Kuuishi Wito Wako, Unahitaji Nidhamu ya Kujifunza

PICHA: findingmastery.net/ Nimekutana na vijana wengi wanaotaka niwaonyeshe njia ya mkato ya kufanya kazi za ndoto zao. Wanafikiri kupata kazi inayoendana na vipaji na tabia zao ni jambo la siku moja. Ingawa huwa ninawasaidia kujiuliza maswali ya msingi yanayowachochea kugundua hazina iliyolala ndani yao, bado husisitiza umuhimu wa kuwa na mtazamo mrefu wa kuona yasiyoonekana kwa macho. Nitatumia mfano wa Robert Green, mwandishi nimpendaye aliyeandika vitabu maarufu vya ‘The 48 Laws of Power, ‘Mastery’ na ‘The Art of Seduction.’ Ingawa tangu akiwa mdogo aligundua alitaka kuwa mwandishi, Robert hakuwa na uhakika anataka kuandika masuala gani. Baada ya kumaliza chuo, Robert alianza kufanya kazi kama mwandishi wa habari. Kazi hiyo, hata hivyo, haikumwendea vizuri. Mhariri wake alimshauri, ‘Tafuta kazi nyingine ya kufanya. Wewe si mwandishi. Hujui kupangilia mawazo yakaeleweka. Nakushauri ukatafute maisha mengine.” Robert anasema alijisikia vibaya kwa ...