Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Katika mchakato wa kuomba ajira baada ya kuona tangazo la kazi, mambo matatu ni dhahiri. Mosi, huombi kazi hiyo wewe mwenyewe. Wapo watu wengi wanaoandika maombi na hivyo kuongeza ushindani wa nani atapata.

Pili, nyaraka unazotuma kwa mwajiri mtarajiwa ndizo zinazojenga utambulisho wako kabla wewe mwenyewe hujafahamika. Tatu, afisa mwajiri hatatumia muda mrefu kusoma maelezo yako. Katika hali ya kawaida, atatumia dakika moja kuamua ikiwa amevutiwa na maelezo yako ama la.

Kwa sababu hizo, maandalizi ya nyaraka utakazotumia kuomba kazi ni muhimu yafanyike kwa umakini ili kuongeza uwezekano wa kuitwa kwenye usaili.

Katika mfululizo wa makala hizi, tutajadili namna unavyoweza kuandaa nyaraka mbili kuu ambazo ni wasifu (maelezo) binafsi, pamoja na barua ya maombi ya kazi. Katika makala ya leo, tunaanza na wasifu binafsi.

Wasifu binafsi ni maelezo yanayopambanua maarifa, ujuzi na uzoefu alionao mtafuta kazi kwa lengo la kumshawishi mwajiri kuwa anazo sifa na vigezo vya kuweza kufanya kazi iliyotangazwa.

Katika kuandika wasifu binafsi, mambo saba ni ya muhimu kuzingatia:


Taarifa za msingi za mtafuta kazi 


Weka taarifa zinazokutambulisha kama vile majina yako kamili, jinsia, hali ya ndoa, tarehe ya kuzaliwa, utaifa na njia muhimu za mawasiliano zinazoweza kutumiwa kukufikia.

Mfano:
        Jina:
        Utaifa:
        Mahali pa kuzaliwa: 
        Tarehe ya kuzaliwa: 
        Hali ya Ndoa: 
        Anwani ya Posta: 
        Simu:
        Barua pepe: 

Hata hivyo, zipo taarifa nyinginezo zinazoweza kuwa muhimu lakini zisizo na ulazima wa kufahamika. Hizi ni kama kabila, dini, idadi ya watoto na mitazamo au ufuasi wa kisiasa.

Unaweza kuwa na aya moja yenye mhutasari wa wasifu wako, ukaeleza tunu zinazoongoza utendaji wako wa kazi. Aya hii inapoandaliwa vizuri hujenga taswira ya mtu anayejitambua.


Sifa za kitaaluma


Kuna namna nyingi za uandikaji wa sifa hizi, lakini kilicho muhimu ni kueleweka. Anza na ngazi ya juu zaidi ya kitaaluma uliyofikia na shuka mpaka ngazi ya chini. Onesha mwaka yalipofanyika mafunzo hayo, tunuku ya kitaaluma (mfano cheti, Stashahada, shahada) na chini yake taja taasisi iliyotoa tunuku hiyo na mahali ilipo (mfano shule, chuo na kadhalika).

Mfano;             
                          2011-2013: Shahada ya Sanaa katika Stadi za Mazingira
                                             Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge, Moshi  

Kwa kawaida, sifa hizi huwa ni zile zinazohusiana na mafunzo ya ujuzi yatolewayo kwa ngazi ya chuo kukupa utaalam. Lakini waweza pia kutaja ngazi ya Cheti cha Juu cha Elimu ya Sekondari na Cheti cha Elimu ya Sekondari.


Uzoefu na historia ya kuajiriwa

Onesha ajira ulizowahi kuzifanya iwe kwa ajira rasmi au kwa kujitolea. Orodhesha uzoefu wako kwa mtiririko wa aina ya ajira kuanzia ya hivi karibuni zaidi au uliyonayo, taasisi husika pamoja na mwaka wa kuanza na kumaliza kazi hiyo.


Kumbuka kuwa mwajiri makini hutafuta kuona maneno muhimu kama "kuzalisha/kuongeza (ufanisi)", "kupunguza/kuondoa (changamoto)", "kubuni", "kuanzisha", "kusababisha", "kubadili", "kuchangia mabadiliko", "kuwezesha" na mengineyo.
Kwa mfano,
2013-2015: Mwandishi wa Habari za Mazingira, Mwananchi Communications Ltd
            Kwa kushirikiana na wenzangu, nilibuni utaratibu wa…ambao ulisaidia kuondoa changamoto ya…iliyokuwepo awali.

Usipoteze muda kueleza majukumu yako ya kila siku. Tafuta maeneo ambayo mchango wako ulionekana na yataje kwa kutumie vitenzi tulivyovitaja hapo juu.

Ujuzi na weledi

Katika sehemu hii onesha aina ya ujuzi na weledi uliowahi kuupata kupitia warsha, semina na makongamano yalivyokusaidia kuongeza ujuzi mwepesi unaoweza kukusaidia "kuzalisha", "kukuza", "kubuni", "kuanzisha", "kusababisha", "kubadili", "kuchangia mabadiliko" na "kuwezesha". Onesha mahali, mwaka, shughuli husika na malengo yake kwa mtiririko wa kuanzia hivi karibuni mpaka yale ya zamani.


Machapisho na tafiti

Kama kazi unayoomba inahusiana na masuala ya taaluma na elimu (mfano ualimu, ukufunzi, utafiti, uhadhiri), onesha machapisho na tafiti ulizowahi kuzifanya na kuziandika. Hapa, utaonesha jina la chapisho husika, mchapishaji na mwaka lilipochapishwa. Lengo ni kuonyesha ushiriki wako katika kutafuta majibu ya changamoto zinazoikabili jamii, ikiwa ni pamoja na kuchangia kukuza maarifa yaliyopo.


Tuzo au heshima 

Mwajiri huvutiwa na mtu anayeweza kuonesha namna jitihada zake zilivyotambuliwa na wengine. Onesha namna bidii, na ari yako ya kazi ilivyowahi kutambuliwa katika ajira zilizopita. Si lazima iwe kazini tu, yaweza kuwa katika masomo, lakini ziwe tofauti na zile tunuku za kitaaluma moja kwa moja.

Maneno kama, "nilishinda", "nilituzwa" na "nilitambuliwa", kwa sababu ya shughuli, majukumu, jitihada zilizowahi kufanywa, yanakuongezea nafasi ya kukubalika.


Orodha ya wadhamini

Taja watu wanaoaminika wanaoweza kutoa ushuhuda wa uwezo na weledi wako. Orodhesha angalau watu watatu wenye nyadhifa zinazotambulika na wanaokufahamu vizuri iwe kwa sababu wamekufundisha au waliwahi kufanya kazi na wewe.

Ni vizuri kuwasiliana nao kabla ya kuwataja kwa kuwa wanaweza kuulizwa pasipo wewe kujua. Na wakati mwingine ni vyema kuwaomba kukuandikia barua ya utambulisho ukazitumia inapolazimika.


Zingatia
·         CV nzuri hubadilika kukidhi matakwa ya kazi inayoombwa.
·         Imeandikwa kwa ufupi na haizidi kurasa mbili
·         Ina taarifa nyingi muhimu lakini kwa maelezo yanayoonekana kirahisi
·         Imeandikwa kwa umakini na haina makosa ya kiuchapaji
·         Haina taarifa zilizotiwa chumvi au uongo
·         Haina picha ya mwombaji


Maoni

  1. KAKA, nakupa hongera sana kwa darasa zuri unaloliendesha. MUNGU akubariki sana

    JibuFuta
  2. Hongera sana na asante kwa mafunzo

    JibuFuta
  3. iko poa sana so helpful

    JibuFuta
  4. Imekidhi mahitaji, so ipo ok

    JibuFuta
  5. Tafadhali unaweza kuattach video yangu nikielekeza namna ya kuandika cv kwa kutumia simu ya mkononi

    Link yake hii hapa
    https://youtu.be/l3JEl78gMso

    Natanguliza shukran

    JibuFuta
  6. Ameiandika kazi yake vizuri na ipo wazi,asante sana

    JibuFuta
  7. Ime kaa poa sana kaka sija wahi kuandika cv ila umeni fundisha xx naweza kuandika

    JibuFuta
  8. Asant mkuu kwa darasa lako nimeelewa shukran

    JibuFuta
  9. Asante mkuu kwa darasa nimeelewa shukran

    JibuFuta
  10. Nzuri Sana kaka

    JibuFuta
  11. เฮง เฮง 888 สล็อต เว็บตรง มาแรง การเล่นสล็อตออนไลน์กำลังเป็นที่นิยมอย่างต่อเนื่องในวงการเกมโอนไลน์ pg โดยเฉพาะเมื่อมีเว็บไซต์ที่เปิดให้บริการโดยตรงที่มีชื่อเสียงและมีความน่าเชื่อถือ

    JibuFuta
  12. Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159
    dawnacuna314@gmail.com

    JibuFuta
  13. Uchawi wa mapenzi wa Dkt. Dawn hufanya maajabu kweli.

    Niliwasiliana na Dkt. Dawn wakati uhusiano wangu ulipovunjika kabisa. Mpenzi wangu wa zamani alikuwa ameniacha na kunizuia kwenye mitandao yote ya kijamii. Nilivunjika moyo na kupoteza tumaini. Baada ya kushauriana na Dkt. Dawn, kila kitu kilibadilika. Mpenzi wangu wa zamani alirudi peke yake, akaomba msamaha kwa dhati, na akaomba msamaha. Leo, tunaishi pamoja kwa furaha, na hata tuna mtoto.

    Maneno hayatoshi kuelezea jinsi ninavyoshukuru. Kutokana na uzoefu wangu, naweza kusema kwa ujasiri kwamba Dkt. Dawn ni halisi, anayetegemewa, na mwenye nguvu. Ikiwa unakabiliwa na hali yoyote ngumu maishani mwako hivi sasa, Dkt. Dawn anaweza kukusaidia.

    ANAWEZA KUKUSAIDIA KWA MATATIZO YAFUATAYO:
    Kurudisha ndoa na mahusiano yaliyovunjika
    Kuvutia mafanikio na ukuaji katika biashara
    Matatizo ya uanaume, utasa, na ukosefu wa watoto
    Kurejesha mali zilizoibiwa au zilizopotea
    Kurudisha kazi zilizopotea au fursa za kazi
    Kinga dhidi ya uchawi na macho mabaya
    Hirizi za mvuto
    Kutatua migogoro ya ardhi na mali
    Kuwafanya wapenzi kutimiza ahadi zao
    Kushinda kesi mahakamani, na mengine mengi
    Huu si ulaghai — ni ushuhuda kutoka kwa uzoefu.
    Kwa maelezo zaidi, wasiliana naye moja kwa moja kwenye WhatsApp. +2349046229159
    dawnacuna314@gmail.com

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Uislamu ulianza lini?

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Kama sio utumwa ni nini hiki?