Aprili: Utasoma vitabu vingapi?

Mkesha wa kuukaribisha mwezi mpya ndio huu. Kesho tutauanza mwezi mpya kwa siku iitwayo 'ya wajinga'.

Masuala ya kuangazia kidogo:

Ni kwa kiasi gani umepoteza muda mwingi pasi na sababu ya msingi?
Soga. Stori zisizojenga. Kuwakatisha tamaa watu. Mabishano. Na kadhalika. Na kadhalika.

Umesafiri kilomita ngapi mwezi huu? Hebu fikiria, kama ungeamua kuzitumia kilomita hizo kusoma, ungesoma vitabu vingapi?

Kwa mwezi Machi, umeweza kusoma vitabu vingapi?

Ni fedha kiasi gani umetumia kununua vitabu?
Utasema hela hazitoshi.

Hivi unajua ni shi'ngapi umeteketeza kwa kukwangulia vocha mwezi huu? Umekwangua vocha kusaidia kusambaza 'text messages' za mizaha!

Umeona ulivyo na fedha?

Haya. Hima na tuanze kuzitumia hizo hizo vitabuni mwezi huu! Na tusome.

Mwezi Aprili uwe ni wa kusoma.

Maoni

  1. Watu watakuambia hawanunui vitabu kwa vile ni ghali. Ukienda baa, utawaona watu hao wanakula ulabu kama vile wanapewa bure. Lakini wanasema hawana hela ya kununulia kitabu cha shilingi elfu sita. Nashukuru umelileta suala hili. Naliongelea mara kwa mara hapa.

    JibuFuta
  2. Nimesafiri kilomita hazihesabiki, na wakati nipo usafirini, husoma... nafahamu halikuwa swali lililohitaji jibu :)
    Vitabu kuvinunua au hata kuviomba maktabani ni tabia... kwa wengine Kaka Mbele anavyosema, ni mambo ya kupiga budget... haja yako ikiwa bia, au vocha, utatafuta vitabu kwa nini?

    Serina.

    JibuFuta
  3. Profesa, nakubaliana na wewe. Hata kama kusoma bado hakujawa 'ulabu' wetu, mabadiliko yanawezekana.
    Tupaze sauti kwa pamoja.

    Dada Serina,
    Nimeipenda tabia yako ya kujisomea safarini. Bila shaka tabia (nzuri) hujengwa kwa gharama. Tukubali kuingia gharama hizo kupata faida.

    JibuFuta
  4. Nashukuru baba yetu ametujengea tabia ya kupenda kusoma, tangu kuzaliwa kwangu nimekuta tabia hii kujisomea imejengeka pale nyumbani kwetu, dada zangu kaka zangu na wadogo zangu wote wamekuwa ni watu wanopenda kusoma, nyumbani baba anyo maktaba kubwa tu yeye vitabu mbalimbali vya kitaaluna na vya hadithi.
    Nimegundua kuwa kama mzazi ukiwa na tabia ya kupenda kujisomea hata watoto wanaiga na muchukulia kama ndio sehemu ya maisha.
    Kwa kawaida kama ninatumia usafiri wa daladala huwa sikosi kubeba kitabu, na nikikosa kitabu ninanunua gazeti.
    Ni mara chache sana nimewahi kupanda daladala na kukuta mtu ameshika kitabu anajisomea, nasema ni mara chache sana. hili nadhani ni tatizo tulilonalo watanzania.

    NB: Nimesikia kuwa Prof: Mbele ametunga vitabu vingi, je vinapatikana wapi? Nimepita kule maktaba ya chuo kikuu lakini sijabahatika kupata vitabu vyake, naomba msaada kwa yeyote anayefahamu vinapopatikana vitabu vya msomi huyu hazina ya taifa letu.....

    JibuFuta
  5. Koero,
    Vitabu vya Profesa Mbele vinapatikana kwenye maduka pepe, unaweza kuagiza mwenyewe ama kutumia ndugu, jamaa au rafiki ama wasiliana na mwenyewe Profesa Mbele atakufahamisha unavyoweza kuvipata. Prof. alieleza jinsi ya kupata vitabu vyake kwenye posti yake hii (bofya hapa)

    JibuFuta
  6. kusoma huonekana kama vile ni tabia ya watu wachache. najsfia kwa kusoma vitabu na nina wadogo zangu fulani wao na kitabu usiwaambie kitu. kiasi kwamba nikinunua kitabu kama sijamaliza kukisoma nalizimika kukificha ili wasikiibe kabla sijakimaliza kwani ni utaratibu wangu kutokugawa kitabu ambacho sijamaliza kukisoma.

    kama anavyosema koero, raha ya kusafiria daladala ni kuwa na kitabu pembeni. yaani foleni za dar hazikuzingui wala nini wewe unakuwa bize na kitabu chako. wabongo wengi na hasa vijana jawana mpango wa kusoma vitabu. kuna baadi ya vitabu vya thamani ninavyovipata kwa shida, na hivyo nikiwa napita kwenye maeneno yangu ya kujidai, huwa nalizimika kuvificha kwani vikiibwa sitopata vingine kiurahisi lakini kumbe ni wasiwasi wangu tu. weka kitabu chochote cha thamani, wanakianaglia kama vile hawakioni. ukimueleza mtu uzuri wa kitabu, basi atakiangalia juu, nyuma na kukifungua flululululu, na kukiweka pembeni.

    nijigambe kidogo kwamba nina vitabu kadhaa vya utambuzi na kujitambua na vile vyenye lengo la kukukuza kiroho lakini sio vya kikristo wala kiislamu, ni vya kukua kiroho na hivyo, kwa mtu yeyote anayehitaji, naviazimisha bure kabisa. pia ninazo DVDs za kukukuza kiroo, hizo na kubania na kukupatia kwa gharama zangu, bure kabisa.

    vitabu vinavyoshindikana kupatikana, basi wadogo zangu wanavi-heck na kuviprint kutoka mtandaoni.

    karibuni na wewe nipe vyako.

    JibuFuta
  7. Nuru Shabani1/4/09 10:10 AM

    Ni kweli watu wengi hawapendi kujisomea.Mi binafsi hupendelea sana kujisomea kama hautanikuta na kitabu basi walau gazeti.Utakuta mtu amesimama kwenye foleni amenununa kwa sababu ya foleni lkn kama ukiwa na kitabu cha kujisomea hautaona kama kuna foleni utaingoja foleni huku kuna kitu unafanya.

    JibuFuta
  8. Wanablogu walioandika vitabu kama Profesa Mbele watuhabarishe! Tuanzie bloguni. Halafu tukawatangazie walio nje.

    Kuandika bila kusoma ni sawa na kupenda kula wakati hupiki.

    Kamala,

    Inachekesha ila inasikitisha. Kuonesha uzito wa tatizo la kutokujisomea, hata uache kitabu wapi utakikuta ulipokiacha. Sio kwamba watu ni waaminifu sana, no. Sahau simu uone!

    Umenikumbusha siku moja nikiwa Mbeya. Nilisahau kitabu nilichokuwa nakisoma kwenye internet cafe fulani pale mjini. Niliporudi kesho yake nilikikuta pale pale (pamoja na kwamba wateja walikuwa wakipita hapo). Nilifurahi kwani kilikuwa kimegharimu boom, lakini wakati huo huo nikishangaa inakuwaje.

    Vingi vinaibwa, lakini si vitabu. True confension: Nikiwa adolescent miaka hiyo nimeiba sana vitabu vya maktaba mbalimbali nlikowahi kupita. Huwa nikikumbuka hujionea haya, lakini pia 'wizi' huo ulinisaidia sana kusoma.

    JibuFuta
  9. Duh!! Kaka Bwaya mimi niliwahi kusimamishwa mstarini shuleni na kutangazwa kuwa ni mwizi mzuri.
    Kwanini?
    Subiri nisimulie.

    Kuna siku niliiba kitabu ambacho kilikuwa ni kitabu pekee walichokuwa wakitumia waalimu kuchotea matirio ya kutufundishia, sasa mwalimu akkisahau na kukiacha darasani, nilipokiona nikakiiba na kutaam,baa nacho nyumbani.
    Yule mwalimu alikuwa ni kishoka yaani msahaulifu hivyo hakukumbuka kama alikiacha wapi, ukawa ni mtihani kwake kukitafuta.
    basi siku moja akaingia darasani, wakati anafundisha nikatangulia kujibu swali fulani ambao lilikuwa Kompliketedi, aknistukia kuwa labda ninacho hicho kitabu kwani nilijibu kwa kukarir, baadae aliniita ofisini, alinibana kwa ahadi chungu mzima nikakiri kuwa nilikichukua, sikuadhibiwa lakini nilifedheheka......

    JibuFuta
  10. Nuru Shabani1/4/09 2:23 PM

    Bwaya bwana!
    Umenikumbusha mali sana,ukweli nilikuwa ninaiba sana vitabu kwenye maktaba za serikali ili tu kujisomea.
    Kamala soma na vitabu vingine sio tu vya utambuzi li uwe na wigo mpana wa ufahamu.

    JibuFuta
  11. Hei, kumbe 'wezi' tuko wengi?!

    JibuFuta
  12. Bwaya Mimi sikuiba bali nilisogeza!!!

    JibuFuta
  13. Ni kweli muda umefika wa kuanza kusoma vitabu. Tatizo ni kwamba sisi watanzania tunachelewa sana kuwaanzisha watoto wetu kuanza kusoma vitabu. Kwa uzoefu wangu nimeona hata nilipokuwa mdogo wengi wa lika yangu walikuwa hawajui kusoma tena wala kuandika. Na sasa huku niishiko nimeona watoto wanaoenda chekechea wanapomaliza ule mwaka wa mwisho wanaweza kusoma. Na ndio inakuwa rahisi kusoma. Lakini pia inategemea TZ kila mtu ametoka katika familia inayopenda kusoma au vipi. Ngoja niwape mfano nina binti anasoma darasa la nne yeye kwa mwezi anasoma vitabu kumi. Nina bahati sana sihitaji kumlazimisha kusoma. Ninachotaka kusema kupenda kusoma ni msingi tangu utotoni (chekechea) pia kuwasomea watoto hadithi nk.

    JibuFuta
  14. Lo, huu mjadala unasisimua sana. Sijawahi kuwa na gari Tanzania na ninapokuwa Dar hutumia dala dala. Ninapenda kuwa na kitabu, nisome ninapokuwa kituoni. Lakini nimeona kuwa kwa kufanya hivyo, watu wananiangalia kwa mshangao au wasi wasi.

    Nikishachoka na jua la Dar, hupenda kuingia baa, kupata bia ya baridi, huku nikisoma kitabu changu. Humo pia watu wananiangalia kwa mshangao au wasi wasi wasi.

    Ni faraja kubwa kufuatilia mjadala huu. Ninaamini kuwa tukiendelea kuhamasishana na kutoa mfano kwa wengine, kidogo kidogo tutaweza kuwashawishi wengine wafuate tunavyofanya, na hasa nawafikiria watoto. Tunaweza kuwa mfano kwa watoto, tukachangia kujenga Taifa imara la kesho, lenye kuthamini usomaji wa vitabu.

    Kuhusu vitabu vyangu, ni kwamba nimeviandika kwa kiIngereza, ila ninapangia kuvitafsiri kwa kiSwahili. Kuongezea taarifa walizotoa wachangiaji hapo juu, kuhusu upatikanaji wa vitabu hivi, vinapatikana pia Dar, simu namba 0754 888 647 na 0717 413 073.

    Nimepata wazo leo la kutoa nakala kwa wanablogu mnaoshiriki mjadala huu. Naamini kuwa kufanya hivyo kunaweza kutoa changamoto ya mjadala mbele ya safari. Nitafurahi kupata maoni yenu.

    JibuFuta
  15. nuru niumesoma vitabu vingi na sasa bado ninavyo vya kutosha sana na ninaendelea kuvisakama lakini utambuzi umenikamata kabali. yaani ni kati ya vitabu muhimu maishani mwangu kwani baada ya kujitambua, mengine yote yanawezekana likiwemo hilo la kusoma vingenevyovyote bila choyo wala ego

    JibuFuta
  16. @Yasinta,

    Ni kweli kwamba wazazi wana mchango muhimu kuwajengea watoto utamaduni wa kusoma. Tabia ya kusoma haizuki kama ugonjwa wa kipindupindu. Inajengwa.

    Nikitoa mfano wangu mwenyewe. Nimekua nikiona baba akisoma. Labda pengine ni kwa vile ni mwalimu.

    Tulizoea kumwona akitumia muda mwingi akisoma. Si tu hesabu anazofundisha, lakini pia mambo mengine ya kawaida.

    Aliporudi safari, zawadi ya maana kwa wanae ilikuwa vitabu. Hapo hujazungumzia magazeti yenye makala ndefu, majarida nk ambayo mpaka leo huyakuta pale nyumbani.

    Kwa hiyo, tulijikuta, kama watoto, tukithamini vitabu.

    Mimi na mdogo wangu anayefanya Sayansi ya Siasa na Utawala, tulikuwa tukishindana kusoma. Mpaka leo tunabadilishana vitabu. Sababu hasa, nadhani ni wazazi. Walitulelea vitabuni.


    @Profesa Mbele,

    Asante sana kwa wazo zuri ulilokuja nalo. Ni mfano mzuri wa kuigwa na wasomi waandishi wengine wenye moyo wa dhati wa kutoa maarifa yao kwa jamii yao.

    Ni imani yangu kuwa wadau tutachangamkia ofa hii ya maarifa ambayo bila shaka itatuongezea ufahamu katika masuala mengi.

    Tuvisome, tushibe maarifa, halafu tutawanye maarifa hayo kwa wenzetu wanaotuzunguka.

    JibuFuta
  17. Kusoma vitabu kumbe ni tabia.Mimi nilikuwa na kauvivu ka kusoma vitabu lakini kupitia mjadala huu nimepata mwamko mpya wa kujikita kwenye usomaji wa vitabu.Tabia hii hakika ina manufaa makubwa kwani inaongeza wigo wa uelewa wa mambo.
    Prof Mbele nashukuru sana kwa ofa yako,natamani sana nianze na vitabu vyako ili niongeze wigo wa uelewa wa tamaduni mbalimbali na mambo mengine.

    Wachangiaji wengi hapo juu wamesema wanasoma vitabu sana tu, lakini hawajasema huwa wanasoma vitabu vinavyohusiana na nini hasa, pengine wengine wamebobea kusoma vitabu vya darasani kama vya chemistry,physics,n.k. Kamala yeye kasema yeye huwa anasoma sana vitabu vya kiutambuzi.

    JibuFuta
  18. Wow! Hii ni nzuri saana. Utaratibu wa kusoma ni mzuri, na ni tabia. Na wakarti mwingine (ama niseme wakati mwingi) ni maamuzi binafsi. Na kama alivyosema Pro Mbele na wengine hapo ni kuwa mengi ya haya ni tabia ambayo mtu huichukua na kuamua kuiwekeza katika sehemu ya maisha. Pengine mimi si msomaji mzuri, lakini najitahidi. Na tangu nianze kujisomea, nimeona na kujifunza mengi.
    Mifano mingi ni hai na nimefurahia michango ya wengi.
    Amani na Heshima kwenu

    JibuFuta
  19. Jitahidini kuwafikia wasio na mpango na mtandao. Discussions zenu zisiishie ndani ya vyumba vya internet

    JibuFuta
  20. Mie nimejaribu kujiwekea kaji-utaratibu ka kusoma angalau sura moja ya Biblia kila siku (chakula cha kiroho)....kwa "kimwili",najithaidi kutupia jicho andiko/chapisho lolote litakalokatiza mbele yangu...

    JibuFuta
  21. kissima na anonymous chanagamoto zenu ni nzuri na tofauti kidogo. sio kusoma tu bali kusoma nini na sio vitabu tu, bali vitabu gani. katika kujitambua, tunajiambua ili tuishi, tusiishi tu, bali tuishi kama nani/nini.

    evarist, uinaamini biblia itakukuza kiroho kweli? mbona wenye nayo wanamigongano isiyokuza kiroho? ile si ni documentary ya Israel?

    sijui

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?