Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2012

Waholanzi na utamaduni wa baiskeli, sisi tunakimbilia magari binafsi

Picha
Wakati sisi tunashindana kwenda kazini na magari ya bei mbaya, wenzetu wanakuja kazini na baiskeli. Hapa ni Ede, Uholanzi. Baiskeli ndio usafiri maarufu. Jambo hili si la kawaida. Fikiria, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu achilia Profesa wake, apande baiskeli kwenda chuoni. Kwa hakika ni jambo unaloweza kuliewa pale Dar es salaam.


Katika mazingira haya ambapo kila mtu anatafsiri maendeleo kwa kuangalia vitu, na katika mazingira ambayo kila mtu yuko tayari kuonekana naye yupo hata ikibidi kwa mkopo, almuradi aendeshe gari, ni vigumu kupata ufumbuzi wa 'kero' ya kudumu ya foleni jijini Dar es Salaam.  Kila mmoja anafikiri kutatua kero hii kwa kuongeza gari barabarani.


Hebu fikiri kama watu wangeamua kutumia usafiri wa umma, huu huu uliopo, magari mangapi yangeondoka barabarani? Saa nyingine, inachekesha. Magari 40 yanayohangaika kupenya kwenye mataa ya Ubungo yanaweza kuwa yamebeba abiria kati ya 40-42! Kila gari, mtu mmoja! Hivi hao wote akiamua kupanda baiskeli au k…

Mitaa ya Nairobi kwa jicho langu

Picha

Mitaa ya Nairobi, 'Usomini UoN'

Picha

Nilipokutana na Mshairi Serina wa Upande Mwingine

Picha
Katika mkutano wa wanablogu na waandishi wa habari za kiraia uliofanyika Nairobi, Kenya, nimebahatika kukutana na mwanablogu niliyekuwa na hamu sana ya kuonana naye. Naye si mwingine bali, dada Serina Kalande, anayetuandikia kwenye blogu ya Upande mwingine.

Ni dada mkarimu, mpole, mwanana na mwema sana kuzungumza naye. Serina, asante kwa baraka ya kukuona.

Mgomo wa Mabasi ya Abiria Mjini Moshi

Picha
Wakazi wa Manispaa ya Moshi na vitongoji vyake leo wameonja adha ya kukosa usafiri kufuatia mgomo wa mabasi  yanayotoa huduma ya usafiri mjini hapa, maarufu kama daladala. Mgomo huo umetokea kama hatua za waendeshaji wa huduma hiyo kupinga kupanda kwa kiwango cha ushuru kilichotangazwa na Halmashauri ya Manispaa hiyo.


 Kwa  mujibu wa tangazo la Halmashauri hiyo inayoongozwa na CHADEMA, ushuru huo umepanda kwa asilimia 50 kutoka Tsh. 1000 zilizokuwa zikilipwa awali mpaka Tsh 1500 zinazotakiwa kuanza kulipwa mara moja.

Tayari Katibu wa CHADEMA mkoani Kilimanjaro, Bw. Lema, kupitia Radio za FM mjini hapa ametoa tamko la kupinga vikali ongezeko hilo, akiliita kuwa 'hujuma' inayofanywa na baadhi ya watendaji wa Halmashauri hiyo inayoongozwa na chama chake kuonyesha kuwa kimeshindwa kazi.

Blogging Revolution: Shubiri kwa wajiitao serikali

Picha
Kitabu kizuri kinachoangazia mabadiliko ya kijamii na kisiasa yaliyoletwa na matumizi ya zana za uandishi wa kiraia hususani blogu.
 Kinatazama namna blogu zilivyochangia Mapinduzi yanayoendelea katika nchi za kiarabu –maarufu kama Arab Spring – na jinsi ambavyo blogu hizi zinaanza kuwatia hofu watu wanaojiita serikali.

Umemsoma Dambisa Moyo?

Picha
Kama una mpango wa kusoma kitabu kimoja tu mwaka huu, napendekeza hiki cha Dambisa Moyo kiitwacho "How the West was Lost". Ukikisoma utaelewa zaidi kwa nini hawa watawala wanaoitwa "The darling of the west" wanaopigana vikumbo kuhudhuria mkutano wa G8, wamepotea njia. Anacho kingine alichokiandika kabla ya hiki, kiitwacho cha Dead End, bado nakitafuta. Naambiwa ni moto.

Mafanikio ni umiliki wa muda wako

Picha
Mafanikio ni nini? Ajira ya uhakika? Uhakika wa mapato? Uhakika wa pensheni? Ongezeko la muamala mwisho wa mwezi? Tarakimu za shilingi kuongezeka? Kwa gharama ya kunyang'anywa muda wako? Si unajua? Kadri ziongezekavyo ndivyo uuzavyo muda wako?


Mafanikio.... Ni madaraka kazini? Madaraka yaendanayo na ubize? Kutwa u ziarani? U angani kikazi?
Waondoka alfajiri, warudi usiku? Wanao hawakuoni? Mwenza yu mpweke? Haidhuru... Nyumba yanukia noti sio? Shilingi bila muda, kazi yake nini?Mafanikio... Ni kuongezeka kwa kibaba? Ankara zalipika kibaba kinabaki? Ni uhuru wa muda wako? Uhuru wa kujenga familia kwa karibu? Mwenzi achekelee? Wana wasome? Uifaidie jamii?
Sadaka utoe? Wenye shida wakukimbilie?


Si unajua lakini...? Bila shilingi hayo si mepesi? Shilingi yatatua vingi Muda bila shilingi, wa nini? Muda unao unachotatua hakionekani? Na wadai umefanikiwa? Kivipi?

Hujanielewa... Mafanikio ni kuwa na vyote Ni thamani ya muda wako Hiari ya matumizi ya muda wako Mafanikio ni... Mfumo uku…

Nani yu huru?

Picha
Wakurupuka alfajiri, haraka wende kazini Wajutia kuliacha shuka, waogopa kuchelewa Ukifanyacho kimepangwa, mpangaji ni mwajiri Muda ulohisi wako, ukweli si wako Mwajiri kaununua nira kakufungia Wajisifu na ajira?Uhuru ni nini na aliye huru ni nani? Aliyehuru hufugwa na mwingine, ati? Aliye huru yuna muda Cha kufanya akipanga yeye, pa kwenda haamrishwi Huenda atakako kwa hiari ya muda wake Hupata mkate wake pasipo mauzo ya muda wake U huru?

Mtumwa aongozwa na bwana wake Hiari na aendako hanayo Kazini ni lazima Ujira huupata kwa kuuza uhuru wake Hana mamlaka na muda alodhani wake Muda wake kauuza kwa mwajiri Nira kakabidhiwa
Mabega yote juu, meno yote nje
Ajisifu ana ajira!


Upendacho kukifanya, huthubutu kukifanya Si wajua hakikupi muamala? Usichopenda ndo' wakifanya kupata mkate wako Kwa gharama ya muda wako mkate waupata Muda huna shilingi wapata Shilingi wapata kwa kumtumikia mwajiri Na wadai u huru?