Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Nidhamu

Kuuishi Wito Wako, Unahitaji Nidhamu ya Kujifunza

Picha
PICHA: findingmastery.net/ Nimekutana na vijana wengi wanaotaka niwaonyeshe njia ya mkato ya kufanya kazi za ndoto zao. Wanafikiri kupata kazi inayoendana na vipaji na tabia zao ni jambo la siku moja. Ingawa huwa ninawasaidia kujiuliza maswali ya msingi yanayowachochea kugundua hazina iliyolala ndani yao, bado husisitiza umuhimu wa kuwa na mtazamo mrefu wa kuona yasiyoonekana kwa macho. Nitatumia mfano wa Robert Green, mwandishi nimpendaye aliyeandika vitabu maarufu vya ‘The 48 Laws of Power, ‘Mastery’ na ‘The Art of Seduction.’ Ingawa tangu akiwa mdogo aligundua alitaka kuwa mwandishi, Robert hakuwa na uhakika anataka kuandika masuala gani.   Baada ya kumaliza chuo, Robert alianza kufanya kazi kama mwandishi wa habari. Kazi hiyo, hata hivyo, haikumwendea vizuri. Mhariri wake alimshauri, ‘Tafuta kazi nyingine ya kufanya. Wewe si mwandishi. Hujui kupangilia mawazo yakaeleweka. Nakushauri ukatafute maisha mengine.” Robert anasema alijisikia vibaya kwa ...

Tabia Tano Zitakazokupa Nidhamu ya Muda Kazini

Picha
Mafanikio katika eneo lako la kazi, kwa kiasi kikubwa, yanategemea matumizi ya muda ulionao kwa siku. Kile unachokifanya kati ya saa 6:00 usiku na saa 5:59 usiku wa siku inayofuata, ndicho kinachoamua utekelezaji wa majukumu yako.

Umuhimu wa Kusema Hapana kwa Ngono Kabla ya Ndoa

Picha
PICHA: eskimi.com Majuzi niliwaambia wanafunzi wangu wakitaka kuwa na ndoa bora hapo baadae, lazima wajifunze kuacha ngono kabla ya ndoa. Kusikia hivyo, walicheka mithili ya watu waliosikia kichekesho kipya cha mwaka. Sikushangaa. Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi, wastani wa umri wa kijana kuanza ngono ni miaka kati ya 14 na 15. Wanafunzi wangu walikuwa na kati ya umri wa miaka 21 na 23.

Desturi Zetu Zilivyosaidia Malezi Bora ya Watoto -2

Picha
PICHA: The Community Voice NIMEJARIBU kubainisha baadhi ya desturi zilizosaidia kukuza watoto wanaojitambua. Unaweza kusoma makala ya kwanza hapa . Kwa kuanzia, tuliona namna familia zilivyowajibika kumtunza mama aliyejifungua. Mtoto na mama walipata muda wa kutosha kujenga mahusiano ya karibu.

Desturi Zetu Zilivyosaidia Malezi Bora ya Watoto

Picha
PICHA: Huffington Post WAAFRIKA tumekuwa na utaratibu mzuri wa kuwalea watoto wetu. Mila na desturi za jamii nyingi za ki-Afrika zimeyapa malezi ya watoto uzito unaostahili. Malezi yalichukuliwa kama fursa nyeti waliyonayo wanajamii kurithisha utambulisho wa kabila husika kwa kizazi kinachofuata.

Ufanye Nini Mtoto Anapokuwa Mkorofi?

Picha
PICHA: JGI/Jamie Grill Pengine una mtoto unayefikiri ameshindikana. Unamwita mtundu, mtukutu, asiyeambilika, mbishi, mkaidi na majina mengine. Kikubwa ni tabia yake ya kupenda kushindana. Katika makala haya tunamwita mtoto mkorofi. Huyu ni mtoto anayeweza kukukatalia kitu bila kupepesa macho na ukajikuta ukifedheheka.

Unavyoweza Kumfundisha Mtoto Kuwa Mkweli

Picha
PICHA: Heaths Haven Fikiria uko jikoni ukiandaa chakula cha jioni. Watoto wako wawili wadogo Fred na Joe wanacheza sebuleni. Salome yuko mezani akifanya kazi za shule. Mara unasikia mlio wa kitu kuvunjika sebuleni. Unapatwa na wasiwasi. Unakwenda haraka kujua kilichotokea. Maji yanatiririka sakafuni. Chupa ya chai imedondoka na kupasuka. Unakasirika.

Unahitaji Nidhamu ya Fedha Kujikwamua Kiuchumi

Picha
PICHA: usaa.com Juma lililopita tuliongelea uwezekano wa mfanyakazi kujikwamua kiuchumi . Kubwa ni nidhamu. Unapokuwa na nidhamu ya mshahara, unaongeza uwezekano wa kuwa na usalama wa kifedha. Swali linaweza kuwa, ‘Kinachomfanya mfanyakazi akose nidhamu ya fedha ni nini?’ ‘Inakuwaje mchuuzi mdogo wa bidhaa awe na nidhamu ya fedha kuliko Afisa wa Serikali?’

Jifunze Namna Bora ya Kumrudi Mtoto

Picha
PICHA: IT News Africa Tunapojadili mbadala wa adhabu ya bakora tunatambua changamoto kadhaa. Kwanza, ni wazi bakora zimekuwa sehemu ya malezi yetu. Kwa wazazi wengi, unapozungumzia nidhamu ya mtoto, maana yake unazungumzia bakora. Imejengeka imani kwa watu kuwa bakora ndiyo nyenzo kuu inayoweza kumrekebisha mtoto.

Unavyoweza Kutumia Mshahara Kujikwamua Kiuchumi

Picha
Wapo watu wanawakejeli wafanyakazi kwa kuajiriwa. Kwamba kama mtu asiye na elimu anaweza ‘kuosha magari mtaani’ na akakuzidi kipato kuna sababu gani kuishi maisha magumu ofisini? Upo ukweli wa namna fulani. Wafanyakazi wengi wanaishi maisha ya ukata. Kazi yao kubwa ni kupambana kuhakikisha kuwa mishahara inakutana. Katika mazingira ya namna hii, inakuwa vigumu kupiga hatua za maana kimaisha.

Nidhamu ya Mtoto Bila Viboko Inawezekana

Picha
PICHA: Pinterest Adhabu ya bakora ni utamaduni. Kwa wengi wetu bakora ni imani. Tunaziamini kiasi cha kuwa tayari kuzirithisha kwa wanetu kama ambavyo na sisi tumeziridhi kwa wazazi wetu. Kwa hiyo tunapopendekeza mbadala wa bakora kama adhabu iliyozoeleka tunaelewa hili haliwezi kuwa jambo jepesi. Kama tulivyoona, wazazi tunapowachapa watoto tunaamini lengo ni kuwasaidia wawe na nidhamu. Hata hivyo, kwa kutazama mazingira yanayoambatana na adhabu hii ni dhahiri bakora haiondoi tatizo linalokusudiwa.