Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2016

Mbinu za Kutafuta Ajira Mtandaoni

Picha
Changamoto kubwa inayoweza kukukabili unapotafuta kazi, ni taarifa zitakazokusaidia kujua uelekeze wapi maombi ya kazi. Zamani, ili kupata taarifa za kazi, watu walitegemea radio, magazeti, televisheni na taarifa za marafiki wanaofahamiana nao. Mambo yanazidi kubadilika kwa kasi. Sasa hivi, kwa mfano, matumizi ya mtandao yamerahisisha namna tunavyoweza kupata taarifa hizi. Hata hivyo, pamoja na uwepo wa mtandao, bado kuna changamoto ya wapi hasa waweza kupata taarifa sahihi. Mbinu zifuatazo ni matokeo ya uchambuzi wa tafiti mbalimbali na zinaweza kukupunguzia changamoto ya kupoteza muda na nguvu nyingi kutafuta kazi mtandaoni.

Mambo Matano Yanayoweza Kukusaidia Kupata Muda wa Kuwa Karibu na Mtoto

Picha
Wazazi wengi wanapenda kuwa karibu na watoto  kwa lengo la kuwajengea mazingira ya kujifunza. Changamoto, hata hivyo, ni kukosa muda wa kutosha kufanya hivyo. Kwa mfano, ni kawaida kwa wazazi kutoka nyumbani alfajiri na kurudi usiku wakati ambao tayari watoto wameshalala. Matarajio makubwa ya kikazi yamekuwa kipaumbele na hivyo tunatumia muda mwingi kufanya kazi ambazo kimsingi ndizo zinazotusaidia kuwatunza watoto wetu.  Hata hivyo, majukumu  yetu haya muhimu yanatufanya wakati mwingine tukose muda wa kuwasaidia watoto kihisia, kiufahamu na hata kimahusiano kama tunavyotamani. Makala haya yanajadili hatua tano za kuchukua ili kukusaidia mzazi kupata muda wa kuwekeza katika malezi ya watoto wako.

Unatafuta Kazi? Sifa Sita Unazozihitaji

Picha
Katika makala yaliyopita tuliona takwimu zinazothibitisha kuwa tatizo la ajira ni zaidi ya kukosekana kwa nafasi za kazi. Ingawa watafuta kazi wengi hufanya juhudi za kuthibitisha kuwa wanao ujuzi rasmi waliousomea darasani, si waajiri wengi wanathamini alama za darasani zinazoonekana kwenye vyeti vya waombaji hao. Badala yake, mwajiri kwa kawaida hutafuta ujuzi ambao mara nyingi mtafuta kazi hautegemei. Ujuzi huo, tulioupachika jina la ‘ujuzi mwepesi’, ni pamoja na ule uwezo wa kutumia maarifa ya jumla ya darasani katika kufumbua matatizo halisi yanayomkabili mwajiri katika eneo lake la kazi.

Mambo Sita ya Kufanya Unapotafuta Kazi

Picha
Kutafuta kazi ni kuingia kwenye soko la ajira ambalo kimsingi ni uwanja unaowakutanisha watu wenye mahitaji makubwa ya aina mbili. Upande mmoja, wapo watu wenye ‘bidhaa’ ya ujuzi na weledi, lakini wenye hitaji la kujipatia kipato kwa kutumia ujuzi na maarifa waliyonayo. Hawa wanaitwa watafuta kazi.

Jinsi ya Kumfundisha Mtoto Kuwa Mwuungwana

Picha
Umewahi kumpa mtu kitu anachokihitaji lakini haoni sababu ya kusema, ‘asante’? Mtu anakukosea na hawezi kusema, ‘samahani’, ‘nisamehe’? Wapo wengine hata ufanye vizuri namna gani kusema, ‘hongera umefanya vizuri’ ni kama adhabu na kujishushia hadhi. Hizi ni baadhi ya tabia zinazoweza kuonesha namna mtu asivyo muungwana na zinaweza kumpunguzia thamani yake mbele ya jamii.

Unaweza Kumfundisha Mtoto Adabu Bila Kumchapa

Picha
Mjadala wa fimbo na malezi una historia ya mjadala mkali. Fimbo, kwa hakika, zimekuwa kama sehemu ya maisha yetu . Takwimu zinathibitisha hali hii. Kwa mfano, asilimia zaidi ya 80 ya wazazi wa nchi zinazoendelea wanatumia fimbo angalau mara moja kwa mwezi. Ndio kusema, vipigo kwa watoto vimekuwa sehemu ya malezi katika nchi zetu hizi. Matumizi haya makubwa ya fimbo kwa kiasi fulani yanatokana na imani waliyonayo wazazi kuwa bila mtoto kusikia maumivu hawezi kurekebisha tabia wala kuwa msikivu. Ingawa hakuna ushahidi wowote kuwa viboko vinasaidia kujenga nidhamu kwa watoto, bado wazazi wengi wanaamini adhabu ya fimbo ndiyo jibu la kumnyoosha mtoto.

Namna Michezo Inavyomsaidia Mtoto Kujifunza

Picha
Wazazi wengi wanaichukulia michezo ya watoto kama shughuli isiyo na maana. Kimsingi, ipo imani inajengeka kuwa kucheza ni kupoteza muda. Matokeo yake wazazi hujitahidi kuwazuia watoto wasicheze kwa matumaini ya kuwasaidia wapate muda wa kufanya mambo ya maana zaidi kama vile kusoma na kukamilisha kazi za shule. Pamoja na umuhimu wa kufanya hivyo, hata hivyo, michezo  inabaki kuwa shughuli yenye umuhimu mkubwa katika ukuaji wa jumla wa mtoto kimaarifa, kimahusiano, kimwili na kihisia.

Wajibu wa Mzazi Kama Mwalimu wa Kwanza wa Mtoto

Picha
Tafiti nyingi za mazingira ya kujifunzia zimeendelea kusisitiza kuwa elimu bora kwa mtoto huanzia nyumbani. Kuwepo kwa mazingira rafiki ya kielimu nyumbani kunampa mtoto nafasi ya  kukua kiufahamu na humuandaa vyema kujifunza kabla hajaanza shule rasmi. Kimsingi, mzazi ndiye mwalimu wa kwanza anayemwezesha mtoto kujifunza vizuri. Mtoto hujifunza kutembea, kuongea, kujilisha, kazi za nyumbani na kadhalika kwa msaada wa mzazi. Ikiwa mzazi atatambua wajibu wake kama mwalimu wa mtoto na akautekeleza ipasavyo, kazi ya mwalimu shuleni hurahisishwa.

Mambo ya Manne ya Kufanya Mtoto Akusikilize, Akuheshimu

Picha
Msomaji mmoja wa safu hii aliniandikia hivi majuzi akidai mwanae hamsikilizi. Kwa mujibu wa mzazi huyu, pamoja na kufanya jitihada za kumwelekeza mwanae mambo muhimu ya kimaisha, bado kijana wake huyo haonekani kusikiliza. Anasema, kadri anavyomwadhibu mwanae, ‘ndivyo anavyozidi kuwa mkaidi…’ Mzazi huyu, inavyoonekana, amepoteza mamlaka yake kama mzazi. Mamlaka kimsingi ni uwezo wa kusema kitu na kikasikika bila kulazimika kutoa adhabu. Unapokuwa na mamlaka maana yake unayo nguvu ya ushawishi inayomfanya mtoto awe tayari kukuiga, kukusikiliza, kukuelewa na kufanya kwa hiari yake yale unayomwelekeza.

Mwaka Mmoja Bila Mama, Mkono wa Mungu Haujatuacha…

Picha
Nakumbuka mwezi Juni 2002, nikiwa mwanafunzi wa sekondari, eneo ni stesheni ya gari moshi (treni) mjini Singida nikiwa ninarudi nyumbani nikitokea Dodoma. Ilikuwa ni safari ya kuunga unga iliyoanzia Dar es Salaam kupitia Dodoma na kisha Singida. Wakati huo tulikuwa tunaondoka Dodoma saa nne asubuhi, Singida tunafika saa za jioni kuanzia saa kumi na moja hivi tukiwa taabani kwa uchovu wa kukaa kwenye mabehewa yaliyoonekana kuhangaika mno kupita kwenye mataruma katikati ya vichaka ya Dodoma na Singida. Jioni hiyo ninayoikumbuka vyema tulichelewa kidogo na hatimaye tulifika Singida stesheni saa kumi na mbili unusu hivi za jioni.

Kanuni za Kuongeza Ushawishi wa Hoja Zako

Picha
Kwa nyakati tofauti kila mmoja wetu hutamani kuwa na ushawishi kwa wengine. Ni kawaida, kwa mfano, kutamani hoja tunazozitoa zipokelewe na wale tunaowatumia ujumbe husika. Ili ujumbe upokelewe, inahitajika nguvu inayoweza kuwasukuma wengine kuupenda, kuubali na ikiwezekana kubadilika kwa sababu ya ujumbe husika. Nguvu hii inaitwa ushawishi.