Je, Shule za Bweni Zinafaa kwa Malezi ya Watoto Wadogo?

PICHA: SOS Schools Ongezeko kubwa la shule za bweni kwa watoto wadogo ni kiashiria kimoja wapo cha mabadiliko ya kijamii yanayoendelea kuathiri desturi za malezi. Pamoja na changamoto zake, mzazi anapofanya maamuzi ya kumpeleka mwanae shule ya bweni huamini anafanya hivyo kwa faida ya mtoto.