Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma
Kusoma kitu
usichokielewa ni hasara. Mbali na kuongeza uwezekano wa ‘kupigwa chenga’ wakati
wa mtihani, kutokuelewa kunaharibu dhima ya elimu.
Mtu asiyeelewa kile
alichojifunza, kwa mfano, hawezi kutumia maarifa aliyonayo kuleta tija kwa jamii.
Elimu kwa mtu huyu
inabaki kuwa na maana ya ‘kumeza’, ‘kutapika ulichomeza’ na kufaulu mtihani. Baada
ya hapo, mtu huyu anasahau kila alichojifunza na maisha yanaendelea. Elimu ya
namna hii, kwa hakika, haiwezi kuwa na tija.
Pengine unaweza kuuliza,
kuelewa maana yake nini? Kwa lugha nyepesi, kuelewa ni uwezo wa kujifunza
maarifa mapya kwa namna inayokuwezesha kuyamiliki maarifa hayo.
Unapomiliki maarifa
maana yake unayafanya kuwa sehemu ya maisha yako na hivyo kujiweka kwenye
nafasi nzuri zaidi ya kuyatumia maarifa hayo katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto
zinazoikabili jamii yako.
Katika makala yaliyopita
nilieleza baadhi ya makosa yanayochangia kuwafanya wanafunzi washindwe kuelewa
kile wanachojifunza. Nami kwa wakati fulani, niliwahi kukariri. Nilitumia muda
mrefu ‘kumeza’ mambo nisiyoyaelewa.
Hata hivyo, baadae nilibadilika
na kujifunza namna bora ya kusoma. Ninaamini nilichojifunza kila mwanafunzi anaweza
pia kujifunza na akabadilika.
Katika makala haya, ningependa
kukushirikisha baadhi ya mbinu zinazoweza kukusaidia kubadilika na hatimaye
uelewe kile unachokisoma.
Nini kinakupa motisha?
Motisha ni msukumo
ulioko ndani yako unaokusukuma kufanya kitu. Njaa, kwa mfano, inaweza kuwa
motisha ya kumsukuma mtu kutafuta chakula. Bila njaa, huwezi kula.
Ndivyo ilivyo kwa
mwanafunzi. Usipokuwa na ‘njaa’ ya kujifunza, hutaona sababu yoyote ya kukufanya
uelewe kile unachofundishwa. Ili uweze kufanyia kazi mapendekezo yanayofuata,
lazima kwanza uwe na msukumo wa kutosha ndani yako.
Niliwahi kusoma na bwana
mmoja ambaye siku hizi ni daktari bingwa. Tangu tunaingia shuleni siku ya
kwanza, bwana huyu alionekana kuwa na shauku kubwa ya kujifunza. Wakati sisi
wengine tukiendelea kuzoea mazingira ya shule huyu bwana tayari alikuwa anasoma.
Hakusubiri mwalimu
aingie darasani kumwambia nini cha kusoma. Tayari alikuwa na mhutasari
(syllabus) wa kila somo na ratiba ya nini cha kusoma. Hii ndiyo inaitwa ‘njaa’
ya kujifunza. Usipokuwa nayo, hakuna mtu anaweza kukufundisha mbinu za kusoma
kwa bidii.
Je, unayo sababu yoyote
ya kukufanya usome kwa juhudi? Fikiria namna gani ufaulu mzuri wa masomo yako
unavyoweza kubadili maisha yako siku za mbeleni. Fikiria utoshelevu
utakaojisikia utakapoweza kutumia elimu yako kugusa maisha ya watu katika
jamii.
Fikiria jitihada alizofanya
mzazi wako kukupeleka shule kama aina ya urithi anaoamini ndio muafaka zaidi
kwako. Fikiria ndoto zinazokusukuma kuwa shuleni. Je, una ndoto za kufanya nini
baada ya maisha ya shule?
Ndoto hizo, kwa kiasi
kikubwa, zinategemea yale unayoyafanya leo kama mwanafunzi. Ukishindwa kufaulu
mtihani au kutumia kile unachokijua itakuwa vigumu kuziishi ndoto zako hizo.
Uhusiano huo wa masomo
na ndoto zako uamshe ‘njaa’ ya kujifunza. Bila ‘njaa’ hiyo ya kufikia malengo
yako, itakuwa vigumu kufurahia masomo yako.
Jambo la kuzingatia ni
kwamba, uelewa wako, kwa kiasi kikubwa, unategemea hisia zako. Kitu
usichokipenda akili hukizuia kisipate nafasi ya kusumbua yale unayoyapenda. Anza
kupenda masomo yako utaona namna ‘njaa’ ya kujifunza na kuelewa itakavyokuwa
kubwa.
Husianisha na unachokijua
Kwamba umeweza kusoma
makala haya mpaka hapa, maana yake una motisha ya kutosha kutaka kujua mbinu za
kuelewa. Hiyo, hata hivyo, haimaanishi kwamba lazima utazielewa. Motisha na
uelewa ni mambo mawili tofauti ingawa yanahusiana.
Tukirejea tuliyoyajadili
kwenye makala iliyopita, kikwazo kimoja wapo cha wanafunzi wengi kutokuelewa
masomo ni kukariri.
Kukariri maana yake ni
kuilazimisha akili kukumbuka kitu kisichohusiana na maarifa yaliyoko kwenye
ufahamu wako tayari. Ili kulazimisha akili ishike, wanafunzi wengi husoma vitu
vingi vidogo vidogo ambavyo kwa hakika mara nyingi huwa havina uhusiano wowote.
Mtu anayekariri masomo
ni sawa na mtumiaji wa simu anayejaribu kuweka kichwani tarakimu 15 za vocha
yenye muda wa maongezi. Kwa vyovyote vile itakuwa kazi ngumu kukumbuka tarakimu
hizo kwa sababu hazina uhusiano wowote baina yao.
Kwa hiyo kama unataka
kuelewa, hatua ya kwanza ni kuhakikisha kile unachokisoma kwa namna moja au
nyingine kinafanana na kitu ambacho tayari unacho kwenye ufahamu wako.
Namna nzuri ya
kuhakikisha hilo linawezekana ni kuhusianisha mambo unayoyasoma na maisha yako
ya kawaida. Hakuna maarifa yasiyolenga kufananua mambo ya kawaida tunayoyaona
kila siku. Kazi yako, kama mtu anayejifunza, ni kuhakikisha unasoma mambo kwa
kutumia miwani ya maisha yako ya kila siku.
Fikiria namna gani mambo
hayo unayoyasoma yanafanana na mambo unayoyasikia, unayoyaona na pengine
unayoamini. Fikiria namna kile unachokisoma kinavyooana na uzoefu wako wa kila
siku.
Tengeneza wazo kuu kwanza
Unapoanza kusoma, unahitaji
kwenda hatua kwa hatua. Kwanza kabisa, soma kupata wazo kuu utakaloliingiza
kichwani. Wazo hili kuu ndilo litakalotumiwa na akili yako kama rejea kadri
unavyoendelea kusoma.
Hatua inayofuata ni
kujua undani wa wazo ulilolitengeneza tayari. Kazi hii ya kuelewa undani wa
wazo kuu haitakuwa ngumu kwa sababu tayari akili yako itakuwa imeshachora kitu
itakachokirejea.
Kwa mfano, unaposoma
kazi za ‘nucleus’ kwenye seli, lazima uwe unajua seli yenyewe inafanya nini na
inahusianaje na maisha yako ya kila siku. Usipofanya hivyo, kazi yako haitakuwa
tofauti sana na mtu anayejaribu kukumbuka tarakimu 15 za vocha ya muda wa
maongezi.
Kadri unavyosoma, unayo
maswali mawili makubwa ya kujiuliza. Kwanza, namna gani hiki ninachokisoma
kinafanana na kile ninachokijua tayari. Kama unachokisoma hakifanani na kile
unachokifahamu tayari, maana yake unakariri.
Swali la pili, ni namna
gani hiki ninachokisoma kinatofautiana na kile ninachokijua tayari. Kama huoni
tofauti maana yake, hujifunzi na utasahau kabla hujamaliza.
INAENDELEA
Safi sana mwakimi hakika makala zako ni nzuri
JibuFutaSafi sana mwakimi hakika makala zako ni nzuri
JibuFutahttp://jurnaldikbud.kemdikbud.go.id/index.php/jpnk/comment/view/717/0/0?refresh=1
JibuFutadompetcasino.org online casino agent is essential if people want to work on online gambling. http://www.dompetcasino.net/ to make the play scene should really be done so that the smoothness in playing gambling can be enjoyed gambling agency sites online casino agency page can also be done with a system of observing recommendations and recommendations from more experienced players.
judi online
pokerstar365.net is a card game that shares betting rules and is usually (but not always) in hand ranking. The Poker Online game is different in terms of how cards are shared. In the most modern Poker Games, the first round of betting starts with several forms. Type of card arrangement in Online Poker.
poker online
Asantee nitumie MB
JibuFuta