Ukiigiza Ukatili, Unakaribisha Tabia ya Ukatili
Kuna wakati unaweza kufikiri unaigiza msimamo na kejeli kwa maumivu ya mtu, unakuwa na maoni yasiyo na haya kwa mateso ya wenzako ukijua unawafurahisha watu fulani lakini hayo maigizo ya kukosa huruma kwa mwenzako yana uwezekano wa kugeuka tabia kweli na ukawa mtu katili kweli kweli. Michezo, dini na siasa visikuchochee kujiona una haki ya kubeza masaibu wanayopitia wenzako kwa sababu mdogo mdogo mizaha hugeuka ukweli.
Mwaka 1971, Philip Zimbardo, mshunuzi na mwalimu wa Chuo Kikuu cha Stanford, alifanya utafiti maarufu kama #StanfordPrisonExperiment akilenga kuchunguza nguvu ya mazingira kwenye tabia.
Utafiti ulivyofanyika
Zimbardo alitengeneza gereza la kuigiza hapo chuoni likiwa na seli, mahali mfungwa angekaa mwenyewe, mahali pa wanyarapa kuishi, mahali wafungwa wangetoka na kuteswa na wanyapara. Washiriki walifanyiwa mchujo wa haiba kuona kama ni watu wenye utimamu wa tabia na hisia.
Kwa njia ya nasibu (random assignment) wanafunzi 24 wa kiume walitawanywa kwenye majukumu wengine kuwa wafungwa (waliovalishwa jezi bangabanga na vibandiko vya namba) na wengine wakawa wanyapara wa gereza (walivaa sare, wakapewa marungu na miwani nyeusi kuashiria mamlaka).
Sharti kubwa kwa washiriki lilikuwa kuigiza tabia zinazoendana na jukumu walilopewa. Utafiti ulilengwa kukamilika baada ya wiki mbili lakini ulikatishwa baada ya siku sita kufuatia athari kubwa kihisia zilizojitokeza.
Matokeo
Igizo likageuka kuwa uhalisia wa gereza la Stanford. Wanyapara ghafla waligeuka madikteta kweli, wasio na soni wala hawa, wasiojali hisia za wafungwa, wakiwanyanyasa kwa amri na mateso makubwa. Wafungwa nao ghafla maigizo yakageuka ukweli, wakaonesha dalili zote za sonona, ile tabia ya ‘fanya-lolote-na-sijali’ (helplessness) na wengine waligeuka kuwa waasi dhidi ya wanyapara. Baadhi ya wafungwa walipitia ukatili mkubwa wa kihisia.
Tafsiri
Philip Zimbardo alihitimisha kuwa mazingira na hali tunazolazimika kupitia kama sehemu ya majukumu yetu, yana nguvu kubwa ya ‘kuunda’ tabia mpya zinazoweza kuzidi hata nguvu ya nasaba katika tabia.
Mazingira ya gereza yaliyowapa wanyapara uwezo wa kuonesha wana nguvu dhidi ya wenzao, kwamba wanaweza kufanya chochote na hakuna kitu wale wafungwa wangefanya, yaliwageuza watu hawa waliokuwa wema mwanzoni kuwa wakatili kweli, wenye tabia zisizo na utu wala ubinadamu. Kadhalika, mazingira hayo hayo ya gereza yaliyowaweka wafungwa kwenye upande wa ‘wanyonge’ yaliwafanya wajifunze kukubali kutii, kupitia madhila ya sonona, na hata kuchochea uasi, kwa maana ya kutaka kushindana na wanyapara wa gereza.
Ukatili katika jamii ni matokeo ya mashindano ya tabaka linalotaka kulinda mamlaka yake na tabaka linalolazimishwa kutambua mamlaka hayo. Unapokuwa na pande mbili zenye nguvu na maslahi tofauti, kwa mfano, unachochea tabia za kikatili kwa namna mbili. Kwanza, upande unaotaka kuonesha uwezo wake wa kuamuru, mabavu na nguvu za kuamua mustakabali wa wengine unajifunza tabia mpya ya ukatili dhidi ya wenzao.
Upande wa pili usiokuwa na nguvu (wafungwa) unaokumbushwa umuhimu wa kutii, kufuata na kuheshimu nao unajifunza tabia za kupingana na mamlaka kama namna ya kujitetea, na hilo linaposhindikana upande huu huishia kujifunza unyonge na kujiaminisha kuwa hawana lolote wanaloweza kufanya kujitetea na nguvu za upande wa pili. Kwa msingi huo, chanzo cha tabia za hovyo katika jamii ni watu fulani kutaka kuthibitisha mamlaka yao dhidi ya wengine —power and control. Ukiwa na power (au karibu na wenye power) uwezekano wa kutaka kuumiza wengine kuonesha nguvu yako unakuwa mkubwa.
Tunachojifunza
Tuna lolote la kujifunza kwenye utafiti huu?
1. Mazingira yanayokuza tofauti za kimamlaka baina ya watu, yanaongeza uwezekano wa watu kujifunza tabia hatari kupitia majukumu yanayolenga kuthibitisha tofauti hizo za kimamlaka. Kujijengea matabaka —wenye nguvu na wanyonge—kunahamasisha tabia za kikatili.
2. Mamlaka yasiyodhibitiwa yana hatari ya kutumika vibaya. Kuna umuhimu wa kuwa na mifumo madhubuti inayowabana wenye mamlaka kwa kuwakumbusha umuhimu wa kutumia nafasi zao kuwalinda wanyonge na tishio lolote dhidi ya utu na ubinadamu wao.
3. Ukishaanza kujiona una nguvu dhidi ya mwenzako, una uhalali wa kubeza maumivu yake kwa sababu zozote zile, wewe tayari umeshakuwa mwovu. Uovu unaanza na kujiona una haki ya kumuonea mwingine —ikiwa ni pamoja na kubeza maumivu yake.
4. Upo uwezekano wa kuiga tabia za kikatili kwa watu unaojitambulisha nao. Katika mazingira haya, tabia mbaya za kuumiza watu huanza kama mchezo wa kuigiza kulinda maslahi ya kundi fulani. Kamwe usibeze maumivu ya mtu kwa kujifariji kuwa unachofanya ni mzaha wa siasa, michezo au dini.
Baada ya kuwa na uhusiano naye kwa miaka saba, aliachana nami. Nilijaribu kila niwezalo kumrudisha lakini yote yalikuwa bure. Nilitamani arudi vibaya sana kutokana na mapenzi niliyonayo kwake na nilimsihi kwa moyo wangu wote, nilimpa ahadi lakini alikataa. Niliwasiliana na mganga aitwaye DR Dawn, ambaye angeweza kunisaidia kuniroga ili kumrejesha lakini mimi ni mtu ambaye sikuwahi kuamini uchawi, sikuwa na jinsi zaidi ya kujaribu. Nilimtumia barua pepe mganga huyo na akaniambia kwamba hakuna tatizo lolote, kwamba kila kitu kitakuwa sawa baada ya siku mbili na kwamba mpenzi wangu wa zamani angerudi kwangu baada ya siku tatu. Alipiga uchawi na cha kushangaza, siku ya pili, ilikuwa karibu 4:00 PM. Mpenzi wangu wa zamani alinipigia simu, tukasuluhisha tofauti zetu na sasa tuna furaha pamoja. Yeyote anayeweza kuhitaji usaidizi wa mtangazaji huyo anaweza kumtumia barua pepe kwa ( dawnacuna314@gmail.com ) au /WhatsApp kwa: +2349046229159
JibuFutaKwa uchawi wa kuungana tena.
Kwa ujanja wa ujauzito.
Kushinda bahati nasibu.
Kushinda kesi mahakamani.
Mimea ya kutibu, kila aina ya magonjwa kama,
VVU UKIMWI Kansa malengelenge na zaidi.