Mambo ya Kutafakari Unapoanzisha Uhusiano wa Kimapenzi Kazini

PICHA: Shalinii Choudhary Sehemu kubwa ya maisha yako kama mfanyakazi unaitumia kwenye eneo la kazi. Ingawa inategemea na aina ya kazi unayoifanya, ni wazi muda mrefu kwa siku unaoutumia kutekeleza majukumu yako unakuweka karibu zaidi na wafanyakazi wenzako kuliko hata familia na marafiki. Mazingira haya ya ukaribu wa kikazi, wakati mwingine, yanatengeneza uwezekano wa uhusiano wa kimapenzi baina ya wafanyakazi.