Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2017

Umuhimu wa Kumpunguzia Mtoto Shinikizo la Kufaulu

Picha
PICHA: Stressed Out Students Ufaulu wa mitihani umepewa nafasi ya pekee katika mfumo wetu wa elimu. Shule zetu, kwa hakika, hazina namna nyingine ya kumwelimisha mtoto zaidi ya kumtaka akusanye, akumbuke na kutumia maarifa aliyonayo kujibu maswali ya mtihani. Ingawa ustawi wa jumla wa mwanadamu hautegemei eneo hilo moja la ukusanyaji na utumiaji wa maarifa, shule zetu zinaonekana kuamini pasipo mtu kuwa na maarifa mengi hawezi kufanikiwa.

Ufanyeje Kijana Chipukizi 'Anapokata' Mawasiliano na Wewe?

Picha
PICHA:  Parent Pump Radio Kama nilivyoeleza kwenye makala yaliyopita, tofauti za kimtazamo kati ya mzazi na kijana anayechipukia ni hali zinazotarajiwa. Wakati mwingine tofauti hizi zinaweza kuonekana kama mambo madogo yasiyo na msingi. Lakini tofauti hizi zinazoonekana kuwa ndogo zisiposhughulikiwa zinaweza kukomaa na hatimaye kusababisha matatizo makubwa. Wazazi, mara nyingi, hatupendi kuzipa uzito tofauti hizi mara zinazopoanza kujitokeza. Kijana wako anaweza kuanza kuwa mkimya bila sababu za msingi, anaanza kukukwepa na hata kupunguza mawasiliano na wewe, lakini ukachukulia ‘kawaida.’

‘Homework’ Zinavyodumaza Ukuaji wa Watoto Wadogo

Picha
PICHA:  PhillyVoice Ukiwauliza wazazi kitu gani wanafikiri kikisitizwa mapema zaidi kwa watoto kitawasaidia kufanikiwa, wengi  watakwambia elimu. Kwa sababu hiyo, wazazi hasa wasomi wanaharakisha kuwapeleka shule watoto wenye umri mdogo. Ninawafahamu watoto wengi wa miaka minne wanaosoma darasa la kwanza. Wazazi wa watoto hawa wanafanya hivyo wakiamini mtoto akisoma mapema, maana yake uwezekano wa kufanikiwa maishani unakuwa mkubwa.

Maswali Matano Yatakayokusaidia Kujua Thamani ya Kazi Yako

Picha
Nianze kwa kukuuliza swali rahisi. Kitu gani kinakupa motisha ya kuamka asubuhi na kwenda kazini? Unafikiri nini hasa kinaongeza thamani ya kazi yako? Kwa mujibu wa tafiti, takribani asilimia 80 ya watu wanaofanya kazi za kuajiriwa au kujiajiri hawapati utoshelevu. Kwa hakika mambo mengi yanachangia watu kutokupenda kazi zao. Kuna migororo kazini, kutokufikia matarajio waliyokuwa nayo na wakati mwingine mazingira hafifu ya kazi. Pia, sababu nyingine ni kutokuona namna gani kazi anayofanya mtu inakidhi makusudi mapana ya maisha yake. Katika mazingira haya, ni vigumu kuona thamani ya kazi yake na hivyo itakuwa vigumu kutosheka. Mtu anayependa kazi yake mara nyingi anakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuwa mbunifu, kuwa na bidii zaidi na hivyo kupata matokeo mazuri kuliko mtu anayesukumwa kufanya kitu asichoona thamani yake. Kwa kuzingatia ukweli huo, katika makala haya tunaangazia maeneo matano yanayoweza kukusaidia kuelewa kwanini kazi unayoifanya inaweza kuwa na

Hisia Zilizojeruhiwa Zinavyoweza Kujenga Ukatili Usiotarajiwa

Picha
PICHA: Pride News Magazine Baraka amekuwa akilalamikiwa kwa tabia yake ya udokozi tangu akiwa darasa la tatu. Ingawa alikuwa mdogo kwa umbo, jina lake maarufu lilikuwa ‘Baraka kibaka.’ Mbali ya kuwa kibaka, baraka alikuwa mgomvi aliyepambana na karibu kila mwanafunzi shuleni.

Mbinu za Kumshirikisha Mwanafunzi Katika Ujifunzaji

Picha
PICHA:  United Nations Majuzi niliwatembelea walimu wanafunzi waliokuwa wakiendelea na mazoezi ya ufundishaji. Mafunzo kwa vitendo yana umuhimu wa kipekee katika maandalizi ya walimu. Katika kipindi hiki, mwanafunzi anapewa fursa ya kutumia maarifa aliyojifunza darasani katika mazingira halisi ya kazi. Kwa mwalimu, kama mimi, hiki ni kipindi cha kutathmini uwezo wa mwanafunzi wa ualimu kumudu majukumu yake. Moja wapo ya vipindi vingi nilivyopata bahati ya kuhudhuria ni Baiolojia kidato cha III kilichokuwa kikifundishwa na mwanafunzi wangu wa mwaka wa II. Baada ya kufanya utangulizi wa somo lake, mwalimu huyu mwanafunzi aliwaelekeza wanafunzi wake kukaa katika makundi ya watu watano watano kusudi wafanye majadiliano. Majadiliano ni mbinu muhimu ya ufundishaji inayowawezesha wanafunzi kujifunza. Kama tulivyosema kwenye makala yaliyopita, kupitia majadiliano, mwanafunzi hupata fursa ya kusikiliza mtazamo tofauti kutoka kwa wenzake. Aidha, majadiliano ni mbinu

Mbinu za Kuchagua Kazi Itakayokupa Utoshelevu

Picha
Maamuzi ya kazi gani ufanye ni moja wapo ya mambo ya msingi yanayoathiri maisha ya mtu. Kazi iwe ya kujiajiri au kuajiriwa ndiyo maisha yako. Muda unaoutumia ukiwa kazini unaweza kuwa mwingi kuliko muda unaoutumia ukiwa kwingineko. Maana yake ni kwamba unapofikiri kazi ipi uifanye kimsingi unafanya maamuzi yatakayoathiri mfumo mzima wa maisha yako.

Mbinu za Kujenga Ujuzi wa Mwanafunzi

Picha
PICHA: Shutterstock Nakumbuka siku ya kwanza kusikia neno ‘cell’ nikiwa kidato cha kwanza haikuwa kazi rahisi kupata picha kamili. Mwalimu wetu aliandika ubaoni, ‘ cell is a basic unit of life .’ Niliduwaa. Sikujua anamaanisha nini zaidi ya kutazama kamusi kujua maana ya maneno aliyoyatumia. Mwalimu alirudia maneno hayo hayo kuweka msisitizo, na kisha akatafsiri kwa Kiswahili. Alisema, ‘maana yake ni hivi kuna kitu kidogo kisichoonekana kwa macho kwenye miili yetu kinachofanya tuishi. Mmeelewa?’  Kwa kweli hatukuwa na namna nyingine zaidi ya ‘kuelewa’ na tukaitikia, ‘ndiyo!’

Vyuo Vikuu Vinawajibika Kukuza Ujuzi wa Wahitimu Wake

Picha
Kukosekana kwa ujuzi unaohitajika katika soko la ajira ni moja wapo ya sababu kubwa zinazochangia ukosefu wa ajira unaoendelea kuwa tatizo hapa nchini. Akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya uanangezi mjini Dodoma wiki iliyopita, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema waajiri wengi wamekuwa wakilalamika kuwa vijana wengi wanaoingia kwenye soko la ajira wanakosa ujuzi unaohitajika katika kazi.

Mwalimu Anavyoweza Kukuza Uelewa wa Mwanafunzi

Picha
PICHA: Sunday Adelaja Dhima kuu ya elimu iliyo bora ni kuzalisha raia wenye sifa ya udadisi. Hawa ni raia wanaofikiri kwa makini, wanaohoji mazoea, wasioridhishwa na majibu yaliyozoeleka na wenye ari ya kutafuta majibu ya changamoto zinazoikabili jamii yao. Hatua ya kwanza ya mwanafunzi kuwa mdadisi ni kuelewa kile alichojifunza. Mwanafunzi asiyeelewa maudhui ya somo, hawezi kuwa na fursa ya kufanya udadisi.

Sababu za Watu Kufanya Uchaguzi Mbaya wa Kazi

Picha
Uchaguzi wa kazi ni maamuzi anayoyafanya mtu kuanzia pale anapopata wazo la kazi anayotaka kuifanya mpaka anapostaafu. Haya ni maamuzi anayoyafanya mtu kutimiza ndoto zake kimaisha tangu anapokuwa masomoni; anapoomba kazi kwa mara ya kwanza na kuipata; anapobadilisha kazi na hata pale anapofikia umri wa kustaafu kazi.

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Picha
PICHA: thesouthern.com Siku moja nikiwa kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanafunzi wa shahada za awali waliingia kufanya mtihani wa muhula wa mwisho wa masomo. Wakati wanaingia, mmoja wao alijigamba kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kukanyaga maktaba tangu amejiunga na chuo hicho miaka mitatu iliyopita. Nilishangaa inawezekanaje mwanafunzi wa chuo kikuu kujisifia jambo la fedheha kama hilo.

Namna ya Kutambua Kazi ya Wito Wako

Picha
Kuna mawazo yanapandikizwa kwenye fahamu za vijana kuwa mafanikio hayaji bila mtu kufanya aina fulani ya kazi. Wahubiri wa mawazo haya wanapima tija na heshima ya kazi kwa mizani ya kipato. Mtazamo huu,   kwa kiasi kikubwa, unachochewa na mfumo wa kibepari unaotukuza faida anayopata mtu binafsi dhidi ya manufaa mapana ya jamii. Katika mfumo huu, mtu anaweza kufanya kazi yoyote almuradi inamnufaisha yeye binafsi.

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -2

Picha
PICHA: Shutterstock Katika makala yaliyopita tuliona mbinu tatu unazoweza kuzitumia kuelewa mambo unayojifunza. Kwanza, ni ‘njaa’ inayokusukuma kuelewa. Unapokuwa na ari ya kuelewa jambo, mara nyingi, utahamasika kulielewa bila kutumia nguvu nyingi. Pili, tuliona ni muhimu kutengeneza picha kubwa ya jambo unalojifunza kabla hujaanza kujifunza undani wa mambo madogo madogo ndani ya picha hiyo. Kwa mfano, unaposoma aina za vyakula, lazima kwanza uelewe vyakula. Uelewa wa jumla wa vyakula utakurahisishia kazi ya kuchanganua aina zake kwa sababu tayari unayo rejea utakayoitumia kuelewa zaidi. Mbinu ya tatu ni kukihusisha kitu unachokisoma na mambo unayoyafahamu tayari. Unaposoma aina za vyakula, kwa mfano, lazima uwe unafikiria vyakula mbalimbali unavyovifahamu katika mazingira yako. Unapojaribu kuhusianisha kile unachokisoma na maisha yako ya kila siku, unaurahisishia ubongo wako kazi ya kupokea kuliko kuingiza kitu kipya kisichohusiana kwa vyovyote vile na kile

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma

Picha
PICHA: Oxford Learning Kusoma kitu usichokielewa ni hasara. Mbali na kuongeza uwezekano wa ‘kupigwa chenga’ wakati wa mtihani, kutokuelewa kunaharibu dhima ya elimu. Mtu asiyeelewa kile alichojifunza, kwa mfano, hawezi kutumia maarifa aliyonayo kuleta tija kwa jamii.

Kinachofanya Wanafunzi Wasielewe Wanachokisoma

Picha
PICHA:  SciTech Daily Ujifunzaji (learning) ni mchakato wa kupata uzoefu mpya katika maeneo makubwa matatu. Kwanza, kubadili namna mtu anavyofikiri. Maarifa mapya huja na uzoefu mpya unaobadilisha uelewa wa mambo.

Elimu Isinoe Ufahamu Pekee, Itufanye Tuwe Binadamu Timamu Wanaojitambua

Picha
PICHA: EDUCATION / BUNKIE BILA shaka umewahi kukutana na mtu unayeamini ni msomi akifanya mambo usiyoyatarajia. Jambo hilo hilo lingefanywa na mtu asiyekwenda shule wala usingeshangaa. Lakini kwa kuwa anayefanya hivyo ni ‘msomi’  basi unakata tamaa na kuhoji, “Hivi huyu naye amesoma? Kama kusoma kwenyewe ndio huku, basi hakuna haja ya kusoma.”