Tuko ndani ya uwanja wa ndege wa Sao Paulo, Brazil. Ni usiku, tunangoja usafiri wa kwenda Dubai, kama lisaa limoja lijalo. Nimekamata kitabu changu nasoma. Ni kitabu cha rafiki yangu kanigawia nionje yaliyomo. Yeye naye kakaa zake kimya anasoma kitabu changu pia. Saa nyingine tunafunika vitabu, tunazungumza mawili matatu, tunaendelea kupekua pekua. Ni katika kuongoja tu usafiri. Faizul, Deo, Bijoy, na mimi jijini Sao Paulo. Picha: Dr Awab Mara wanatufuata watu wawili waliovaa kiraia. Mmoja kajazia, kajichora tatuu mkononi, kavaa viatu vinavyompyaya. Mtu wa mazoezi. Mwingine mdogo dogo tu, ila shida yake hasemi kiingereza. Kwa hiyo ni "mpole fulani hivi". Baunsa anatuonesha kitambulisho chake. Ni askari wa Kibrazil. "Ninaomba kuona hati yako ya kusafiria tafadhali?"askari bonge ananiambia, mwenzie akimsaidia kwa macho. Nilisita kidogo, nikijiuliza inakuwaje aje kwangu wakati nilikuwa na wasafiri wengine. Ndicho nilichomwuliza. Baada ya kudai kuwa anafanya ...