Tatizo ni dini au watu wenyewe?

Nimefuatilia kwa makini mjadala ulianzishwa na Idya Nkya kwenye blogu yake kuhusu dini. Nimesoma michango ya wanafalsafa waliochangia. Majadala ni mkali na unatia changamoto kweli.

Nilivutiwa kuundeleza mjadala huu chumbani hapa chuoni na ilikuwa ni kasheshe tupu tulipokuwa tukijadili suala hili. Mjadala ulikolezwa na mistari ya Ndesanjo inayokwenda kwa jina la Yesu/Isa na watanzania, Mtu ni utu si dini na nyinginezo nilizozitoa pembezoni mwa kibaraza chake upande wa kulia.

Dini nyingi tulizobebeshwa (tulizozishika?) zina mafundisho mazuri. Zinatufundisha kuwa watu wazuri katika jamii. Zina makatazo mengi ambayo kimsingi yanalenga kutuchonga tuwe jamii yenye watu waungwana, wastaarabu ambao hatimaye wanaahidiwa maisha ya umilele. (Jambo zuri hili!)

Dini zote lengo lake ndilo hilo. Pamoja na kwamba Ndesanjo ana wasi wasi na baadhi ya mafundisho ya dini hizo. Lakini ningependa kuamini kuwa dini zote (nyingi)maudhui yake yanashahibiana na yana faida yakifanyiwa kazi. Tofauti kubwa ni namna ya kuwa na maadili hayo. Hapo ndo tofauti inaanzia.

Wapo walioshikilia kuwa si muhimu kuwa na utitiri wa "madini" haya yanayopingana kiimani. Kwamba yanachochea tofauti zisizo za msingi katika jamii zetu. Ndio maana watu wanafikia hata kuulizana imani zao. Dini! dini! dini! Iwe kwenye siasa na kwingineko. (Mimi mwenyewe niliwahi kumwuliza Ndesanjo kuhusu dini yake)

Ninachojiuliza hivi sasa, ni kwamba tatizo ni nini, watu au dini zenyewe? Tatizo ni kutokushika mafundisho ya dini husika, au ni uwapo wa dini zenyewe? Hivi zinaweza kuwa ni ubatili mtupu au tatizo liko wapi? Je zisingekuwapo? Ni afadhali kutokuwa na dini kabisa? eti?

Maoni

  1. Dear friends,
    I want to share with you about Audio Bible (http://www.biblegateway.com/resources/audio), Sometimes it could so hard to read on your own from the bible but the solution is here just about your finger tips and you click http://www.biblegateway.com/resources/audio and hear Audio Bible in any chapter you prefer.

    Please forward this e-mail I send to you to anyone you know and GOD will bless and remember you in his kingdom because you are spreading his messages.

    Remember you can use just half an hour to educate your self, Think how much time you are wasting for other issues so please spends your time with GOD today.

    God loves you all and that’s why is using me to send this message, just think what will you do when judgement day is today? Are you prepared enough? So try to talk with GOD to remember you, your generation and the whole world to his Kingdom. Think now and do actions because time is near.

    Every blessing,
    MK

    JibuFuta
  2. Swali zuri sana hili Bwaya: je tatizo ni dini au watu?

    Pengine tunaweza kuongeza swali jingine:
    je kuna dini bila watu?

    JibuFuta
  3. Sikubaliani na hitimisho la mtazamo wako kuhudu dini, kuwa dini zote zinatufunza mambo mema na hivyo zinafaa. Nitafafanua kwenye makala yake maalum.

    JibuFuta
  4. Dini ni mfumo wa maisha,hata hao wanaoabudu shetani nao huo ni mfumo wao, hakuna tatizo hapo unapofanya chochote katika muundo wa kimfumo tambua hiyo tayari ni dini, kabla ya waarabu na wazungu, wayunani nk wazee wetu waliamini mifumo yao nazo tunaamini ni dini, hakuna maisha bila mfumo na kila mfumo ni (dini)hakuna watu bila mifumo nayo hiyo mifumo ni dini kila kitu kina kwenda kwa mfumo wake ambao kwa maana nyingine ni dini yake hata blog ina mfumo wake ambao ni dini yake

    JibuFuta
  5. nashukuru mwalimu kwa hili somo lako.kaza buti kazi bado mbichi.

    JibuFuta
  6. kazi nzuri kaza buti mwalimu

    JibuFuta
  7. Hapo Nyembo umechanganya mambo. Tofautisha kati ya watu na mfumo. Mfumo lazima uundwe na watu lakini watu hawalazimiki kuundwa na mfumo.

    Kwa mfano watu huunda dini, lakini dini haiundi watu. Pia sikubaliani na usemi kuwa kila mfumo ni dini. Kumbuka kuna mfumo wa uchumi, mfumo wa siasa, mfumo wa chakula, uzazi, mfumo wa utawala nk nk. Ingawa dini ina visifa vyo mfumo ila kimsingi dini inamaanisha jumla ya imani ya watu kuhusu yale wanayoangalia kama takatifu, kiroho au kuhusiana na Mungu (kamusu-elezo-huru)

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?