Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2014

Mtoto ni nani?

Picha
Sheria na mikataba mbalimbali inayozungumzia huduma na haki za mtoto, inamtambulisha mtoto kama mtu yeyote mwenye umri wa miaka chini ya 18. Hata hivyo, kutumia umri kama msingi wa tafsiri ya utoto hakuwezi kutusaidia kujua kwa nini mtu mwenye umri huo aitwe mtoto. Katika makala haya, ningependa tumtazame mtoto kwa kuangalia mitazamo tofauti katika jitihada za kumtofautisha mtoto na mtu ‘mzima’ bila kutumia idadi ya miaka kama msingi mkuu.

‘Hakuna uhusiano wa elimu ya mzazi na ubora wa malezi’ –watafiti

Picha
IMEJENGEKA dhana kwamba kiwango kikubwa cha elimu anachokuwa nacho mzazi kinaamaanisha ubora na ufanisi wa malezi. Katika nchi za ki-Magharibi kwa mfano, ubora wa malezi kwa maana ya uelewa wa mahitaji ya kisaikolojia ya mtoto umekuwa ukihusishwa na elimu ya wazazi inayokwenda sambamba na uwajibikaji wa kimalezi. Hali inaonekana kuwa tofauti katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. 

Kwa nini ni rahisi kumsifia mtu akifa kuliko akiwa hai?

Picha
Hatupendi kuwasifu wengine wala kusikia wakisifiwa na wengine, lakini ni wepesi sana kumsifia marehemu. Na ni nadra kusikia tabia ya marehemu ikikosolewa. Hata waliokuwa hawamsifii akiwa hai, huomba fursa ya kuusemea vizuri wasifu wa mpendwa aliyetutoka. Mtu fulani maarufu akifa, kwa mfano, watu ambao hata siku moja hawakuwahi kumsema marehemu enzi za uhai wake, ndio huanza kushindana kutundika picha zake zikiambatana na maneno ya ‘apumzike kwa amani’. Sasa swali, kwa nini ni vyepesi kumsifia marehemu asiyesikia kuliko kumsifia binadamu anayesikia?

Unaanzisha mahusiano ya ndoa/mapenzi?

Picha
MAZUNGUMZO mengi yanayohusu maandalizi ya ndoa hujikita katika kufanikisha tukio la siku ya harusi. Na wakati mwingine wanaojiandaa kwa ndoa huandaliwa siku chache sana kabla ya tukio hilo. Kwa ujumla, suala la ndoa limerahisishwa kiasi cha kuonekana kuwa yeyote anaweza kukabiliana nalo kwa uzoefu pasipo maandalizi ya kutosha. Hata hivyo, pamoja na wepesi wa maandalizi halisi, na msisitizo uliowekwa na jamii katika 'siku ya harusi', ndoa nyingi huishia kwenye migogoro mingi muda mfupi baada ya tukio la harusi.

Malezi yanayofanya mtoto amsikilize na kumwamini mzazi

Picha
TAFITI zinaonesha kwamba watoto wengi   ni 'mayatima' wenye wazazi tunaoishi lakini hatupo kwenye maisha yao. Wazazi tupo lakini hatuna muda wa kujua hisia zao, fadhaa zao, maoni yao, hofu zao na hata matumaini yao. Aidha, tafiti hizo hizo zinasema wazazi wengi tunatumia muda mwingi na watoto wetu ama kuwaonya, kuwakosoa ama kuwapa hotuba/maagizo ya ‘fanya hivi, acha hiki’ kuliko tunavyowasaidia kujenga mahusiano ya moja kwa moja kati yetu na watoto.