Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2018

Mbinu za Kumfundisha Mtoto Kusoma Akiwa Nyumbani

Picha
Katika utafiti uliofanywa na program ya Uwezo iliyochini ya Shirika la Twaweza, zaidi ya nusu ya watoto wa darasa la nne na tano katika nchi za Afrika Mashariki hawana uwezo wa kusoma na kuandika. Nilimwuuliza Bahiya Abdi, mhadhiri wa masuala ya mitalaa, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge, maana ya kutokujua kusoma na kuandika. Anasema: “Kuna mambo kadhaa ya kuangalia tunapozungumzia uwezo wa mtoto kusoma. Mbali na mtoto kutambua herufi, lazima awe na uwezo wa kusoma kwa haraka.” “Lakini pia, uwezo wa kusoma unapimwa kwa kiwango cha kuelewa kile anakisoma. Kama mtoto anaweza kusoma tu lakini hawezi kupata ujumbe vizuri, hapo tunaweza kusema uwezo wake uko chini ya kiwango.” Kwa mujibu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) mtoto wa darasa la kwanza na la pili anatarajiwa kutambua na kusoma kwa ufasaha maneno 50 yenye maana kwa dakika na maneno 40 yasiyo na maana kwa dakika. Kadhalika, anatarajiwa kuandika kwa ufasaha herufi kubwa na ndogo, na kufanya hesabu za kujumlisha na k

Unaweza Kumruhusu Mtoto Afuate Dini Apendayo?

Picha
PICHA: Pixabay Ipo nafasi muhimu ya imani/dini katika malezi ya watoto. Imani si tu inamsaidia mtoto kujitambua, lakini pia ina nafasi ya kumtengenezea mtoto sauti kutoka ndani yake inayomsaidia kupambanua lililo jema na baya. Sauti hii inaitwa dhamira. Utakuwa shahidi kuwa kuna mambo wakati mwingine unatamani kuyafanya lakini unajisikia hatia kuyafanya. Unaweza, kwa mfano, kuwa na uhuru wa kutaka kufanya chochote, lakini kuna sauti ndani yako ikakunyima ujasiri wa kukifanya. Hakuna anayekuona, hakuna anayekuhukumu, lakini kuna kengele ndani yako inakwambia kuwa unachotaka kukifanya sio sahihi. Mwanasaikolojia wa kale anayeitwa Sigmund Freud aliita kengele hiyo ‘Superego’ kumaanisha mkusanyiko wa maelekezo tunayoyapata kwa watu wanaotuzunguka. Kwa kawaida, sauti na maelekezo hayo inayoumbika ndani yetu ndiyo inayoamua namna gani tunadhibiti matamanio yetu ya asili kama hasira na tamaa za mwili. Imani, tafiti zinasema, ina kazi kubwa ya kujenga dhamira. Mtu mwenye

Kwa Nini Unatamani Kubadili Tabia Lakini Huwezi?

Picha
PICHA:  Coherentnews.com HEMEDI anavuta zaidi ya ‘pakiti’ moja ya sigara kwa siku. Ingawa, mara kadhaa, amejaribu kuacha tabia hii asiyoipenda, bado hajafanikiwa. Nia ya kuacha sigara anayo lakini kuacha ameshindwa. Unaweza kufikiri Hemedi yuko tofauti na sisi wengine. Lakini ukweli ni kwamba nasi, kwa namna tofauti, tunakabiliwa na mitihani mikubwa ya kitabia, pengine kuliko huo alionao Hemedi.   Kuna mambo fulani kwenye maisha yetu tunatamani kuyaacha lakini hatuwezi. Inawezekana ni matumizi mabaya ya fedha; kuongea kupita kiasi; hasira ya kulipuka; kusengenya na tabia nyingine tusizosipenda. Kwa upande mwingine, tunaweza kutamani kujenga tabia mpya lakini tunashindwa. Nawafahamu watu wengi ambao kila mwaka mpya unapoanza wanajipanga kufikia malengo makubwa. Wanautazama mwaka mpya kwa mtazamo tofauti na wanatamani kuwa watu tofauti na walivyokuwa kwa mwaka uliomalizika. Wengine wanajiapiza kuanza kusoma vitabu; wengine kufanya mazoezi ya mwili; wengine kuanza ku

Je, Kazi yako Inakuza au Inadumaza Wito Wako?

Picha
Inawezekana unafanya kazi ambayo hukuwahi kufikiri kama siku moja ungeifanya. Labda unadhani hukuchagua vizuri kipi cha kufanya, au pengine mazingira yalikulazimisha kushika kilichokuwa kinapatikana. Kwa upande mwingine, inawezekana pamoja na kuipenda kazi yako, unahisi kuna namna fulani ya udumavu. Hupati fursa za kupanda ngazi kiutendaji na umeanza kujihisi unapoteza wito wako. Vyovyote iwavyo, bado kuna tumaini. Unaweza kabisa kufanya kazi unayojua fika haiendani na wewe, lakini hatua kwa hatua, ikakutengenezea jukwaa zuri la kuumba vizuri wito wako. Hapa ninakuletea uzoefu utakaokusaidia kujitathmini na pengine kuchukua hatua muhimu katika kuchochea ule uwezo wa pekee ambao Mungu ameuhifadhi ndani yako. Unafanya kazi yenye staha? Mratibu wa Ukuuzaji wa Ujuzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Dar es Salaam, Bw. Albert William Okal anaeleza namna gani mazingira yako ya kazi yanavyoweza kukuza wito wako: “Hakuna kitu kama uchaguzi mbaya wa kazi. Kila kaz