Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2016

Nani Awezaye Kutuletea Mabadiliko Tunayoyataka?

Picha
Ukisikiliza mazungumzo ya wa-Tanzania  –iwe vijiweni, mitaani, mitandaoni ama kwingineko –ni wazi wengi wetu tunayo hamu ya mabadiliko. Tuna shauku ya zama mpya. Shauku hiyo ya mabadiliko imetufanya wengi wetu tutumie muda mwingi kutafuta watu tunaohisi ‘wanatukwamisha.’ Ni hivyo kwa sababu tumejijengea dhana kwamba ili kupata mabadiliko tunayoyataka tunahitaji watu maalum wenye uwezo wa ‘kutuletea maendeleo’. Kwa hiyo ni kama tunasubiri wakombozi fulani fulani waje kutubadilishia mfumo tunaoamini ndio tatizo.

Madikteta wa Familia Tunaweza Kudai Demokrasia?

Picha
Madai kuwa baadhi ya watawala wetu wa ki-Afrika ni madikteta hayashangazi. Inasemekana watawala hawa  hawasikilizi maoni ya watu wanaowaongoza, hawashauriki wakati mwingine na watu walioteuliwa kuwashauri, wanaminya uhuru wa maoni/kujieleza na kadhalika. Madai haya yanaonekana kuwa ni matamanio ya wananchi kuwa na serikali zinazoheshimu demokrasia -nguvu ya wananchi kushiriki katika uongozi/utawala wa taifa lao kwa kuamua utaratibu gani utatumika kujitawala na nani anaweza kupewa jukumu la kuwaongoza. Haya yote yanadai ushirikishwaji wa wananchi kwa kukuza uhuru wa kila raia kusema/kutoa maoni na kadhalika.