Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Visa

Unayafahamu Anayopitia Mwanao na Hakuambii?

Picha
Kama sehemu ya wajibu wangu wa kitaaluma, huwa ninaandaa, kuendesha na kutathmini mafunzo ya ulinzi wa mtoto kwa walimu, wanafunzi na wazazi kwenye shule mbalimbali nchini. Nimeendesha mafunzo hayo kwa shule nyingi hususani za binafsi na zile zinazoendeshwa na mashirika binafsi na kidini.     Hivi karibuni nilipata bahati hiyo kwenye shule moja kubwa inayoendeshwa na shirika moja la kitawa. Imani tuliyonayo wazazi wengi kwa shule hizi ni mfumo madhubuti wa malezi unaowahakikishia watoto usalama wao. Ingawa ni kweli matarajio ya wazazi wengi ni ufaulu mzuri, hili la malezi yenye kumjenga mtoto kimaadili ni kubwa zaidi.   Siku hiyo, Ijumaa, kabla ya kuzungumza na wazazi Jumamosi yake, nilipata wasaa wa kusema na watoto wa kidato cha kwanza na cha pili. Madhumuni ya kuanza na watoto ni kupata uzoefu halisi ninaoweza kuutumia kama rejea kwenye mazungumzo na wazazi. Nafahamu sisi wazazi huwa hatupokei jambo kirahisi hasa linapoonekana halina uhalisia. Ninapokuwa na mifano hali...