Umewahi kujiuliza kwa nini, wakati mwingine, mtu mwenye akili nzuri, mwenye weledi na uelewa mpana wa mambo, hujikuta na majanga mengi linapokuja suala la namna anavyoishi na watu? Shida ni nini? Iweje mtu aelewe mambo mengine vizuri lakini asindwe mambo madogo kama kuwa msikivu, mvumilivu wa mawazo tofauti, mwenye subira hali inayoweza kumuingiza kwenye magomvi na watu? Kinyume na tunavyoamini wengi wetu, hisia hubeba maamuzi yetu mengi na ukitazama matatizo yetu mengi ya kitabia unaweza kuona mchango mkubwa wa kushindwa kuzielewa na kuzimudu hisia zetu. Ingawa tunazipuuza, ukweli ni kwamba ukishashindwa kuzishughulikia hisia zako, uwezekano wa kukabiliana na matatizo mengi ya kimtazamo, kimaamuzi na kitabia unakuwa mkubwa. Hapa ninakuletea, japo kwa mukhtasari, elimu ya hisia, UmahiriHisia (UH) — emotional intelligence — ambao kimsingi ni uwezo kuelewa namna hisia zetu zinavyofanya kazi, kuzitambua kadri zinavyoitokeza, kuelewa nini kinazichochea, kuzirekeb...
Bwaya, hapa umenichekesha sana. Nimejaribu kutafakari, nikaona ya kuwa wote wapo sawa tu. Ha ha haaa
JibuFuta