Ulionao ni watoto au mitoto?

“Wenzangu nyie mnafanyaje watoto wawasikilize?” analalamika mama Rehema. “Hata sijui nilimkosea nini Mungu! Hii niliyonayo ni mitoto.” Namuuliza kwa nini? Kama mtu asiyeamini anaulizwa swali la kijinga ananijibu: “Haina akli, mijinga, mitundu, mikorofi, pasua kichwa kazi kunitia hasara tu,” anasema kwa hasira. Kanisimuliza juzi kwenye mtihani wa nusu muhula mwanae mkubwa kawa wa thelathini na nane kati ya watoto arobaini darasani mtihani. “Huwezi amini hata sijashangaa. Mtoto wa Asha kapata A anawaongozea darasani!” Kwa muda mfupi niliokaa pale kwake, watoto ni kama watumwa ni mwendo wa kelele na amri kwenda mbele. “Mama Rehema si ungerekodi tu amri ziwe zinatokea kwenye spika?” namwambia kwa kejeli baada ya kuona anatumia nguvu kubwa kutoa amri zile zile. “Rehema! Unafanya nini?” “Samweli? Hujanisikia?” “We Rehema uko wapi hebu njoo nipe rimoti” Mama Rehema anawakilisha tabia zetu wazazi wengi. Ingawa tunawaita ...