Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia June, 2017

Tusimhukumu Mtoto Mjamzito kwa Makosa Yetu Wenyewe

Picha
Matukio ya watoto wa kike kupata ujauzito yanaongezeka. Kwa mujibu wa Takwimu za Elimu (BEST) wanafunzi 4,718 wa sekondari kwa mwaka 2012 na 3,439 mwaka 2015 walikatishwa masomo yao kwa sababu ya ujauzito. Takwimu kamili hazipatikani lakini kwa elimu ya msingi hali haina tofauti kubwa. Hata hivyo, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) linadai kwamba msichana mmoja kati ya sita wenye umri wa miaka 15 mpaka 19 wakiwemo wasiokuwepo shuleni hupata ujauzito kila mwaka hapa nchini. Ni wazi kuwa mimba za utotoni ni tatizo kubwa katika jamii yetu.

Namna Bora ya Kuwasiliana na Wafanyakazi Unaowaongoza

Picha
Maisha ya kazi kwa kiasi kikubwa ni mawasiliano. Karibu kila tunachokifanya kazini ni kuwasiliana. Tunawasiliana na wateja. Tunawasiliana na wakubwa wa kazi. Tunawasiliana na walio chini yetu. Kwa ujumla kazi ni mtiririko wa mawasiliano.

Ukitaka Kuaminiwa Jenga Mazingira ya Kuaminika

Picha
“Nina mke asiyeniamini kabisa,” aliniambia bwana mmoja hivi majuzi. “Hana imani kabisa na mimi.  Juzi kati hapa nimemkuta anachunguza simu yangu. Tuligombana sana.” Nilimwuliza kwa nini anafikiri mke wake hamwamini. “Basi tu ndivyo alivyo. Hata ufanyaje hana imani.”

Mabadiliko ya Kijamii Yanavyoathiri Malezi -1

Picha
TUNAISHI katika nyakati ambazo maarifa kuhusu malezi ya watoto vinapewa umuhimu. Sambamba na ongezeko la mijadala ya malezi katika majukwaa mbalimbali, malezi yamevutia hisia za watafiti wengi kuliko ilivyopata kuwa. Kila siku, kwa mfano, zinachapishwa tafiti nyingi kuchunguza changamoto za malezi ya watoto.

Mambo Yanayokuza Motisha kwa Wafanyakazi

Picha
Pengine umewahi kufanya kitu kwa sababu tu ulilazimika kukifanya. Moyoni hukusikia msukumo wowote isipokuwa hofu ya kushindwa kufikia matarajio ya mtu mwingine. Lakini pia inawezekana umewahi kufanya kitu bila kusukumwa wala kufuatiliwa. Ndani yako unakuwa na furaha na msukumo unaokuhamasisha kutekeleza jambo si kwa sababu ya hofu iliyotengenezwa na wengine bali shauku ya kufikia kiwango kinachokupa kuridhika.