Ukiona watu wazima wanaumbuana hadharani...

Ukiona watu wazima wa nyumba moja
Wanaodai kwao umoja ndio sera
Hadharani wanaonyana na kuumbuana
Nini maana yake?
Ndani ku shwari?

Maoni

  1. Panapofuka moshi, ikiwa mtu hafahamu wala hajafika mahala hapo basi majibu yanaweza kuwa mawili.
    Mosi: Moto unakolea ndani
    Pili: Ndani kumeshateketea ni moshi wa masalia tu.
    Kila siku ninajisemea, 'siasa si hasa bali visa na mikasa' na siasa zimo kila kona hata usikotaka kuzikuta, wanakuletea.

    JibuFuta
  2. Mtu anakuibia redio na bahati nzuri unatonywa na watoto wako. Basi unaanza kujidai kumfuatilia mwaka mzima. Kelele kila mtaa, e bwana mbona unajizungusha? Unawajibu eti bado unacheki namna kumshughulikia. Kabla hata hujamshughulikia, leo mtaa mzima wanasikie eti mwenzetu umeamua kununua redio ile ile aliyokuibia jamaa. Tukisema nyie mabwana mnajuana na mnatuchezea akili zetu, na kwamba wewe unajidai kuibiwa ni bwege, ni makosa?

    JibuFuta
  3. Bwaya, huyo jamaa si bwege hata kidogo, akili zake timamu tamanu haswa! Wana hila hao na lao lengo ni moja. Kwanza watuache na gumzo mtaani kisha tujengeane hisia mbaya, tuzungukane kwa maneno maneno mwishowe tutumbuane usaha na tuanze kukung'utana, halafu ndiyo wao waje wajidai wema wanataka kutupatanisha nasi tukubali, basi ndo tunakuwa mabwege tena sisi, wao watupatanishe kwa ugomvi waliouunda wao?
    Bwaya nakwambia, 'siasa si hasa bali visa na mikasa tu' na sasa siasa hadi watoto wagodo wameziiga kwenye michezo yao ya gololi na ukutiukuti. Tena wacha niimbe, ukutii ukutii, wa mnaazi wa mnaaazi...!

    JibuFuta
  4. Mtaa mzima mkiwa wa kuzungukwa zungukwa, halafu mnajikuta mnajichanganya wenyewe kwa wenyewe, msielewe kinachofanywa na wenye nyumba ni mchezo wa kuigiza , mtafaa kwa kipi zaidi ya kucharazwa? Ndio tumwite Albert Mnali mcharazwe! Mtashindwaje kuigundua tamthlia?

    JibuFuta
  5. Tamthiliya wameigundua, shida ipo katika kuzungukwa bila kujua mtego upo wapi na pengine hata mtego haupo ni vile tu tumejawa na woga mithili ya majani yale ya 'vifa uongo'. Hadi hapo tutakapo-Mnali-wa, ikiwa itasaidia, pengine tutazipata nguvu zetu, kwa sasa kila mtu na aseme tu, tutasikilizana baadaye wakati midomo yakusemea itapochoka na mikono ikataka kusema.
    ...kwanza tupambe na kisha tusherehekee!

    JibuFuta
  6. Subi mnazungumzia nini mbona siwaelewi? Najaribu kupata picha iz thiz a politic or something?

    JibuFuta
  7. Jose, hapa Bwaya ameleta fumbo ama katumia sanaa ya kufikisha ujumbe ndani ya pazia, ni changamoto kwa kila mmoja kujadili kadiri ya anavyoona yeye kaelewa kauli hii. Mimi ninaandika na kutoa mchango kwa kadiri ya hali halisi inayoendelea katika nchi yetu, Bwaya naye anazungumza kadiri ya kusudi la fumbo lake, nadhani itakuwa nzuri ikiwa kila mmoja atathubutu kutoa tafsiri yake halafu kama ilivyo ada, Bwaya atatupa hitimisho (akipenda).

    JibuFuta
  8. Bwaya sasa hivi tunasikia eti mwizi wa redio mwenyewe alishafikisha kesi mahakamani. Ajabu! Yaani pamoja na yote hayo bado mwenyewe nyumba anathubutu kuinunua redio hiyo hiyo. Kisa? Lazima akaitumie kwenye arusi ya jumamosi?

    Tunachojiuliza ni kwamba siku zote hizo hawakujua arusi ni jumamosi? Na hata kama walijisahau, well, kunasababu gani kung'ang'ania redio ya jambazi?

    Itafika mahala watoto wataamua liwalo na liwe. Siku mkisikia wamebeba mapanga msishangae. Kudanganyana kitoto hivi mchana kweupe jamani?

    Zama za kuila familia zimepita!

    JibuFuta
  9. Lakini hata kaka mdogo wa kambo anaona ni heri baba ainunue redio.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?