Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Katika makala haya, tunatazama kwa ufupi makuzi ya mtoto mwenye umri wa siku moja mpaka miezi 36. Tutaangalia mambo ya msingi yanayonesha ukuaji wa mtoto unavyoendelea katika maeneo makubwa manne; 1) ukuaji wa kimwili 2)  kiakili 3)  kimahusino na watu wengine na mwisho 4) kihisia. Kwa kawaida maeneo haya manne yanategemeana ili kumwezesha mtoto kukua kwa ujumla. Kwa mfano ili mtoto akue kimwili, anahitaji ukuaji wa akili ipasavyo ambayo nayo itaathiri namna anavyomudu hisia zake na hivyo kuhusiana na watu wengine. Kwa hiyo ni sawa tukisema hakuna ukuaji wa eneo moja usiotegemea eneo jingine.

Ukuaji wa kimwili

Kwa kawaida ukuaji wa mwili kwa mwaka wa kwanza huenda kwa kasi kubwa. Kwa mfano, wakati mtoto huzaliwa akiwa na wastani wa uzito wa kilo 3.4 hivi, ndani ya miezi sita uzito huo huongezeka mara dufu na kufikia mara tatu anapotimiza miezi 12. Hii ni kasi kubwa inayotegemea sana ubora wa lishe, mazingira rafiki ya ukuaji, afya ya mwili na hata nasaba za ukuaji alizorithi mtoto kutoka kwa wazazi wake wawili. Ili kuwezesha ukuaji huu kufanyika, mtoto hulala usingizi mfupi mfupi kwa masaa kati ya 16 na 18 kwa siku.  Kulala hutokea mchana kuliko usiku lakini kadri anavyokuwa usingizi huanza kutokea wakati wa usiku kama ilivyo kawaida ya wengi.

Kwa muda wote wa miaka mitatu ya mwanzo, kwa ujumla, mtoto huwa bado akijifunza kuvimudu viungo vya mwili wake na kuvitumia kwa usahihi ili aweze kukabiliana na changamoto za kimazingira. Kinywa ndiyo sehemu inayomsisimua mtoto kipindi hiki. Kila anachoshika, safari yake huishia kinywani. Usafi na uangalizi wa karibu unahitajika vinginevyo anaweza kujikuta akipata magonjwa yatokanayo na uchafu.

Ni katika kipindi hiki ndipo mtoto huweza kuimudu shingo yake vizuri, mikono na kiwiliwili na hivyo anapotimiza miezi sita huwa tayari ana uwezo wa kuhama mwelekeo akiwa usingizini. Asipoangaliwa vizuri mzazi anapostuka usingizini usiku wa manane anaweza kumwokota mtoto akiwa uvunguni.

Baada ya kumaliza miezi sita, mtoto huanza kuota meno kwa mkupuo wa meno mawili mawili yakianzia kwenye ufizi wa chini na kisha ufizi wa juu. Ni wakati huo huo ambapo mtoto huanza kukaa mwenyewe hatua kwa hatua kisha ndani ya miezi 12 ya mwanzo huanza kutambaa, kusimama na hatimaye kuchukua hatua ya kwanza kabla au baada tu ya mwaka wa kwanza.

Mtoto akijaribu kusimama mwenyewe. Picha: Jielewe
Tuanaambiwa na wataalam kwamba mtoto anayesisimushwa mapema na kuwekewa mazingira yanayohamasisha kufanikiwa kwa hatua fulani ya ukuaji (milestone), huwa mbele ya wenzake wanaoachwa wapate hatua hizo wenyewe. Mfano wa visisimushi hivyo ni michezo inayomchangamsha mwili na kumhamasisha kusimama, kutembea na kadhalika.

Baada ya miezi 12 ya awali, mtoto huwa na uwezo wa kuvimudu viungo vyake vizuri zaidi kumwezesha kutembea, kujilisha, kujivalisha na hata kujisaidia wakati ule tu anapokuamua mwenyewe kama akifundishwa. Uwezo wa kuhama mwenyewe kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, humfanya mtoto ajione mwenye kujitegemea zaidi na mwenye uhuru zaidi. Hata hivyo, hiki ndicho kipindi ambacho mtoto hupata ajali nyingi na kuvunja vifaa/vyombo vya nyumbani kwa sababu misuli inayomwezesha kushika vitu kwa umakini bado inakuwa haijapevuka vizuri. Anaweza kusaidiwa kwa kupewa vifaa imara na visivyoleta hatari vikivunjika kama vikombe vya plastiki, bati na kadhalika.


Anapoelekea mwaka wa pili na wa tatu kasi ya ukuaji hupungua kidogo shauri ya shughuli nyingi na hivyo ongezeko la uzito huwa dogo kuliko ilivyokuwa katika mwaka wa kwanza. Sababu kubwa ni ongezeko la harakati za michezo mingi inayotumia nguvu nyingi shauri ya kuimarika zaidi kwa misuli ya mwili. Nafasi ya kutosha katika nyumba na uangalizi wa karibu ambao hata hivyo unalinda uhuru wa mtoto ni mambo muhimu katika umri huu.

Kwa ujumla tunaweza kusema katika kipindi cha miaka mitatu ya mwanzo, ukuaji wa mwili unaoenda kwa kasi huenda sambamba na kupevuka kwa viungo vya mwili ili kumwezesha mtoto kujifunza na kuyasaili mazingira yake. Ukuaji huu kwa kiasi kikubwa hutegemea kupevuka kwa ubongo ambao kwa kawaida huratibu hatua zote za makuzi ya mwili.

Hata hivyo, ukuaji wa mwili ni eneo ambalo kwa kiasi kikubwa liko juu ya uwezo wa mzazi. Zaidi ya kuhakikisha kwamba mtoto anapata chakula bora kitakachosaidia kujenga mwili, wajibu mkuu wa mzazi ni kuweka mazingira yanayompa nafasi mtoto kuyasaili mazingira yake kwa uhuru na kujiamini na kuondoa hatari ya madhara mtoto anapojifunza. Kadhalika, mzazi ana wajibu wa kutathmini kile anachoweza kufanya mtoto kulingana na umri wake ili kuweza kupata msaada wa wataalam kwa wakati ikiwa mtoto ataonekana kuwa nyuma katika ukuaji wake.

Ukuaji wa kiakili

Kiakili, mtoto huzaliwa na ubongo unaochemka vizuri ili kumwezesha kuyaelewa mazingira yake na hivyo kujenga kumbukumbu za mambo anayokutana nayo bila kutegemea mafundisho/maelekezo yoyote.  Kwa kutumia taarifa zinazotoka kwenye viungo vya mwili wake na milango ya fahamu, mtoto anaweza kurekodi yanayoendelea kwenye mazingira yake ili kumsaidia kujifunza.

Kwa ujumla, katika miezi sita ya mwanzo, mtoto huwa na shughuli kubwa ya kujenga uzoefu unaofanana na vipande vya filamu kadri anavyoingiliana na wanaomzunguka kwenye mazingira yake. Ongezeko la vipande hivi vya filamu katika ufahamu wake ndivyo vinavyomsaidia kujenga uhusiano baina ya matukio na kadri unavyoongezeka, humsaidia kufikiri kwa ufasaha. Hii ina maana kwamba anachofikiri mtoto huanzia kwenye kile kinachofanyika kwenye mazingira yake ikiwa ni pamoja na mwili wake mwenyewe. Hana uwezo wa kufikiri kisichoonekana kwa macho.

Kadhalika, milango yake ya fahamu inayoendelea kupevuka hutenda kazi sawa sawa kumsaidia mtoto kujenga tajiriba ya ufahamu pamoja na kwamba uwezo huo unaongezeka hatua kwa hatua. Kwa mfano, ndani ya miezi sita mtoto huwa na uwezo wa kurudia matendo ya mwili wake yanayoleta matokeo yenye kumvutia. Kurudia kinachovutia ni hatua ya kwanza katika hujenga uwezo wa kumbukumbu na utatuzi wa changamoto zinazojitokeza katika mazingira yake. Hiyo ndio kusema, wajibu wa mzazi ni kumwekea mazingira sisimushi yanayomfanya ajenge uwezo wa kutatua vikwazo katika mazingira yake kwa wepesi na uhuru.

Ndani ya mwaka mmoja mtoto huweza kukumbuka uwepo wa vitu asivyoviona kwa macho kuthibitisha kwamba kumbukumbu yake inaimarika. Katika kipindi hiki, hujenga uwezo wa kutafuta vilivyofichwa pamoja na kutambua sauti za watu anaowafahamu wanaomzunguka. Hii ni hatua kubwa sana ya kiakili inayoweza kuimarishwa kwa kumwekea mazingira sisimushi.  

Tukio jingine muhimu la ukuaji wa kiakili ni matumizi ya lugha katika kuwasiliana na wanaomzunguka kati ya miezi 12 na 18.  Mtoto huanza kutumia maneno katika kuwasiliana na wengine. Ingawa ni kweli kwamba idadi ya maneno yanayotamkwa huzidi ufahamu alionao mtoto, ongezeko la msamiati ni dalili ya kukua kwa uelewa wa mtoto. Mpaka anafikisha miezi 24, mtoto huwa na msamiati wa maneno zaidi ya 200 yanayowakilisha dhana, vitu, watu na hali kadha wa kadha katika ufahamu wake. Maana yake ni kwamba sasa mtoto huweza kufikiri kwa kutumia lugha bila kuhitaji kukiona kitu kwa macho.

Ongezeko la uwezo wa kujenga picha ya kinachozungumzwa bila msaada wa kuwepo kwa kitu halisi humsaidia kusikiliza hadithi fupi fupi na kuzielewa. Hiki ndicho kipindi ambacho mzazi anaweza kumsomea hadithi fupi kumfundisha dhana mbalimbali katika maisha kama kuelewa hisia za wengine, matokeo ya tabia zisizokubalika, nidhamu, mambo ya kiroho na kadhalika.

Kwa sababu ya kuimarika kwa uwezo wa kufikiri na kuhoji, mpaka anapofikisha miaka mitatu, mtoto huwa na uwezo wa kuuliza maswali mengi yanayolenga kumsaidia kuelewa mambo yanayomtatiza katika mazingira yake. Pamoja na kumwongezea msamiati wake na uelewa, maswali mengi ni mbinu ya kukuza mahusiano na wanaomzunguka. Ndio kusema, mzazi ana wajibu wa kuyajibu maswali ya mtoto kwa usahihi kulingana na umri wa mtoto.

Bonyeza hapa kwa ukuaji wa kimahusiano na hisia.
christianbwaya [at] gmail [dot] com

Maoni

  1. Good article, thanks for sharing

    JibuFuta
  2. Chapisho hili limeondolewa na msimamizi wa blogu.

    JibuFuta
  3. PROAKUN.WIN | AGEN BANDARQ | QQ ONLINE | DOMINOQQ | BANDARQ ONLINE | JUDI ONLINE TERBAIK DI INDONESIA, adalah Website Rekomendasi Situs Situs Terbaik dan Ternama dengan Hasil Winrate Teringgi Terbaik Di Indonesia.

    Agen BandarQ
    QQ Online
    DominoQQ
    BandarQ Online
    Judi Online

    JibuFuta
  4. อยู่บ้านก็หาเงินใช้ได้ สล็อตออนไลน์ เล่นสล็อต slotxo ฟรีเครดิต ไม่มีโกง เล่นเลยที่นี่

    https://www.slot2xl.com/

    JibuFuta

  5. เล่นเกมแล้วได้เงิน สล็อตออนไลน์ slotxo เล่นง่ายๆ เล่นสล็อต ฟรีเครดิต slotxo
    ได้เงินจริง เล่นเลยที่นี่ คลิกเลย เกมยิงปลา อย่าพลาดมาลุ้นกันเลย slotxo
    https://www.slot4u.com

    JibuFuta
  6. Hi! This is my first comment hereJOKER SLOT

    JibuFuta
  7. เว็บพนันออนไลน์ ที่มีมาตรฐาน ความปลอดภัยสูง ระดับสากล เล่นแล้วได้รับเงินจริงๆ Joker Slot ของเรา รองรับการเล่น บนมือถือสมาร์ทโฟน ทั้งระบบแอนดรอยด์ (android) และ ไอโอเอส (ios) เป็นสล๊อตออนไลน์มือถือ ที่สะดวก สบาย และ ไว้ใจได้ เพราะเราทำงานโดยทีมงานมืออาชีพ การบริการชั้นดี และ การดูแลระบบโดยผู้เชี่ยวชาญ ที่มีประสบการณ์ เข้าใจนักเสี่ยงโชค

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?