Nimebahatika kutembelea Chuo Kikuu cha Taifa Maynooth, Dublin Ireland. Ni chuo cha zamani sana tangu enzi hizo kikiwaandaa makasisi, kikiitwa St Patrick College.
|
Maynooth University, Ireland. Picha: Jielewe |
Jambo la ajabu, nimeona picha zinazoeleza idadi ya wanafunzi waliokuwa wanajiunga kuchukua masomo hayo ya Upadre kila mwaka. Idadi inaonekana kupungua kila mwaka, mpaka walipoamua kukigeuza kuwa Chuo Kikuu kifundishe mambo mengine.
|
Madhari ya Maynooth, Dublin. Picha: Jielewe |
Kwa ujumla, msisimko wa dini haupo nchini humu. Makanisa mengi ya Kikatoliki yamefungwa au kugeuzwa matumizi kusaidia shughuli nyingine.
|
Kanisa maarufu nikiwa jengo la makumbusho. Picha: Jielewe |
'Nikiwa hapa, ndiyo kwanza kashfa za makasisi kudhalilisha watoto zinapamba moto. Mambo yamebadilika.
|
Sanamu ya Papa John Paul II alipotembelea hapa. Picha: Jielewe |
Dublin, mji mkuu wa Ireland ndiko yaliko makazi ya makampuni makubwa ya teknolojia. Ndiko waliko Yahoo! Na makampuni mengine ya mtandoni.
|
Dublin imebaki na sanamu za kidini. Waumi haba. Picha: Jielewe |
Hiyo ndio Ireland. Nchi iliyokuwa koloni la Uingereza kwa miaka mingi. Sasa ikijipiga piga kwenda mbele.
Maoni
Chapisha Maoni