Umewahi kujiuliza kwa nini, wakati mwingine, mtu mwenye akili nzuri, mwenye weledi na uelewa mpana wa mambo, hujikuta na majanga mengi linapokuja suala la namna anavyoishi na watu? Shida ni nini? Iweje mtu aelewe mambo mengine vizuri lakini asindwe mambo madogo kama kuwa msikivu, mvumilivu wa mawazo tofauti, mwenye subira hali inayoweza kumuingiza kwenye magomvi na watu? Wengine tunafikiri tuna misimamo mikali, tumenyoooka na hatujali kutofautiana na nani lakini ukitazama vizuri hiyo inayoitwa misimamo mikali ni changamoto za kihisia, uwezo mdogo wa kuelewa mitazamo ya wengine, na saa nyingine ni kiburi tu kuwa tunajua kuliko wengine, hawana wanachoweza kutuambia na kadhalika. Kinyume na tunavyoamini wengi wetu, hisia hubeba maamuzi yetu mengi na ukitazama matatizo yetu mengi ya kitabia unaweza kuona mchango mkubwa wa kushindwa kuzielewa na kuzimudu hisia zetu. Ingawa tunazipuuza, ukweli ni kwamba ukishashindwa kuzishughulikia hisia zako, uwezekano wa kukabiliana na matatizo...
Heri kwako pia Mkuu!
JibuFutaHeri nawe pia mwana mpotevu.
JibuFuta@Baba Mtakatifu, asante!
JibuFuta@Yasinta, nimerudi!