Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

SAIKOLOJIA, neno lililotoholewa kutoka neno la kiingereza psychology, si elimu inayoeleweka sana katika jamii yetu. Asili ya 'psychology' ni neno 'psyche' lenye maana ya nafsi. Katika makala haya, tunasaili kwa ufupi maana ya saikolojia kama taaluma na kuonesha nafasi ya taaluma hiyo ngeni katika jamii yetu katika kutatua matatizo ya kijamii na hivyo kuharakisha juhudi za watu kujiletea maendeleo yetu.

Saikolojia ni nini?

Neno kuu linalobeba dhana ya saikolojia ni tabia. Tunapozungumzia tabia, tuna maana ya matendo, miitikio au mienendo inayoweza kuonekana wazi, kupimwa na hata kuchunguzika kwa kufuata misingi ya kisayansi. Kwa maana hiyo, saikolojia ni sayansi ya kuchunguza tabia, mitazamo, imani walizonazo watu na namna inavyoathiri wayatendayo.

Upo uhusiano wa karibu kati ya mitazamo na imani zisizoonekana na tabia inayoonekana. Hasira ni tabia kwa sababu kwanza, ni kitendo kinachoweza kuonekana bayana kwa macho kupitia yanayofanywa na mwenye hasira, na hivyo inaweza kupimwa kisayansi kwa kufuatilia vitendo vinavyoonesha hasira ili kuweza kufanyiwa utafiti unaokubalika. Maelezo hayo hayo yanaweza kutumika kuelezea tabia yoyote kama vile kupenda, kunyanyapaa na kadhalika kwa sababu, vyote kwa pamoja, vinaonekana, vinapimika na vinachunguzika kwa kufuata kanuni za kisayansi.

Kwa nini unaona unachokiona kwenye picha hii? Picha: serc.carleton.edu

Ingawa msingi wa tabia yoyote ni mawazo, imani, fikra, mitazamo isiyoonekana, lakini ni wazi kuwa yote hayo hujidhihirisha kwa yake tunayoyafanya dhahiri. Hii ndio kusema kwamba yanayoendelea kwenye ufahamu wa mtu (uelewa) ambayo ni mkusanyiko wa dhana, maarifa, imani, mitazamo aliyonayo mtu huyo, huonekana kwa matendo yanayoonekana bayana kwa jinsi ya tabia. 

Kwa hiyo, tunapozungumzia saikolojia, kimsingi tunazungumzia msingi wa tabia zetu na jinsi tabia hizo zinavyojiumba kwa maana ya namna zinavyoanzia mbali kwenye ufahamu kisha kuhamia kwenye mitazamo ambayo ndiyo huzaa matendo yanayoonekana na ambayo tunayaita tabia.Tabia hii, kama tulivyoona, huchunguzwa kwa kutumia majaribio ya kisayansi na wala sio hisia, maoni au bashiri za kimazoea.

Historia na maendeleo ya elimu ya saikolojia

Safari ya maendeleo ya elimu ya saikolojia imetegemea kwa kiasi kikubwa namna tabia inavyotazamwa kwa maana ya chanzo chake na jinsi  inavyoweza kubadilishwa. Wakati Saikolojia inaanza miaka ya nyuma, iliaminika kuwa  ni elimu ya mambo ya nafsi ambayo kwa hakika hayaonekani kwa macho. Hivyo, wanasaikolojia wa mwanzo walitumia muda mwingi kuchunguza nafsi msisitizo ukiwa katika mahusiano ya tabia na nguvu zilizo nje ya uwezo wa mwanadamu kwa kutumia uzoefu. Mfano, ungeenda kwa mwanasaikolojia na akakusaidia kujitambua kwa kutumia ndoto unazoota mara kwa mara.

Waliamini kuwa tabia hujiumba pasipo jitihada za mwanadamu na hivyo mwanadamu hana uwezo wa kudhibiti wala kubadili tabia yake. Kutokana na hayo wanasaikolojia wa mwanzo walijikuta wakifanya shughuli zisizotofautiana sana na falsafa (speculations) na wanajimu kwa sababu ya mbinu zisizo na misingi yoyote kwenye sayansi na utafiti.

Lakini baadae, elimu hii iliendelea kukua na wanasaikolojia wakaanza kuhusisha mazingira anamokulia mtu na tabia yake. Tabia ilichukuliwa kama matokeo ya kujifunza na hivyo ingeweza kudhibitika na hata kubadilishwa. Kujifunza hutokana na ama namna matendo yetu yanavyoleta matokeo chanya au yanayotuathiri ikiwa na maana tabia inayoambatana na matokeo chanya hukua na kuendelea wakati tabia inayoendana na matokeo hasi hufifia na kupotea. Ili kufahamu matokeo ya matendo/tabia fulani, ni lazima tabia hiyo ionekane na ipimike tofauti na ilivyokuwa katika mtazamo wa awali. Hii ilikuwa ni hatua kubwa katika kuanza kwa tafiti za kisayansi zinazohusu tabia.

Hata hivyo, pamoja na maendeleo hayo, bado yalikuwepo mashaka ya namna mazingira yanaweza kuongoza tabia ya mwanadamu mwenye utashi. Ndipo baadae, saikolojia ikaanza kutazama kwa kina uhusiano wa utashi na mazingira anamokulia mtu katika kujenga tabia. Kwamba pamoja na tabia ya kuathiriwa na mazingira, bado utashi binafsi unaweza kuamua muundo wa tabia husika.

Kwa sasa, mtazamo unaotawala elimu ya saikolojia ni namna utashi, mtazamo na mazingira unavyoathiri tabia na jinsi tabia hali kadhalika inavyoathiri utashi, mtazamo na mazingira ya kijamii. Athari hizo zinazotegemeana kati ya mawazo, uelewa, mitazamo na mazingira ya kijamii huchunguzwa kwa kufuata kanuni za tafiti za kisayansi ambazo mara nyingi hufanyikia maabara.

Malengo makuu ya Saikolojia

Saikolojia ina malengo makuu manne. Moja, ni kuchungua vyanzo vya tabia zetu. Hapa tuna maana ya kujaribu kujua mazingira yapi hasa yanachangia kutengeneza tabia alizonazo binadamu. Pili, kuelezea tabia zetu kwa maana ya kufafanua kwa nini binadamu kuwa na tabia alizonazo. Mfano, kwa nini binadamu hukasirika na wakati mwingine hufurahi.

Tatu, kubashiri tabia ya baadae atakayokuwa nayo binadamu. Kwa kutumia uelewa mpana wa tabia, mwanasaikolojia anaweza kukadiria ni wakati gani na mazingira yapi tabia fulani inaweza kujitokeza. Kwa mfano, tunaweza kuelewa katika umri upi, binadamu anaweza kuonesha tabia fulani ambazo hazijajitokeza kwa sasa. Mwisho, ni kusaidia kudhibiti/kubadili tabia. Hapa tunazungumzia namna gani tunaweza kuwasaidia watu wenye tabia fulani kubadili tabia zao. Ili hayo yawezekane tunahitaji uelewa mpana wa chanzo na mazingira yanayoongoza tabia zetu.

Soma sehemu ya pili ya makala haya hapa.

Mwandishi wa makala ni Mhadhiri Msaidizi wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU). Anapatikana kwa barua pepe: bwaya@mwecau.ac.tz

Maoni

  1. Wataalamu mbalimbali wanazungumziaje saikolojia ya elimu?

    JibuFuta
  2. PROAKUN.WIN | AGEN BANDARQ | QQ ONLINE | DOMINOQQ | BANDARQ ONLINE | JUDI ONLINE TERBAIK DI INDONESIA, adalah Website Rekomendasi Situs Situs Terbaik dan Ternama dengan Hasil Winrate Teringgi Terbaik Di Indonesia.

    Agen BandarQ
    QQ Online
    DominoQQ
    BandarQ Online
    Judi Online

    JibuFuta
  3. Nashukur sn kwa ufafanuz huo kuhusu saikolojia kwa jumla, ila binafs katika maisha yang nimekua najitafuta mimi ni nan haswa na ninaweza nini ambacho Mungu amekiweka ndan yang,baada yankuchukua muda mrefu na kusoma vitabu vya kunisaidia kujitambua nimekuja kujielewa nina kipawa katika eneo la kua Mwanasaikolojia na mshaur ,kwa sifa izi Mzuri katika kuongea navutia kwa maneno na watu kupendezwa, Nafanya mambo kwa ubora sana pale ninapokua mwenyewe, Najitambua sana mwenyewe (udhaifu wang,nguvu zang n.k),Napenda Kukaa peke yangu na kutafakari mambo mwenyewe,sipendi kujichanganya sana na watu, Napenda kujifunza kuhusu tabia zang,madhaifu yang,na uwezo wang,Napenda kujifunza mambo yanayoisumbua jamii/wat na kupenda kuyatatua Mfano kama mt anasumbuliwa na kit,au wat wamekata tamaa juu ya jambo fulan,Napenda kujiajiri, Spendi kuajiriwa,Spendi kuamrishwa,Spendi kutumwa, Spendi kupelekeshwa na maagizo, Niko makin sana na hisia zang na mara nyingi nipo kivyangu vyangu na nipo bize na mambo yangu,Spendi kuwa kwenye vikundi na hata kwenye mazungumzo huwa spendi kuchangia, naamin katika kufanya mambo mwenyewe .Izo ni sifa nilizonazo. Kitu kikubwa nachotaka sasa ni kukitengeneza icho kipawa changu na kukitumia, ivo naomba msaada wa njia ,mbinu na namna ntakavoweza kukamilisha hii ndoto hiyo.Naitwa Bilal Rajab, Dar ,mawasiliano yangu 0683-834534

    JibuFuta
  4. nashkuru kw kuelew vzr

    JibuFuta
  5. 55gaga āļāļēāļĢāđ€āļ”ิāļ™āļ‡āļēāļ™āļ•āļēāļĄāļŠูāļ•āļĢāļšāļēāļ„āļēāļĢ่āļēāļˆāļ°āļĢāļēāļ§āļāļēāļĢāđ€āļšāļēāđ†āđ€āļžิ่āļĄāđ€āļ‡ิāļ™ pg slot āđ€āļžื่āļ­āļ„āļ­āļĒāļ—ี่āļˆāļ°āļ™āļģāđ„āļ›āļžāļ™ัāļ™āđāļĨāļāđ€āļ‡ิāļ™āļ้āļ­āļ™āļ—ี่āđƒāļŦāļ่āļĄāļēāļāļĒิ่āļ‡āļāļ§่āļē āļžāļ§āļāđ€āļĢāļēāļŠāļēāļĄāļēāļĢāļ–āļžāļ™ัāļ™ āļšāļēāļ„āļēāļĢ่āļē āđ„āļ”้āđ€āļžีāļĒāļ‡āđāļ„่ 1 āļŦāļ™่āļ§āļĒāđƒāļ™āļŦāļ™āđāļĢāļ āļ—ี่āđ€āļ”ีāļĒāļ§

    JibuFuta
  6. pg slot āđ€āļ§็āļšāļ•āļĢāļ‡āļ­ัāļ™āļ”ัāļš 1 āđ€āļĄื่āļ­āļžูāļ”āļ–ึāļ‡āļ„āļ§āļēāļĄāļšัāļ™āđ€āļ—ิāļ‡āļ­āļ­āļ™āđ„āļĨāļ™์ āđ„āļĄ่āļŠāļēāļĄāļēāļĢāļ–āļ—ี่āļˆāļ°āđ„āļĄ่āļžูāļ”āļ–ึāļ‡āļŠāļĨ็āļ­āļ•āļ­āļ­āļ™āđ„āļĨāļ™์āđ„āļ”้ PGSLOT āđ€āļāļĄāļŠāļĨ็āļ­āļ•āđ„āļ”้āļāļĨāļēāļĒāđ€āļ›็āļ™āļŦāļ™ึ่āļ‡āđƒāļ™āđ€āļāļĄāļ„āļēāļŠิāđ‚āļ™āļ—ี่āļ™ิāļĒāļĄāđāļĨāļ°āđ€āļ›็āļ™āļ—ี่āļ™ิāļĒāļĄāļĄāļēāļāļ—ี่āļŠุāļ”āđƒāļ™āļĒุāļ„āļ›ัāļˆāļˆุāļšัāļ™āļ™ี้

    JibuFuta
  7. Kwa nn wt wanakuwa na IQ kubwa na wengine wanakuwa na ndogo why? Please help me to understand reason

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Kikao cha tathmini na mipango ya familia

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?