Hebu na tujilinganishe na wenzetu...


TUNAWEZA kulitazama suala la malezi kwa mtazamo mpana zaidi ya sisi binadamu. Kwa sababu sisi ni sehemu ya wanyama, basi nadhani, tunaweza kujifunza kutoka kwa "wenzetu".

Wanyama wengine hawatoi ushirikiano kwa 'watoto' wao baada ya kuwazaa. Kwao, shughuli ya msingi ni kuzaa, kisha watoto huachwa wakizagaa. Kila mmoja hutawanyika kutafuta kinachoweza kumfaa kumwezesha kusogeza siku.

Kwa sababu ya wepesi wa shughuli yenyewe, wanyama wengi huzaa kwa mikupuo mingi.

Chukulia aina nyingi ya samaki ambao 'hulipua' maelfu ya vijisamaki kwa mkupuo huu (mmoja). Mara tu baada ya uzazi, kila samaki hujitafutia maisha yake mwenyewe. Matokeo yake wengi wao hujifilia bila taarifa.

Hali ni hiyo hiyo kwa wanyama wengine wengi.

Lakini jamii kubwa ya ndege imethibitika kuwa na maandalizi kabla ya uamuzi wa kuzaa. Kutengeneza kiota na kadhalika. Na hata baada ya kutotoa mayai, wengi wao wanao uwezo mzuri wa kufuatilia maendeleo ya 'vifaranga' vyao mpaka watakaporidhika na upevukaji wa walichokizaa kwa hiari.

Tunapokuja kwa binadamu, anayejigamba kuwa na akili (utashi) kuliko wenzake tuliwataja, hali ya malezi ikoje? Je, uzao hufanyika katika mazingira gani? Je, uangalizi baada ya kuzaa, huenda mbali kiais gani na kwa sababu gani?

Inaendelea...

Maoni

  1. Kama tungekuwa kama samaki basi katika dunia hii tungekuwa wengi sana. Na hata hivyo si tofauti sana sisi binadamu tunawazaa watoto wetu na kuwatunza na baadaye wanapokuwa na umri wa kuhama , basi wanahamu na kutuacha sisi wazazi kama tulivyokutana.

    JibuFuta
  2. Unyago, kicheni pati na jando, elimu zinazotolewa hulenga hasa maisha ya wawili watakaoishi pamoja.Elimu ya malezi ya watoto watakaozaliwa sina hakika kama inafundishwa.Hili ni tatizo kubwa sana.Kuna makundi mawili makuu ya watoto kwa mtizamo wangu, kuna wale wenye bahati(waliozaliwa ktk familia zinazozingatia makuzi sahii ya watoto.Hawa huwa na mafanikio sana ktk maisha na wasiohitaji nguvu sana kuyatafuta mafanikio) na kuna wale wasio na bahati(hawa ni wale waliozaliwa ktk familia zisizofahamu mbinu na hazizingatii makuzi mazuri ya watoto.Hawa hukua na huchukua mkondo wowote tu wa maisha labda mbaya au mzuri kulingana na mazingira atakayokutana nayo mbali na familia.Kuna wanaoweza kujikwamua ktk bahati mbaya hii na kutambua wanatakiwa kufanya nini na hatimaye kuwa sawa na wale niwaitao wenye bahati. Hapa kujielewa na utambuzi huchukua nafasi kubwa kabisa.)

    JibuFuta
  3. Dada Yasinta,

    kisayansi hata kama tungezaliana kwa wingi unaozidi samaki, bado tusingekuwa wengi. Kadiri wazaliwao/offspring wanavyoongeza, ndivyo ungalizi wa kiuzazi unavyodorora, na kukatisha maisha ya wengi. Mambo yasingebadilika sana.


    Kissima, nimependa maelezo yako. Kwamba sehemu kubwa ya tatizo la malezi ni ukosefu wa maarifa sahihi ya kulea. Elimu hii haitolewi kwa wanandoa, kwa hisia kuwa kulea si jambo la kujifunza sana.

    Matokeo yake ni watoto wengi kuishia wakiambaa-ambaa kama samaki tuliowagusia hapo juu wakitafuta majaaliwa ya wapi pa kwenda.

    Tunaihitaji elimu hii kwa gharama zozote zilizo halali.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Pay $900? I quit blogging

Heri ya mwezi mpya!