Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2009

Rafiki yangu wa ujanani...

Nasikitika mwezi huu umekuwa mzurimbaya. Kwanza nilivinjari miji kadhaa hapa nchini nikakutana na watu wa namna mbalimbali. Hiyo ilikuwa nzuri sana kwangu kwa mwezi huu. Hata hivyo, uzuri huo ukasababisha ubaya mwingine. Sikuweza kuwa mwandikaji mzuri. Hayo mawili. La tatu zuribaya, ni hili. Mara nyingine nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali kupitia simu ya kiganjani. Imenisaidia mara nyingi hasa nikiwa barabarani. Bahati nzuri juzi nikiwa kwenye usafiri wa daladala kuna 'tukio la mzunguko wa kiuchumi' lilitokea, simu yangu niliyoipenda sana, ikawa imependwa zaidi na mtumiaji mwingine nisiyemfahamu. Bila shaka inamsaidia huko alipo japo hakuniarifu wakati anaichukua, lakini inavyoonekana aliihitaji kuliko mimi. Akaondoka na majina ya watu wangu kwenye simu yangu ambao nsingependa kuwapoteza. Bahati nzuri wakati nakaribia kabisa kuipoteza simu hiyo, nilikuwa nimetoka tu kuwasiliana na rafiki yangu wa ujanani niliyepotezana naye kwa miaka kadhaa. Nilisoma naye madaras

Tuzo kwa wataalamu je?

TUMEKUWA tukishuhudia, si mara moja, vyombo vya habari vikitangaza 'tuzo' za kuwaenzi wasanii wetu. Ni habari njema kwamba utolewaji huo wa tuzo hushabikiwa mno na hadhira ya Watanzania kiasi cha kuweza kuyashawishi makapuni makubwa makubwa kudhamini tuzo hizo kifedha. Hilo ni jambo jema. Laiti kasi hii hii tunayoiona katika usanii ingesambaa kwenye maeneo mengine. Hivi ingekuwaje kama tungeamua kuwaenzi na watu wengine walioweza kuonyesha juhudi za kufanya tafiti muhimu za kitaaluma? Ingekuwaje kama serikali ingekuwa na, kwa mfano, siku maalumu ya kuwapa tuzo wasomi waliobobea ama wataalamu walioweza kuleta changamoto muhimu kwenye jamii? Ingekuwaje kama makampuni makubwa makubwa haya haya tunayoyaona kwenye 'usanii' nayo yangeamua kushabikia wanazuoni? Tungekuwa na kwa mfano, tuzo ya mtafiti bora wa mwaka; ama daktari bora wa mwaka; ama mwanasayansi bora wa mwaka; ama mwalimu bora wa mwaka; ama mwandishi bora wa vitabu wa mwaka; na kadhalika na kadhalika.

Mtandao unapokuwa wa manati...

Nilikuwa safarini kwa kama majuma mawili hivi. Kuna "tupicha tuwili tutatu" nimekuwa nikijaribu kutubandika humu bila mafanikio. Jitihada za kugundua kikwazo hiki kimetokana na nini zinaendelea. Ila walau kwa sasa nadhani ni haya mambo ya mtandao wa kuunga na kamba za katani. Tunablogu katika mazingira magumu saa nyingine. Unapobofya mara nyingine unalazimika kuendelea na shughuli nyingine, wakati ukisubiri kiungo kifunguke! Hapo hujaoongelea kupandisha picha. Lol... Haya nisilalamike sana. Haya ndio maisha ya watanzania tulio wengi.

Nuru anakuuliza: "...Sura yako hasa ni ipi?"

Kuna kitu ambacho huwa ninajiuliza kila mara, hivi mimi sura yangu ni ipi? Huwezi ukakubali kwa haraka hadi utakapojifanyia uchunguzi ndipo utakapogundua hauna sura moja. Unapokuwa unaongea na mpenzi wako unakuwa na sura gani? Unapokuwa unaongea na wazazi wako unakuwa na sura gani? Unapokuwa umefurahi unakuwa na sura gani? Unapokuwa umekasirika unakuwa nasura gani? Unapoongea na bosi wako Je? Unapoandika email au kuchangia maoni je? Haya ni maswali ambayo huwa ninajiuliza mara kwa mara. Je sura yangu ni ipi na nifanye nini ili niijue sura yangu halisi? (c) Nuru Shabani, 2009

Nimemkuta Prof. Mbele Arusha

Picha
Awali kuna rafiki yangu aliniambia. Nilipofika Arusha wiki hii na kupita pita kwenye maduka ya vitabu, nikakutana uso kwa uso na kitabu cha Prof. Mbele, "Africans and Americans: Embracing Cultural Differences". Pale KIMAHAMA mkabala na Golden Rose kinauzwa bei nafuu Tsh. 15,000. Kwa wadau wa Arusha, mnaweza kujipatia kitabu hicho pale mjionee wenyewe.