Nani yu huru?

Wakurupuka alfajiri, haraka wende kazini
Wajutia kuliacha shuka, waogopa kuchelewa
Ukifanyacho kimepangwa, mpangaji ni mwajiri
Muda ulohisi wako, ukweli si wako
Mwajiri kaununua nira kakufungia
Wajisifu na ajira?

Mwajiriwa akilinda kibarua chake|Picha ya picturesof.net
                                     


















Uhuru ni nini na aliye huru ni nani?
Aliyehuru hufugwa na mwingine, ati?
Aliye huru yuna muda
Cha kufanya akipanga yeye, pa kwenda haamrishwi
Huenda atakako kwa hiari ya muda wake
Hupata mkate wake pasipo mauzo ya muda wake
U huru?


Mtumwa aongozwa na bwana wake
Hiari na aendako hanayo
Kazini ni lazima
Ujira huupata kwa kuuza uhuru wake
Hana mamlaka na muda alodhani wake
Muda wake kauuza kwa mwajiri
Nira kakabidhiwa
Mabega yote juu, meno yote nje
Ajisifu ana ajira!



Upendacho kukifanya, huthubutu kukifanya
Si wajua hakikupi muamala?
Usichopenda ndo' wakifanya kupata mkate wako
Kwa gharama ya muda wako mkate waupata
Muda huna shilingi wapata
Shilingi wapata kwa kumtumikia mwajiri
Na wadai u huru?


****************************************

Pasina muda swahiba huwezi kuwa uhuru

Maoni

  1. Kutokana na shauku kusema kweli hata sijasoma ulichoandika. Kwanza nataka kukulaki kwa furaha zote kwa kurejea hapa nasi ...karibu sana kaka Bwaya..yaani wewe ni mwiko kukufikiria nilipanga kesho nikutangaze na nipeleke tangazo kwa polisi ila umewahi ..ntarudi kesho kutoa maoni ya mada...

    JibuFuta
  2. Ha ha ha haaaa! Upo dada Yasinta? Nimefurahije kuonana na wewe saa hizi? Karibu mwaka ati! Yaani ndio kwanza nafuta futa vumbi ndani ya nyumba iliyohamwa siku nyingi, hata dekio lenyew sijashika, mara jirani wabisha hodi? Asante sana kwa mapokezi moto moto. Ngoja nikague usalama tutalizana za siku!

    JibuFuta
  3. sikuzote sio rahisi kwa mtanzania kufikiria juu ya uhuru wake yeye mwenyewe kinachojaliwa sana ni pesa na kujikimu kimaisha unajukumu lingine kubwa la kusama ni kwa vipi basi mtu aweza pata huo uhuru

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?