Katika zama hizi za maendeleo ya kidijitali, ni rahisi sana kufahamiana na watu wengi ambao, hata hivyo, wanaweza wasiwe marafiki. Unaweza, kwa mfano, kuwa na ‘marafiki’ elfu tano kwenye mitandao ya kijamii, lakini usiwe na rafiki hata mmoja katika maisha halisi. Marafiki wa kweli na wa karibu ni moja wapo ya mahitaji muhimu katika maisha. Tunaweza kuwa na sababu nyingi kuhalalisha kwa nini hatuna (haja na) marafiki wa karibu. Hata hivyo, zipo nyakati hufika tukajikuta katika maisha yenye kujaa upweke na msongo wa mawazo kwa sababu hatukutumia muda wetu kutengeneza urafiki wa karibu na watu tunaofahamiana nao.
DUH! UMEBADILISHA KICHWA CHA HABARI?
JibuFutaAU.......
La kuvunda halina ubani!
JibuFutaUtalipatia ubani gani la kuvunda? Llikishavunda harufu yake ndo marashi yake tena.
Koero, sijabadili. Pengine ni kwa sababu nimepost zote na hiyo ya juu kwa muda unaokaribiana!
JibuFutaSubi, labda tuliweke kwenye jokofu, waonaje?
La kuvunda halina ubani, kifo hakina kinga,
JibuFutala kuvunda! Hata ukiliweka kwenye jokofu , litavunda tu, la kuvunda, hata kama sio leo, wala kesho, hata mtondo go, iko siku litavunda tu, kuliweka jokofuni, waliongezea tu siku za kutovunda! lakini litavunda tu.
La Kuvunda halina ubani
JibuFuta