Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mafumbo

Changamoto za kuwanyima watoto kufurahia utoto wao

Picha
  Tunaishi kwenye dunia inayopitia mabadiliko mengi. Mabadiliko haya ya kijamii na kiuchumi, kwa kiasi kikubwa, yamezidisha matarajio tuliyonayo kwa maisha. Ukiacha matarajio mengi tuliyonayo kwetu binafsi, kuna matarajio mengi hata kwa wenzi wetu. Mke, kwa mfano, anatarajia mume awe kila kitu anachokifahamu kuhusu mwanamume. Mume ana kazi ya kuwa mcha Mungu, mtu wa sala, mtafutaji na mchapa kazi hodari, mcheshi, rafiki msikivu, kiongozi bora,     baba mzuri na mume mzuri asiyechelewa kurudi nyumbani. Matarajio haya makubwa yana faida zake lakini pia yana upande wa pili unaochanga migogoro mingi katika familia.   PICHA:  Wikimedia Commons   Hatuishii kuwa na matarajio makubwa kwa wenza wetu. Tunazidisha pia matarajio kwa watoto wetu kiasi cha kuwanyima fursa ya kufurahia utoto wao. Hebu fikiria mtoto asiyeruhusiwa kufanya makosa. Kila analojaribu kufanya, anapodadisi mazingira yake,  anakuwa anatafsirika kama mtoto asiye na nidhamu na adabu kwa wa...

Kwa nini wewe tena Oktoba hii?

Picha
Unatusumbua! Kadiri siku zinavyosonga wajikomba sa-na Salaamu mpaka unaboa! Eti ‘mmeamkaje wapenzi wangu niwapendao…’ Fataki mkubwa wewe! Ulikuwa wapi siku zote? Kisa cha kumsalimia mtu barabarani? Umejua maana yetu eh? Hivi hukutujua siku za nyuma? Unadhani tumesahau… Sikia, Tunakumbuka nyodo zako mara chache ulizokuja Tunakumbuka kauli zako za maudhi Eti sie wako tu iwe isiwe Tukupe tusikupe haikusumbui Ukasema hata ukiwa kule sie wa hapa ni wako Sasa babu sikiliza Mwaka huu ni wa hapa hapa Wote ‘twajua huna uumini wowote Unatafutaga nini kipindi hiki? Ni hivi hivi tu waja majisidi? Wenzio ‘twaswali weye unadipu Kisa? Eti ule mpango wa mlo huko nje Unachekesha… Yaani mie mwenye njaa nikulishe wewe unayebeua! Yaani unitumie fasta, kama kondomu sina maana tena? Umesahau ulivyotufanyia siku zile? Tumekupa ukala ukaondoka? Shukrani yako sitasahau: vumbi la fo wili mjini Kama hunijui vile… Nashangaa umenirudia...

Ni wakati wa kukiasi kivuli cha ukweli…

Hutokea mtu akaishi maisha fulani duni sana lakini asijue kabisa kuwa yu duni. Wengine wetu tutakumbuka, angalau wakati ule tukiishi katika umasikini mkubwa wa familia zetu lakini hatukulifahamu hilo. Tuliishi maisha ambayo tunaamini kabisa kuwa hayo ndiyo yalikuwa yenyewe pasi hofu na mashaka. Maisha yalisonga mbele hata kama tulivaa fulana ndefu iliyosaidia kuondoa ulazima wa kuvaa kaputula. Tulipangana kitandani kila mmoja kwa welekeo wake, na bado hatukuuhisi umasikini. Umasikini wetu tulikuja kuujua baadae sana tukiisha kuwa tushahama maisha hayo kwa namna hii au ile. Tukaangalia nyuma na kujisikitikia kwamba “kweli” tulikuwa masikini. Kwa mfano huo, ukweli tulioishi nao ulikuja batilishwa na kugeuka ukweli mwingine tofauti na ule wa mwanzo. Namaanisha, kipindi kile cha umasikini usioonekana, ukweli haukuwa huu tulionao leo kwamba tulikuwa masikini siku zile. Bila shaka unanipata kwa kadiri ninavyotaka unipate, sivyo? Tafakari watu walioishi katika pango lenye giza nene mais...

Shuzi la mwenye nyumba halinuki?

Kwa wale wenye uzoefu huu, tusaidiane kufikiri. Baba akichafua hewa (ashakumu si matusi akijamba) mbele ya wageni na wanae, nani hasa huwajibikia tendo hilo? Yeye, ama wanae? Manake mara nyingi hukosi kusikia mzee akijiwahi: ' Nyie watoto, sipendi kabisa hiyo tabia yenu...nendeni mkacheze nje.' Watoto pamoja na kuujua ukweli kwamba mtumiwa halisi ni baba yao, ambaye anawasingizia wao, huenda nje wakilalamika '...baba sio mimi...mi'shijajamba labda Mangi...!' Je, kuna ulazima wowote wa baba kukiri kuuwajibikia uchafuzi wake huo wa hewa badala ya kuwabebeshea wanawe?

Nimeikumbuka hii hapa...

Picha
Nimekuwa nikiamini kuwa tofauti ya mawazo ndiyo msingi wa majadiliano. Tofauti hizi ni pamoja na mitazamo na uelewa, namna tunavyo'react' tukiguswa kwenye maeneo tunadhani hayajadiliki, namna tunavyoheshimu mawazo ya wasemaji wengine wanaoamini tofauti na sisi, namna tunavyoweza kuvumiliana na bado tukajadiliana (hata kama inakuwa kama vurugu fulani vile) lakini mwishowe mnajifunza: Hakuna anayejua. Wote mnahitaji kujifunza kwa wengine. Nimefurahi kusoma maoni ya mchangiaji aliyeamua kujificha kwenye kichaka cha jina la 'Natiakasi.' Ni bahati mbaya kwamba alidhani mimi nina chuki na dini yake anayoitetea kwa nguvu zote. Nimeona pengine itafaa nikimwonyesha chuki yangu hasa ni ipi kwa kumpeleka kwenye makala hii , niliyoiandika miaka mitatu iliyopita. Enzi hizo nilikuwa bado naandika makala ndefu ndefu (kwa sasa huwa sioni ulazima wa kurefusha ninachotaka kukisema) kwa hiyo naomba msamaha kwa makala ndefu inayochosha. Pamoja na kwamba wachangiaji wa wakati huo wen...

Methali! Methali!

Wahenga walilonga: " La kuvunda..."

Ukiingalia vizuri picha hii unaona nini?

Picha

Kutoka kwa Da'Subi, unaelewa picha hii ilivyo?

Picha
Ukiiangalia kwa makini picha hii, utaamua mwenyewe ikiwa hawa jamaa wanajenga darini ama sakafuni? HIyo ngazi iliyowekwa ina kazi gani? Huu ni mfano mzuri wa jinsi akili zetu zinavyofanya kazi. Unakifikiri kinatokana na ulichokiingiza ubongoni mwako kabla.

Ukiona watu wazima wanaumbuana hadharani...

Ukiona watu wazima wa nyumba moja Wanaodai kwao umoja ndio sera Hadharani wanaonyana na kuumbuana Nini maana yake? Ndani ku shwari?

Unaona nini kwenye picha hii?

Picha
Ukitazama picha hii kwa makini, unaweza kubaini utata fulani wa kimaamuzi. Ukiitazama kwa haraka haraka, huwezi kuuona utata huo na hivyo huwezi kukubaliana na mtazamaji mwingine atakayedai kuuona utata usiouona wewe. Sasa itazame kwa makini kadiri unavyoweza halafu ujiridhishe kwamba unachokiona ndicho kinachopaswa kuonwa. Heri ya mwezi mpya.

Saa nyingine usipende kuamini unachokiona

Umewahi kumwona kunguni anavyokimbia? Sasa ndugu msomaji huwezi amini spidi yote ya kunguni kumbe anakokwenda ni nyuma ya godoro!? Usipende kuamini unachokiona. Hoji. Tafakari. Utaona kisichoonekana katikati ya mistari.

Fumbo mfumbie mwerevu

Kwa sasa sipatikaniki vya kutosha kwa sababu ambayo nitaieleza hapa chini kwa maneno matano. Kwa wale wanaopenda chemsha bongo mnaweza kujaribu na kisha kuweka majibu kwenye kisanduku cha maoni ama kuniandikia kupitia sanduku la barua pepe: Meelekezo: Hizi ni herufi zilizofichwa (codes) ambazo ili kukupa ujumbe, inakubidi kugundua kanuni iliyotumika kuziandika ili kupata maneno matano ya kiswahili fasaha. OJUBLVXB OB OJUIBOJ KVNB MJKBMP! Chemsha ubongo kidogo ndugu msomaji.

Usawa wa viumbe mbele za Mungu uko wapi?

TURUDI kwenye ule mjadala wetu wa suala la Mungu ambalo bado ninalitafutia wakati mzuri zaidi. Kuna changamoto ndogo nadhani itastahili kutazamwa. Nayo inahusu usawa wa viumbe mbele za Mungu wao. Tunaamini kwamba Mungu alituumba sisi wanadamu pamoja na viumbe wengine mfano mimea pamoja na aina nyingine za wanyama. Na inavyoonekana, mbingu iko kwa ajili ya sisi wanadamu zaidi. Sasa hoja ni kwamba nafasi ya hawa viumbe wengine iko wapi katika ufalme wa mungu? Kwa sababu hatuelezwi wazi kuwa viumbe wengine watafaidikaje na umilele tunaoutarajia (sisi wanadamu) ambao tu viumbe kama wao. Jibu la haraka haraka ambalo mtu anaweza kulitoa kama majibu ni kwamba viumbe wengine hawana upeo/utashi wa kutambua. Lakini jibu hili nadhani haliwezi kuwa sahihi. Kwa sababu hebu tuchukulie mfano ng'ombe anapopelekwa machinjioni. Anapofikishwa pale, kiumbe huyu huonekana kupatwa na mfadhaiko mkubwa kiasi cha kuweza hata kubomoa uzio ushahidi kwamba anajua kinachoendelea. Kwamba kuna kundi la viumb...

Laiti ningeweza kuisemea nafsi vizuri!

Natamani sana kuandika kila siku. Natamani ningekuwa na shughuli moja tu ya kusema yaujazayo moyo. Kusema na kusema. (Hakuna kitu nafurahia kama kuyatoa yaliyopo moyoni). Huwezi kuyatoa kama hayapo huko yanakodhaniwa kutokea. Huwezi kusema kama huna cha kusema. Huwezi kuandika kama huna cha kuandika. Mimi nina agenda moja kubwa: Kujielewa. Natafuta namna nzuri ya kuiweka agenda hii mahala pale. Kuisema mpaka isemeke. Lakini tatizo kubwa ninalokabiliana nalo ni mwingiliano wa majukumu. Majukumu mengine hayasubiri kama ambavyo wengi wetu tunajua. Majukumu ya kitumwa tumwa hivi, kwamba tuwasikilize wenzetu watujaze yale yanayoitwa maarifa yapatikanayo katika taasisi ziitwazo 'shule'. Nadhani hatujafika mahala tukakubaliana kwamba majukumu haya yanaweza kusubiri. Hivyo ninawajibika kwayo, walau kwa sasa. Pamoja na ukosefu wa muda (hivi kweli ni ukosefu ama udhaifu wa mpangilio wa muda?) wa kubwabwaja hapa, huwa nafidia kwa kujibwabwajia mwenyewe. Nadhani kujisemea kuna nguvu...

Fujo huanzishwa na 'wenyenguvu' si wanyonge

Hakuna mahali katika historia (labda niambiwe vingine) panapoonesha kuwa matumizi ya nguvu - mapigano na vita, huanzishwa na wanyonge. Ni hivyo kwa sababu wao wenyewe (wanyonge) ni matokeo ya ' maguvu' ya wenye nguvu. Ni hivyo kwa sababu pasingelikuwapo watu wanaoitwa wanyonge, bila hao wanaojiona wana nguvu kuzidi binadamu wenzao, wenye haki kama wao. Hivyo, mapigano huanzishwa na mabwana wakubwa wao wenyewe, kwa kiburi chao cha kugoma kuwatambua na kuwasikiliza wenzao kama binadamu pia. Mapigano huwa hayaanzishwi na wale wanaoonewa, wanaonyonywa na wasiotambuliwa na kuheshimiwa. Wasiopendwa huwa hawasababishi chuki, bali wale wasiopenda wenzao ambao hujipenda wao wenyewe. Si wasiojiweza - waathirika wakuu wa ugaidi - huweza hata kufikiri kuanzisha ugaidi, bali wenye maguvu ambao hutumia maguvu hayo kupunja haki za wenzao kwa kuwahesababu kama watu wawezao kuondoshewa uhai wao wakati wowote ule. Si waliodharauliwa huweza kuanzisha visasi, bali wale wenye dharau wenyewe. ...