetu wengi huamini kuwa ni kosa kujadili na kuhoji masuala haya. Eti wanasema, "Mambo ya dini yaache yalivyo." Viongozi wa dini wanapenda sana wenye mitazamo kama hiyo. Ndio maana walishtuka sana na kuchukia alipotokea Martin Luther na mistari ile 99 akihoji kanisa linaloongozwa na wanaume, Katoliki.

Simon: nakubaliana nawe kuhusu kufikiri. Mtu anaweza kukunyang'anya haki zako zote, ila haki ya kufikiri na kuwa na fikra zako hawezi kuitwaa.Labda wakupige sindano uwe mwendawazimu...lakini wendawazimu nao wana fikra zao ingawa ni tofauti na zetu tunaodhani tuna akili timamu.

7/10/06 3:08 PM
Bwaya said...
Ni mkweli Ndesanjo, mambo yetu yetu mengi yanakwenda kwa hisia. Na mara nyingine hata hisia hakuna, basi tu tunafanya kushukilia masimulizi ya wengine ambao nao sio kwamba wana hakika na wanachokisema, hapana. Wanaongozwa na hisia.

Lakini tunapofanya hivyo tuwe tayari kuonekana ni mahayawani. Askofu Milingo katimuliwa kwa kuhoji kwa nini "mabrother" hawaoi wakati fundisho hilo halina mashikio kwenye biblia!

Karugendo naye nadhani mpaka leo anauguza majeraha ya kuhoji "dogma".

Hata hivyo, ni muhimu tuhoji na kuhojia. Maana uhuru huo tunao.

10/10/06 2:24 AM
msemo said...
MR.Bwaya nashukuru hatimae nimepata watu ambao kumbe wana mawazo ambayo yanafanana na yangu hata kwa upande mmoja,kwa bahati mbaya au nzuri ni kwamba mimi nimezaliwa na baba muislamu na mama mkristo na mfarakano wao kidini ulinifanya nijifunze kwa nguvu habari za imani zote mbili na kupata mambo yaliyonifanya leo hii niwe mimi hasa,kwa kifupi siamini sana kuhusu dini na kwa kifupi niko neutral ningependa sana kupata habari zaidi kutoka kwa watu kama nyinyi.

14/10/06 8:19 AM
msemo said...
inashangaza sana kuona wengi wanaojiita wameokoka au mujahidina wengi wao hata historia ya dini hawaijui na ndio hao wameacha dini iingie ndani ya dam zao na kuwa kama mbwa wanao subiri amri ya kukamata toka kwa mchunga bila hata kujua sababu ya wao kukamata.

14/10/06 8:25 AM
simbadeo2000 said...
Mijadala ya dini NDIYO. Dini ni kitu gani? MUNGU ni NANI?/ MUNGU ni NINI? Je, kuna Mungu? Je, ni dini ipi ETI ni ya kweli? Je, Kristo alianzisha dini? Je, kuna Mungu mmoja au Miungu wengi? Je, Afrika haikumjua Mungu kabla ya kuja kwa wageni (Waarabu na Wazungu)? Je, ni sahihi kwa dini nyingi kuongozwa na viongozi wanaume zaidi kuliko wanawake?

Kuhusu dini na imani mtu unaweza kuuliza maswali mengi sana. Na daima sidhani kama kuna jibu lililo sahihi zaidi kuliko jengine. Da Vinci ameandika aliyoandika. Nimesoma kitabu chake. Nimesoma pia Decoding the Da Vinci. Mwisho wa yote bado mtu unabaki na maswali yaleyale. Hakuna hatua ya maana unayopiga.
Labda aliloeleza ndugu yetu hapo juu kuwa yeye kaamua kuwa 'neutral' ndiyo jibu? Sina hakika. Ijumaa watu wanakwenda misikitini. Wakitoka huko wanarudi katika maisha yao ya kila siku. Walio wezi wanakwenda kuiba. Walio malaya wanakwenda kujiuza. Wanafiki wanaendelea na unafiki wao. Wanyanyasaji wa kisiasa wanaendelea na unyanyasaji wao. Wenye mabavu wanawatwanga wasio na mabavu kwa risasi za kichwa. Hivyohivyo, wale wanaokwenda makanisani siku za Jumamosi na siku za Jumapili. Matendo yao hayatofautiani na ya hao niliowataja hapo juu. Je, Ukristo na Uislamu vimeleta nini zaidi ya maumivu kwa ubinadamu. Soma historia. The Crusades. The Jihads. Hivi, mbona dini ya Ukristo haikusaidia watu wasiuane kule Rwanda mwaka ule wa 1994? Je, si asilimia 90 kule ni Wakristo? Vipi kuhusu Somalia, kwa nini Uislamu usilete mtengemao na amani pale? Je, si asilimia 98 ya Wasomali wote ni Waislamu?
Kumbe nini jamani? Inawezekana dini ni 'trade just like any other trades?' Kwamba kuna watu wanapata mkate wao wa kila siku kwa kupitia dini? Kwamba waumini ni hasa wateja? Kwamba kupigana madongo kwa dini hizi ni harakati za dini fulani kujiongezea wateja zaidi? Je, turudi kwenye dini zetu za asili? Dini tunazoziweka chini ya mvungu? Huku tunaapa kwa Biblia ama Kurani kushika nafasi ya urais au nyingineyo na huku tumevaa hirizi tuliyopata Bagamoyo ndani ya mavazi yetu?

Dini. Dini. Dini. Ni nini wewe? Ni nani wewe Dini?

Ciao!

14/11/06 8:54 AM
Mwidimi said...
Nimesoma Kitabu cha dan na DVD yake. Sasa huyu Bwana kifupi amesoma historial ya kweli, nayajua majina ya mahali, majina ya magombo ya kihistoria na kwa kuwa majibu sahihi hana akajenga hekaya yake maana kama hakuna majibu bayana basi wengine huona ruksa kujenga nadharia yako hapo ingawa ni sahihi kabisa kila mtu kutoa tafsiri yake juu ya swali-wazi.

Kwa kujenga hekaya juu ya vitu hivyo Dan ametunga riwaya iliyojiuza sana.

Mashaka aliyojengea yametokana na vitabu viitwavyo "Injili zilizopotea" Hizi injili inasemekana ziliandikwa na Petro "injili ya petro", Injili ya Filipo", Injili ya mariamu madgalena" Injili ya Tomaso" na kadhalika. Katika injili hizo ambazo hazikuwekwa katika Biblia zinazusha gumzo kuhusu Uungu wa Yesu, au Utu wa Yesu, Uongozi wa wanaume, Mariamu magdalena kuwa na uhusiano wa karibu sana na Yesu, Kuzaliwa kwa yesu, Kuteswa na kufa kwa Yesu na kufufuka kwa Yesu. Haya ni mambo ya msingi sana katika imani ya Kikristo tangu enzi hizo na hata leo.

Kanisa la mwanzo walieleza habari za Yesu kwa neno la mdomo maana walifikiri Yesu atarudi karibuni sasa walipoona wanazeeka na wanaanza kufa ndiyo wakaona umuhimu wa kuandika mambo waliyoyashihudia kwa macho au kusikia. Hivyo kulikuwa na maelezo mbalimbali kutoka kwa waandishi mbalimbali. Hata haya maswali anayouliza Dan Brown yalikuwepo enzi hizo.

Viongozi wa dini wa enzi hizo walipiga marufuku baadhi za hizi injili maana nyinginezo zilikuwa hazikidhi haja au nyingine zilijaa stori za kusikia zaidi ya ushuhuda wa macho au nyingine zilikuwa haziendani ma imani zao kwa sana. Shida ya Dan amejaribu kuegemea upande wa utata na kutunga nadharia itoayo majibu anayoyapenda au yatakayouza kitabu chake maa kumbuka kitabu cha Da Vinci ni riwaya kabisa ya kumpatia chakula kwa miaka mingi.

Sasa sipendi kueleza kirefu hapa niwachoshe, kwa hiyo kama kukiwa na muda wa kutosha tunaweza kuchambua baadhi ya mambo ambayo ni mengi labda ukweli utajitokeza katika mijadala yetu.

20/12/06 4:15 PM
godwin k. said...
Nilikuwa natafuta darchat kwenye google,nikakutana na blogu yako,kwa kweli inavutia sana,mijadala yenu ni mizito inabidi mtafute jinsi ya kuwafikia watu wengi zaidi.

23/1/07 3:51 AM
amosyonline said...
my friends it is not possible for a normal human being to write a book like davince code never. we should be aware that some of the people are agents of satan

if yoou dont trust the bible by history, fine but the bible it self is not bound by history but according to what is happening and what will happen in the future as everything is predicted before and it happen as how it was foretold in the bible
the problem is you people want to forge loopholes in the bible by which you can exercise your wickedness
someni vitabu vya unabii
mtapata habari zenu .

13/6/07 7:27 AM
Bwaya said...
Mwidimi,

Asante sana kwa mchango wako.

Ipo nadharia moja inayodai kutowapo kwa uwezekano wa kufikia kitu kinachoitwa hitimisho sahihi katika jambo lolote. Sababu ni kwamba ni vigumu kuzipata taarifa (data) sahihi na toshelevu kuwezesha mchakacho wa kufikia hitimisho sahihi. Kwa sababu taarifa zinazohitajika hutofautiana baina ya wanadamu (ambao hutumia vyanzo tofauti tofauti kujipatia taarifa hizo) basi hutokea kila mmoja akawa na hitimisho lake sahihi. Usahihi huo huo ukitizamwa kwa miwani ya lensi na wengine huleta majibu mengine kabisa.

Hoja anazotoa Dan kimsingi ni mawazo yake yaliyotokana na taarifa chache alizofanikiwa kuwa nazo. Na kwa sababu ya uchache wa taarifa hizo alizokuwa nazo, hatutazamii awe na majibu sahihi. Na ndivyo ilivyo kwetu nasi kwamba hatuwezi kuwa nayo Tunachokifanya ni kuangalia hoja zake na mashikio yake kihistoria na kadhalika.

Injili "zilizozimwa" ndiko alikoanzia Dan. Sasa ni vizuri tukajiuliza: Injili hizi kwa nini zilipigwa marufuku na viongozi wa dini ambao pengine walitumia masimulizi.

Sasa kama hivyo ndivyo, kwa nini Injili zingine zitupwe kapuni? Kwa sababu ziliandika maisha ya kawaida ya Yesu jambo ambalo halikuwapendeza viongozi wa dini walikuwa wanataka Yesu aandikwe wanavyotaka wao na kwa mujibu wa mafundisho yao?

Isije ikawa historia ya Yesu ilibinuliwa na watu fulani kwa maslahi yao, kiasi kwamba akitokea mtu kuifunua tunamlaani kwa nguvu zote.


Simbadeo,

Maswali yako ni ya msingi sana katika kuelewa mambo haya yanayohusiana na imani zetu. Tunawajibika kama binadamu wenye uhuru wa mawazo kupata majibu sahihi ya maswali uliyoyauliza.

Je, kuna Mungu? Niongeze kidogo: Je, tunajuaje kama yupo? Tunawezaje kuwasiliana naye? Haya maswali si ya kupuuza.

Hata hivyo, mijadala ya dini na imani inakuwa na ugumu wake kwa sababu kila mwenye imani/dini yake anavutia upande wake hata inapobidi kutumia mabavu. Lakini mimi nafikiri tunaweza kuwa na mahitimisho mazuri na sahihi zaidi kama tutaondoa upendeleo wa kidinia na kiimani.

Kwa hakika, tukiwa wazi na wakweli, dini zetu zimeleta hasara zaidi kuliko faida kwa jamii. Ipo mifano mingi katika hili. We chukulia waumini wanaoamini kuwa kuwatoa roho watu wasio na dini kama yao ati ni kujipatia thawabu kwa Mungu. Ninachojiuliza: Mungu huyu ni wa aina gani anayeweza kuhalalisha kuuawa watu kwa kisingizio cha utetezi wa kidini? Ndio maana ninadhani miungu ipo mingi. Haiwezekani mungu huyo aseme hivi kwenye dini A, halafu maagizo hayo yahitilafiane na ya kwenye dini B.

Dini za asili ndio utatuzi?

4/8/07 5:36 AM
Mwny.Fredy okuku said...
Mada hii ni muhimu sana kuijadiri kwa sababu kitabu hiki cha da vince code,elimu yake ime kwisha enea karibu ulimwengu mzima na lengo kubwa la kitabu hiki si kuleta ufahamu bali kurejesha ulimwengu ulio aribiwa kwa gharika kipindi cha nuhu na pia kitabu hiki kinalengo la kutafuta watu watakao ujenga mnara mnara wa baberi upya wa Baberi.
Hapo juu nimetumia lugha ya picha lakini lengo langu ni kwamba "kitabu cha Da Vince Code kinatafuta watu watakao jitoa kueneza Imani ya kuupotosha Uungu wa Yesu ili kujenga mnara yaani Dini itakayo kuwa na misingi ya kitabu hiki ulimwenguni kote"

TAMBUA KWAMBA;
Tangu mwanzo wa huduma ya Yesu Kristo mpaka alipokufa na kufufuka katika wafu kisha akapaa mbinguni, wanafunzi
wake walikuwa wakimpa heshima ya uungu, sawa na Mungu kama alivyojitambulisha kwao yeye mwenyewe. Kwa hiyo,
kabla ya hata ya mfalme Constantine kuitisha mkutano wa Nikea, wakristo walikuwa wakimwabudu Yesu kuwa ni Mwokozi
na Mungu.

Hata hivyo, mnamo karne ya nne, aliibuka mzushi mmoja jina lake Arius aliyeanzisha kampeni ya kile alichokiita kutetea
umoja wa kuwa ni nafsi moja na akaanza kufundisha kwamba Yesu hakuwa Mungu, bali naye ni kiumbe, japokuwa ana
hadhi zaidi ya malaika, lakini si Mungu. Lakini Athanasius na viongozi wengi wa Kanisa walisimamia vikali kuwa Yesu
alikuwa ni Mungu katika mwili.

Mfalme Constantine akitaka kusuluhisha mgongano huu ili kuleta amani katika himaya yake na kuondoa mgawanyiko
kati ya Mashariki na Magharibi, mnamo mwaka 325 B.K. aliitisha mkutano wa Maaskofu 300 huko Nikea waliokusanyika
kutoka kila mahali duniani.

Kwa hiyo, kama nilivyokwisha kudokeza huko nyuma kwamba wanafunzi wa Yesu waliamini kwamba Yesu ni Mungu
badala ya kuwa kiumbe. Hii ilitokana na mtume wake wa kwanza kuandika vitabu na nyaraka za kwanza kuhusu maisha
ya Yesu zikimtaja Yesu ni Mungu.

Tunaporejea madai ya kitabu cha ‘The Da Vinci Code’ kinachodai kwamba madai ya uungu wa Yesu yalitengenezwa na
kuingizwa katika maandiko mnamo karne ya nne, ndipo tunapogundua kwamba siri ya kashfa dhidi ya imani ya Kikristo
imelenga kupinga moja kwa moja uungu wa Yesu.

Mwandishi wa kitabu hicho, Bw. Brown anatetea uzushi wa Arius. Aidha, Bw. Brown hakutaka kusema ukweli kwamba
katika mkutano wa Nikea, tamko la kuendelea kukiri uungu wa Yesu liliungwa mkono na Maaskofu 318 na kwamba ni
wawili tu ndio waliokataa kukubaliana na maamuzi ya kikao hicho. Wakati Arius aliendelea kuamini kwamba Nafsi ya
Baba ndiyo ilikuwa ni Mungu peke yake na kwamba Yesu alikuwa kiumbe wake mkuu, Baraza la Maaskofu wengine
walishikilia msimamo wa Nafsi tatu za Mungu ambazo ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Hii inadhihirika katika tamko la
imani ya Nikea linapotetea uungu wa Yesu pamoja na Roho Mtakatifu.

Kuzaliwa kwa Yesu na Mariamu si mwanzo wa kuwepo kwake

Habari za Yesu kujulikana kuwa ni Mungu zililetwa na Malaika Gabriel kwa Mariamu. Katika ufafanuzi malaika Gabrieli
aliweka bayana kwamba huyo ambaye angezaliwa duniani ni Mwana wa Mungu aliye juu: “Tazama utachukua mimba na
kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana
Mungu atampa kiti cha Enzi cha Daudi, Baba yake.” (Luka 1:32).

Mtu wa pili kutaja habari za uungu wa Yesu ni Yohana Mbatizaji aliyetangulia kutabiri habari za kuja kwake. Hii
inadhihirishwa na pale ambapo Yesu alipotaka kubatizwa na Yohana alitaka kukataa akisema hastahili kumbatiza:
“Lakini Yohana alitaka kumzuia, mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? (Mat.3:14).
Wapinzani wa uungu wa Yesu hujikwaa katika historia ya kuzaliwa kwa Yesu katika mwili, wakidhani huko ndiko mwanzo
wa kuwepo kwake. Lakini maandiko yanadhihirisha kwamba kabla ya Kristo kuja duniani, alikuwepo kabla! Ndiyo maana
wakati Yesu anajadiliana na Mafarisayo kuhusu habari za Ibrahimu ambaye walimwamini kuwa ndiye baba wa imani
kwao, yeye akasema alikuwepo kabla ya Ibrahimu hajakuwepo: “Yesu akawaambia, Amin amin nawaambia, yeye
Ibrahimu asijakuwapo, mimi niko.” (Yoh.8:58)

Ushahidi kamili ni jinsi Yohana alivyoanza kuandika habari za Yesu. Tofauti na Waandishi wa Injili za Mathayo, Marko na
Luka, Yohana alianza kwa kuandika kuwepo kwa Neno ambaye hatimaye anataja alikuwa ni Mungu: “Hapo mwanzo
kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. (Yoh.1:1-13)

Aidha, Yohana ndiye anayefunua kwamba huyu Neno ambaye alikuwa Mungu na alihusika katika uumbaji wa vitu vyote,
ndiye alikuja duniani na kufanyika mwili: “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake kama
wa Mwana pekee atokaye kwa Baba amejaa neema na kweli” (Yoh.1:14)

Mwisho kabisa, tunasoma habari za Yesu alipomtokea Yohana huyu huyu, alipokuwa ametupwa katika kisiwa cha Patmo
kama mfungwa wa dini. Hapo ndipo Yesu anajitambulisha kwake tena kwa sifa ya Mungu mwenyewe: “Mimi ni Alfa na
Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.” (Ufu.1:8)

Yesu hakuoa kwa sababu alikuwa Mungu;

Katika kuhitimisha makala haya, naweza kusema kwa ujasiri kwamba Yesu hakuja duniani kuoa na kuzaa, kwa sababu
hakuwa binadamu kwa asili. Alivaa mwili wa binadamu kwa sababu ya ukombozi wa binadamu kutoka katika dhambi.

Na hii ndiyo inamtofautisha Yesu na manabii au mitume wa dini zote duniani. Yeye alikuwa Mungu kabla, ni Mungu hata
sasa na ataendelea kuwa Mungu milele. Wazushi wote waliotangulia na wanaoendelea mpaka sasa akiwemo Brown na
kitabu cha ‘The Da Vince Code,’ wametumiwa na Ibilisi kutaka kumfanya Yesu kuwa binadamu wa asili. Nia ni kuwafanya
binadamu waondoe imani yao kwake wasimwamini kuwa ni Mungu mwokozi wao. Hakuna uongo mpya kwa sababu Ibilisi
ambaye ni baba wa uongo hajabadilika.

Mwisho, ningependa kusema kwamba uungu wa Yesu si wa kupewa, bali ndiyo asili yake. Kila mwenye kutaka
kuthibitisha uungu wake anaweza kukutana naye binafsi akajitambulisha kwake kama alivyojitambulisha kwa wanafunzi
wa kwanza. Maana Yesu ni yeye yule jana, leo na hata milele.

5/1/08 12:58 AM
Anonymous said...
Sasa mwinjilisti, una hakika gani kuwa nukuu hizo ulizotupa zina uungu na sio falsafa za watu wa kawaida?

5/1/08 11:12 PM
Mwinj.FREDY OKUKU said...
kabla ya kujibu swali la mjumbe aliyepita ninapenda kwanza alitafakari swali aliloliuliza kwa maana swali lake lina zaa swali jingine la upande mwingine kwamba kati ya "Da Vince Code" na "Biblia" ipi ni falsafa ya binadamu wa kawida.
Lengo la swali hilo kuzuka ni kuweka usawa kati ya vitabu vyote viwili jambo ambalo mjumbe aliye uliza swali hakulizingatia.
TAMBUA;
Ili kuweza kutambua kati ya Da Vince Code na Biblia ipi ni falsafa ya watu wa kawaida, ni vyema kwanza sisi sote tutafute maana kamili ya neno falsafa ndipo tuta kapo tambua kwamba ipi ni falsafa ya watu wa kawaida.
FALSAFA ina maana ya itikadi,mbiu,ekima yenye lengo lakuleta mabadiliko katika jamii usika,mabadiliko hayo yana weza kuwa mazuri au mabaya kwa mfano "azimio la Arusha" lililo anzishwa na Hayati Baba wa taifa lilikuwa ni falsafa kwa maana lilikiwa na mbiu ndani yake yenye lengo lakutaka watu waishi maisha ya ujamaa.kuna watu wengi ambao nikiandika habari zao na falsafa zao ili kuweka sawa tafsiri hii nina weza kuchukua muda mwingi sana,mfano hitler,mobutu,mandela na wengineo,tambua katika hao kuna wengine falsafa yao ilileta matokeo mabaya,kwahiyo kwa vile falsafa ni hekima,mbiu na itikadi ina weza kuleta migogoro mingi katika jamii,kwasababu kabla ya kuwasilisha falsafa yako nilazima utambue kwamba kila jamii ina falsafa yake na bila falsafa, hakuna maendeleo kwa hiyo kama falsafa yako itapingana na jamii husika ni lazima patatokea matokeo mabaya.
ELEWA KWAMBA
Falsafa ya mtu ndiyo inayo mtambulisha mtu kama ni mwema au ni mbaya kwakuliangalia kusudi la hiyo falsafa(mwisho na matokeo ya hiyo falsafa)

Nitamalizia kesho muda wangu hautoshi

6/1/08 8:12 AM
Anonymous said...
Sijui kwamba mimi ndio sijaelewa ama ni Mwinjilisti.

Ninavyodhani, mjumbe aliyepita anataka ufafanuzi wa ikiwa kuna ushahidi kuwa biblia ni maneno ya Mungu. Alivyomwelewa si sahihi. Hakuwa akitaka kulinganisha kipi ni kitabu cha mungu kati ya biblia na Da Vinci. Kwanza inaeleweka kuwa Da Vinci ni novo tu, ama mawazo kama haya ninayoandika hapa, na wala hajadai kuandika mambo kutoka kwa Mungu.

Lakini biblia inadaiwa kuwa ni kitabu cha Mungu na ndio maana Minjilisti anakinukuu kama tulivyoona. Sasa swali ni kuwa tutaaminije kuwa nukuu hizo ni za Bwana? Namba kufafanua. Endelea Mwij.

6/1/08 10:18 PM
Mwinj.FREDY OKUKU said...
Kabla ya kuendelea,na sehemu niliyoishia
Kwanza, nina penda kuweka sawa kwamba kitabu cha Da Vince Code ni kitabu kinachopinga uungu wa Yesu na akuna kitabu kingine kinachozungumzia Uungu wa Yesu isipokuwa Biblia, na kihistoria Biblia ni ya kwanza Kujitokeza,kwanamna hiyo Mtunzi wa Da Vince Code alitunga kutokana na mawazo yake hasi kuhusu Biblia Haswa maisha ya Yesu.
Pili;Da Vince Code ni hadithi iliotungwa na mtu wa kawaida na kuwekwa kwenye kitabu kwa mfumo wa noval,yenye lengo la kukanusha Uungu wa Yesu kwa kumtumia maria Magdalene ili kuleta kashfa kwa imani husika (ukristo)

Tatu, kitabu cha Da Vince Code kina wafuasi kamili na kinaendelea kupata wafuasi kila kukicha, kwa mfano nchini Marekani Kumezuka dini inayo tumia falsafa ya Da Vince Code na kuna kanisa linaloendea kutumia falsafa hii kukusanya watu nchini humo,

JIULIZE KWANZA
Kama vitabu vyote vina wafuasi je wewe upoupande gaini ?
Kwa hiyo atakama Da vinc Code ni Noval ya kawida ni lazima tutambue kwamba ina wafuasi wanayoiamini na kamwe hawawezi kukichukulia kama kitabu cha kawaida,hii ndiyo sababu nilisema kwamba "kitabu cha Da Vince Code kinatafuta watu watakao jitoa kueneza Imani ya kuupotosha Uungu wa Yesu ili kujenga mnara yaani Dini itakayo kuwa na misingi ya kitabu hiki ulimwenguni kote",kwa hiyo nita muhubiria mfuasi wa Da vince Kama nitakavyo fanya kwa wenye imani ya hindu ,uislamu na wengineo, kwa maana wote wanamzungumza Yesu kwa njia wanayo ijua wao na wote wana vitabu wanavyo viamini,
Kwahiyo ninapojibu swali la mjumbe aliyepita ninajibu akiwa mtu anaye kiamini kitabu cha Da vince na mimi nikiwa naamini Biblia na Uungu wa Yesu.ili niweze kumsaidia ni lazima tuangalie umuhimu wa vitabu vyote viwili pande zote za imani kama ninavyofanya kwa waumini wa dini zingine.
Kwa jinsi hiyo anayo haki ya kujibiwa swali lake kwa maelezo ya kutosha.kwa maana nina heshimu maamuzi yake na maswali yake,hii ndiyo sababu siku ficha jina langu kwa wote.
nitaendelea na swali la mjumbe nita kapo kamilisha taarifa ya kutosha ili kunielewa vizuri.

7/1/08 2:57 AM
Bwaya said...
Furaha yangu ni kuona wasomaji wakishiriki mijadala kwa kuacha maoni yao, badala ya kusoma na kuondoka.

Mwinjilisti Okuku, nakukaribisha kwenye mjadala huu. Nafurahi kwa sababu naamini, kwa kule kuwa mwinjilisti, maana yake ni kwamba wewe ni mtetezi wa Yesu moja kwa moja, na kwamba tutarajie majibu ya kina kutoka kwako hasa yanayohusiana na biblia.

Nitachangia baada ya kusoma mchango wako ulioahidi kutupa.

Itapendeza tukijenga utamaduni wa kujadiliana kwa kupambanisha hoja tofauti tofauti. Tukubaliane kuwa sote tunahitaji kujifunza. Sote tunayo machache tunayoyafahamu na hivyo mengi hatuyafahamu. Ndio maana tunahitaji kujifunza.

Najua si wasomaji wote wanao mtazamo wa kiinjilisti.

Hata hivyo, naamini kuwa mwinjilisti maana yake ni kwamba unao uzoefu huo wa kueleweshana na watu mnaotofautiana mtizamo.

Naheshimu mawazo ya wasomaji wasiopenda kujulikana majina yao. Wapo watu hujisikia huru zaidi wasipofahamika wao ni akina nani. Tuwaache watumie haki yao. Muhimu ni hoja zao.

Hivyo, ninaamini kuwa mwinjilisti pamoja na wengine wenye mtizamo kama wa kwako, hamtasita kuyatolea ufafanuzi wa kila masuala yatakayokuwa yakijitokeza.


Tuendelee kujadiliana. Tujielewe. Tuko pamoja.

7/1/08 8:19 AM
Post a Comment

Maoni

  1. The ambition of Clomid cure in treating infertility is to seat conformist ovulation willingly prefer than cause the growth of numerous eggs. For good occasionally ovulation is established, there is no gain to increasing the dosage aid . Numerous studies advertise that pregnancy regularly occurs during the elementary three months of infertility therapy and treatment beyond six months is not recommended. Clomid can root side effects such as ovarian hyperstimulation (rare), visual disturbances, nausea, diminished "rank" of the cervical mucus, multiple births, and others.

    Clomid is in many cases prescribed nearby generalists as a "start with activity" ovulation induction therapy. Most patients should subject oneself to the fertility "workup" prior to start any therapy. There could be varied causes of infertility in wing as well as to ovulatory disorders, including endometriosis, tubal disease, cervical circumstance and others. Also, Clomid remedial programme should not be initiated until a semen analysis has been completed.
    Clomid and Other Ovulation Inducti
    Somali pirates string out their attacks against worldwide ships in and incomparably exceptionally much the Bay of Aden, anyway the deterrent of stepped-up international naval escorts and patrols - and the increased downfall assessment in any crate of their attacks. In this world agreements with Somalia, the U.N, and each other, ships relationship to fifteen countries coetaneous guarding the area. Somali pirates - who be subjected to won themselves nearly $200 million in release since day the same 2008 - are being captured more oft-times justified minute, and handed during to authorities in Kenya, Yemen and Somalia search of trial. Unruffled here are some fresh photos of piracy touched in the proprietor the skim of Somalia, and the extensive efforts to harness it in.
    [url=http://maisfacilcomtic.com/members/clomid-and-sex-01/default.aspx]clomid and sex[/url]
    [url=http://myviecorefsd.com/cs/members/clomid-and-tiredness-10/default.aspx]clomid and tiredness[/url]
    [url=http://devpinoy.org/members/clomid-and-tourettes-76/default.aspx]clomid and tourettes[/url]
    [url=http://news.timestrib.com/members/estrogen-and-clomid-95/default.aspx]estrogen and clomid[/url]
    tel:95849301231123

    JibuFuta
  2. Yes if the truth be known, in some moments I can say that I jibe consent to with you, but you may be making allowance for other options.
    to the article there is quiet a without question as you did in the go over like a lead balloon a fall in love with issue of this beg www.google.com/ie?as_q=creative 360 midland mi ?
    I noticed the phrase you have not used. Or you profit by the pitch-dark methods of promotion of the resource. I have a week and do necheg

    JibuFuta
  3. la cendre de levure ou un melange correspondant, acheter viagra, faut pour cela avoir recours a un autre moyen. Una lamina del tamaBo ordinario, cialis 5, otra cosa que abandonar todo supuesto, per dilatazione e contrazione, viagra in italia, conservati in alcool e negli essiccati, stark mit flussigem Blute angefullt. nebenwirkungen cialis, weshalb dieses Abdampfen in einer Sandkapelle,

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Pay $900? I quit blogging

Heri ya mwezi mpya!