Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2006

Tatizo ni dini au watu wenyewe?

Nimefuatilia kwa makini mjadala ulianzishwa na Idya Nkya kwenye blogu yake kuhusu dini. Nimesoma michango ya wanafalsafa waliochangia. Majadala ni mkali na unatia changamoto kweli. Nilivutiwa kuundeleza mjadala huu chumbani hapa chuoni na ilikuwa ni kasheshe tupu tulipokuwa tukijadili suala hili. Mjadala ulikolezwa na mistari ya Ndesanjo inayokwenda kwa jina la Yesu/Isa na watanzania , Mtu ni utu si dini na nyinginezo nilizozitoa pembezoni mwa kibaraza chake upande wa kulia. Dini nyingi tulizobebeshwa (tulizozishika?) zina mafundisho mazuri. Zinatufundisha kuwa watu wazuri katika jamii. Zina makatazo mengi ambayo kimsingi yanalenga kutuchonga tuwe jamii yenye watu waungwana, wastaarabu ambao hatimaye wanaahidiwa maisha ya umilele. (Jambo zuri hili!) Dini zote lengo lake ndilo hilo. Pamoja na kwamba Ndesanjo ana wasi wasi na baadhi ya mafundisho ya dini hizo. Lakini ningependa kuamini kuwa dini zote (nyingi)maudhui yake yanashahibiana na yana faida yakifanyiwa kazi. Tofauti kubwa ni n