Mbinu za Kumfundisha Mtoto Kusoma Akiwa Nyumbani




Katika utafiti uliofanywa na program ya Uwezo iliyochini ya Shirika la Twaweza, zaidi ya nusu ya watoto wa darasa la nne na tano katika nchi za Afrika Mashariki hawana uwezo wa kusoma na kuandika.
Nilimwuuliza Bahiya Abdi, mhadhiri wa masuala ya mitalaa, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge, maana ya kutokujua kusoma na kuandika. Anasema: “Kuna mambo kadhaa ya kuangalia tunapozungumzia uwezo wa mtoto kusoma. Mbali na mtoto kutambua herufi, lazima awe na uwezo wa kusoma kwa haraka.”
“Lakini pia, uwezo wa kusoma unapimwa kwa kiwango cha kuelewa kile anakisoma. Kama mtoto anaweza kusoma tu lakini hawezi kupata ujumbe vizuri, hapo tunaweza kusema uwezo wake uko chini ya kiwango.”
Kwa mujibu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) mtoto wa darasa la kwanza na la pili anatarajiwa kutambua na kusoma kwa ufasaha maneno 50 yenye maana kwa dakika na maneno 40 yasiyo na maana kwa dakika.
Kadhalika, anatarajiwa kuandika kwa ufasaha herufi kubwa na ndogo, na kufanya hesabu za kujumlisha na kutoa sambamba na kutambua herufi zinazokosekana.
Suala la watoto wetu kushindwa kusoma na kuandika kwa kiwango kinachotakiwa limekuwa mjadala mrefu katika majukwaa mbalimbali ya elimu. Zinatajwa sababu nyingi.
Moja, ni mazingira yasiyo rafiki katika shule zetu yanayowanyima watoto fursa ya kujifunza kwa ufasaha. Mazingira ni pamoja na vifaa vya kujifunzia pamoja na walimu wenye sifa na ari ya kufundisha.
Lakini pili, ni mrundikano wa masomo mengi katika madarasa ya awali. Mtoto mdogo –ambaye kimsingi bado anakua kiufahamu –anapolazimika kusoma mambo mengi kwa wakati mmoja inakuwa vigumu kuelekeza nguvu zake kwenye kukuza uwezo wa kusoma na kuandika.
Mbali na sababu hizo, ipo nyingine ya wazazi kutokuweka mazingira  yanayomwezesha mtoto kujifunza akiwa bado nyumbani. Bahiya Abdi anasema, “Mazingira ya nyumbani yana nafasi kubwa ya kumwezesha mtoto kusoma, kuandika na hata kuhesabu. Mzazi akitambua nafasi yake, kazi ya mwalimu atakayekutana na mtoto shuleni itakuwa rahisi sana.”
Katika makala haya tunajadili maeneo matano yanayoweza kukuza uwezo wa mtoto kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu katika mazingira ya nyumbani.
Picha za irabu
Jema Karume, mkufunzi wa Chuo cha Ualimu Singachini nje kidogo ya mji wa Moshi, anashauri  wazazi kuwapa watoto vifaa vinavyowasaidia kutambua irabu.
Anasema, “Hatua ya kwanza kujifunza kusoma na kuandika ni kutambua irabu na tarakimu. Hapa mzazi anahitajika kumnunulia mtoto mabango (poster) yenye irabu na tarakimu. Mtoto ataanza kuzoea zile irabu na huo ndio mwanzo wa kujifunza kusoma na kuandika.”
Ushauri huu wa kitaalam ni wa msingi kwa wazazi wanaotamani kuona watoto wao wanajifunza kusoma mapema. Badala ya kumnunulia mtoto midoli isiyomsaidia kujifunza, mtafutie mtoto vifaa vinavyohusianisha picha na maneno. Unapopata nafasi, mwelekeze. Hatua kwa hatua mtoto atajifunza kusoma.  
Vifaa vya kuandikia
Upendo Zakaria, mkufunzi wa Chuo cha Ualimu Singachini, naye anashauri wazazi wawape watoto vifaa vya kuandikia. Anasema, “Unaweza kumpatia mtoto kalamu na penseli akajifunza namna ya kuishika.”
Katika hatua za ukuaji wa mtoto, kwa kawaida mtoto anaweza kuanza kushika kitu vizuri kwa vidole vyake katika umri wa miaka mitatu. Kwa nini ni muhimu mtoto aanze kuzoeshwa kushika kalamu mapema?
Mkufunzi Upendo anajibu: “Kushika kalamu ni mazoezi ya kukomaza misuli ya mikono na vidole. Mtoto hawezi kuandika kama misuli yake miepesi (smooth muscles) haijakomaa vizuri.”  
Desturi ya kusoma nyumbani
Doris Lyimo, mhadhiri wa lugha Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge, anafikiri ni muhimu kujenga desturi ya kusoma katika mazingira ya nyumbani.
Anasema: “Mtoto huiga kwa mzazi kama anayo desturi ya kusoma. Lazima mzazi amwongoze mtoto kusoma kwa kuhakikisha si tu na yeye anaonekana akisoma, bali nyumba ina vitabu na magazeti ya kusoma”
Pia kuna suala la maagizo tunayowapa watoto wetu kama anavyofafanua Jema Karume, anayeandaa walimu wa shule za msingi: “Mzazi ampe mtoto maagizo yanayochochea kufikiri na kuhesabu. Mfano, unamwambia mtoto niletee vijiko viwili. Hapo unamlazimisha kujifunza kuhesabu vitu.”
Vitabu vya hadithi
Bahiya Abdi, ambaye pia amekuwa akifanya tafiti kadhaa za kubaini mazingira yanayorahisisha kusoma na kuandika, anashauri wazazi wawapatie watoto vitabu vya hadithi fupi fupi. Anasema:
“Nunua vitabu kwa ajili ya mwanao. Mtafutie vile vitabu vya hadithi fupi fupi za kusisimua ajenge mazoea ya kusoma. Wewe kama mzazi msikilize wakati anasoma na kisha mwuulize maswali ajibu.”
Utaratibu kama huu ukifanyika mara kwa mara una nafasi kubwa ya kumjengea mtoto hamasa ya kujifunza kusoma kwa umahiri zaidi. Mbali na kumfundisha kusoma, mtoto anakuwa na uwezo wa kuelewa kile anachokisoma kwa ufasaha zaidi.
Je, hadithi zinawafaa wale wanaojua kusoma pekee? Mhadhiri Bahiya anasema:
“Vitabu vinawafaa hata watoto wasiojua kusoma. Kama mtoto bado hajui kusoma, msomee hadithi na yeye asikilize. Ukishamsomea ni muhimu umpe nafasi aulize maswali yanayohusu hadithi hiyo.”
Michezo
Mhadhiri Bahiya Abdi anafikiri michezo nayo ina nafasi muhimu katika kumwandaa mtoto kusoma na kuhesabu. Anasema, “Wazazi wanatakiwa kuwahamasisha watoto kucheza michezo inayowasaidia kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu. Mfano, mchezo wa kuruka kamba ilihali wakihesabu.”
Jema Karume naye anaungana na ushauri huo wa Mhadhiri Bahiya: “Wazazi wasichukulie michezo kama kupoteza muda. Kupitia michezo mtoto atajifunza kuhesabu vitu vingi. Muhimu tu iratibiwe vizuri na ifanyike kwa muda muafaka.”
Tunafahamu watoto hucheza kwa makundi. Wanapojigawanya kwa makundi ya ushindani, watahesabu idadi yao kwa kila kundi.
Pia, watahesabu idadi ya magoli, mitupo, makosa yanayofanyika na mambo kama hayo ambayo kwa hakika yana nafasi kuwa ya kuwa darasa lisilo rasmi linalowajengea watoto ujuzi wa hesabu kabla hata hawajaandikishwa kwenda shule.

Maoni

  1. SAHABATPOKER AGEN BANDARQ AGEN DOMINO 99 DAN POKER ONLINE AMAN DAN TERPERCAYA
    Susah cari Situs judi online yang bisa di percaya...?
    Mari gabung di AGEN DOMINO
    Bonus Refferal 15%
    Bonus Turn Over 0,5%
    Agen Judi Online Terbesar dan Terpercaya se asia
    Daftar dan buktikan sendiri sekarang juga..
    WHATSAPP : +855967136164
    PIN BB : 2B13CFD
    PIN BB : E34BB179
    LINE ID : @fjq9439d
    LINE ID : sweetycandys

    JibuFuta
  2. TIPS MERAWAT AYAM BANGKOK ADUAN PEMAINAYAM,ORG

    BOLAVITA adalah situs permainan SABUNG AYAM ONLINE TERPERCAYA INDONESIA.

    LINK DAFTAR : Agen Sabung Ayam Online Terpercaya

    Dengan jumlah deposit yang sangat terjangkau kalian sudah bisa bermain berbagai permainan yang disediakan oleh situs kami.
    Minimal Deposit 50 Ribu
    Minimal WD 50 Ribu

    Menerima Deposit Via PUlsa, E-money ( OVO, DANA, GOPAY, LINKAJA)

    Buruan Join Sekarang Bersama Kami di BOLAVITA Situs Judi Online Terbaik Indonesia.

    Kontak WHATSAPP : 0812-2222-995

    TIPS AYAM BANGKOK ADUAN LENGKAP!!!

    Cara Merawat Ayam Bangkok Saat Cuaca Hujan

    JibuFuta
  3. Apakah kamu sedang mencari prediksi togel jitu ? cek blog kami di sini >
    Prediksi Togel SGP 29 November 2021

    JibuFuta
  4. MUSEUMTOTO - WEBSITE RESMI TARUHAN BOLA ONLINE INDONESIA

    PROMO DEPOSIT PULSA | DEPOSIT VIA OVO DANA GOPAY LINKAJA JENIUS SAKUKU

    SPECIAL BONUS :
    *BONUS WELCOME SEBESAR 20%
    *BONUS DEPOSIT HARIAN 5%
    *BONUS ROLLINGAN 0.5%
    *BONUS CASHBACK 10%
    *hingga masih banyak bonus lainnya ,
    Silahkan klik link Promo => PROMO MUSEUMTOTO

    LINK DAFTAR => DAFTAR
    atau
    HUBUNGI KAMI => WHATSAPP : +6287777007391

    JibuFuta
  5. Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
    * upendo
    inaelezea * inaelezea kivutio
    * kama unataka ex wako nyuma
    *acha talaka
    *kuvunja mawazo
    * huponya viharusi na magonjwa yote
    * uchawi wa kinga
    *Ugumba na matatizo ya ujauzito
    * bahati nasibu
    * bahati nzuri
    Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
    Whatsapp:+2349046229159

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia