Guiness: Alama ya Taifa la Ireland

Kiwanda kinacholinda heshima ya walevi, Dublin, Ireland. Picha: Jielewe

Katika bidhaa wanayojivunia wa-Irish, ni pombe maarufu ya Guiness. Ukikatiza mitaa saa za usiku baada ya kazi, wanywaji (najua ni kosa kubwa kuwaita walevi) hawanywi pombe nyinine zaidi ya Guiness. Kila baa ni Guiness.

Nawambia mwenyeji wangu sinywi pombe, wananishangaa. 'Utarudije kwenu hujanywa Guiness?'
Alama ya Guiness ni nembo ya Taifa. Pombe ni urithi wa taifa. Picha: Jielewe

Kitu kingine ambacho nimekigundua, kumbe ile nembo ya Guiness unayoiona, ndiyo nembo ya Taifa. Kwa maana nyingine, wakati sisi urithi wetu ni Ngorongoro na mbuga za wanyama, hawa jamaa, urithi wao ni pombe. Pombe ni urithi wa taifa. Natania.


Mtaani kweli imepangwa. Hongereni.



Nimekumbuka kwetu. Sisi ni wazalishaji wakubwa wa bangi na mirungi tena kwa wingi sana ingawa kwa siri. Wa-Irish ni wazalishaji wakubwa wa Pombe. Sote letu moja. Unalijua?

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?