Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ujifunzaji

Madhara ya Kutoa Ushauri Kienyeji na Kuugeuza Unasihi kuwa Ushauri

Picha
Utamaduni wa (kutoa na kuomba) ushauri umejengeka kwenye misingi ya hekima ya wazee walioona mengi, uzoefu wa mtu mzima unaompa uhalali wa kutoa mwongozo wa kufuata kwa anayemzidi.  Hata tunaposikia unasihi (counselling), aghalabu, mawazo yetu yanaenda kwenye taaluma ya kushauri watu na kuwaambia cha kufanya ili kutatua matatizo yanayowakabili. Wapo, tena wengi, wanaotafsiri ‘counselling’ kama ushauri. Counselling sio ushauri. Katika makala haya, ninajenga hoja kuwa kutoa ushauri ni jambo la hatari na kwamba linaweza kusababisha madhara makubwa kwa anayeshauriwa lakini pia hata anayeshauri.  Kadhalika, ninalenga kuonesha, japo kwa ufupi kuwa hata kwenye unasihi msingi wa kwanza wa kuzingatia kwa mtoa huduma (aliyefuzu) ni kuepuka kabisa kutoa ushauri kwa mtu. Nakusudia kuonesha nini hasa huwa ni malengo ya unasihi. stefanamer/Getty Images Ushauri ni nini?  Unaposema unamshauri mtu unakuwa na maana gani?  Ushauri, kwa kifupi, ni maelekezo mahususi unayompa mtu, maamuz...

Mbinu za Kumfundisha Mtoto Kusoma Akiwa Nyumbani

Picha
Katika utafiti uliofanywa na program ya Uwezo iliyochini ya Shirika la Twaweza, zaidi ya nusu ya watoto wa darasa la nne na tano katika nchi za Afrika Mashariki hawana uwezo wa kusoma na kuandika. Nilimwuuliza Bahiya Abdi, mhadhiri wa masuala ya mitalaa, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge, maana ya kutokujua kusoma na kuandika. Anasema: “Kuna mambo kadhaa ya kuangalia tunapozungumzia uwezo wa mtoto kusoma. Mbali na mtoto kutambua herufi, lazima awe na uwezo wa kusoma kwa haraka.” “Lakini pia, uwezo wa kusoma unapimwa kwa kiwango cha kuelewa kile anakisoma. Kama mtoto anaweza kusoma tu lakini hawezi kupata ujumbe vizuri, hapo tunaweza kusema uwezo wake uko chini ya kiwango.” Kwa mujibu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) mtoto wa darasa la kwanza na la pili anatarajiwa kutambua na kusoma kwa ufasaha maneno 50 yenye maana kwa dakika na maneno 40 yasiyo na maana kwa dakika. Kadhalika, anatarajiwa kuandika kwa ufasaha herufi kubwa na ndogo, na kufanya hesabu za kujumlisha na k...

Umuhimu wa Kumpunguzia Mtoto Shinikizo la Kufaulu

Picha
PICHA: Stressed Out Students Ufaulu wa mitihani umepewa nafasi ya pekee katika mfumo wetu wa elimu. Shule zetu, kwa hakika, hazina namna nyingine ya kumwelimisha mtoto zaidi ya kumtaka akusanye, akumbuke na kutumia maarifa aliyonayo kujibu maswali ya mtihani. Ingawa ustawi wa jumla wa mwanadamu hautegemei eneo hilo moja la ukusanyaji na utumiaji wa maarifa, shule zetu zinaonekana kuamini pasipo mtu kuwa na maarifa mengi hawezi kufanikiwa.

‘Homework’ Zinavyodumaza Ukuaji wa Watoto Wadogo

Picha
PICHA:  PhillyVoice Ukiwauliza wazazi kitu gani wanafikiri kikisitizwa mapema zaidi kwa watoto kitawasaidia kufanikiwa, wengi  watakwambia elimu. Kwa sababu hiyo, wazazi hasa wasomi wanaharakisha kuwapeleka shule watoto wenye umri mdogo. Ninawafahamu watoto wengi wa miaka minne wanaosoma darasa la kwanza. Wazazi wa watoto hawa wanafanya hivyo wakiamini mtoto akisoma mapema, maana yake uwezekano wa kufanikiwa maishani unakuwa mkubwa.

Mbinu za Kumshirikisha Mwanafunzi Katika Ujifunzaji

Picha
PICHA:  United Nations Majuzi niliwatembelea walimu wanafunzi waliokuwa wakiendelea na mazoezi ya ufundishaji. Mafunzo kwa vitendo yana umuhimu wa kipekee katika maandalizi ya walimu. Katika kipindi hiki, mwanafunzi anapewa fursa ya kutumia maarifa aliyojifunza darasani katika mazingira halisi ya kazi. Kwa mwalimu, kama mimi, hiki ni kipindi cha kutathmini uwezo wa mwanafunzi wa ualimu kumudu majukumu yake. Moja wapo ya vipindi vingi nilivyopata bahati ya kuhudhuria ni Baiolojia kidato cha III kilichokuwa kikifundishwa na mwanafunzi wangu wa mwaka wa II. Baada ya kufanya utangulizi wa somo lake, mwalimu huyu mwanafunzi aliwaelekeza wanafunzi wake kukaa katika makundi ya watu watano watano kusudi wafanye majadiliano. Majadiliano ni mbinu muhimu ya ufundishaji inayowawezesha wanafunzi kujifunza. Kama tulivyosema kwenye makala yaliyopita, kupitia majadiliano, mwanafunzi hupata fursa ya kusikiliza mtazamo tofauti kutoka kwa wenzake. Aidha, majadiliano ni mb...

Mbinu za Kujenga Ujuzi wa Mwanafunzi

Picha
PICHA: Shutterstock Nakumbuka siku ya kwanza kusikia neno ‘cell’ nikiwa kidato cha kwanza haikuwa kazi rahisi kupata picha kamili. Mwalimu wetu aliandika ubaoni, ‘ cell is a basic unit of life .’ Niliduwaa. Sikujua anamaanisha nini zaidi ya kutazama kamusi kujua maana ya maneno aliyoyatumia. Mwalimu alirudia maneno hayo hayo kuweka msisitizo, na kisha akatafsiri kwa Kiswahili. Alisema, ‘maana yake ni hivi kuna kitu kidogo kisichoonekana kwa macho kwenye miili yetu kinachofanya tuishi. Mmeelewa?’  Kwa kweli hatukuwa na namna nyingine zaidi ya ‘kuelewa’ na tukaitikia, ‘ndiyo!’

Mwalimu Anavyoweza Kukuza Uelewa wa Mwanafunzi

Picha
PICHA: Sunday Adelaja Dhima kuu ya elimu iliyo bora ni kuzalisha raia wenye sifa ya udadisi. Hawa ni raia wanaofikiri kwa makini, wanaohoji mazoea, wasioridhishwa na majibu yaliyozoeleka na wenye ari ya kutafuta majibu ya changamoto zinazoikabili jamii yao. Hatua ya kwanza ya mwanafunzi kuwa mdadisi ni kuelewa kile alichojifunza. Mwanafunzi asiyeelewa maudhui ya somo, hawezi kuwa na fursa ya kufanya udadisi.

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Picha
PICHA: thesouthern.com Siku moja nikiwa kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanafunzi wa shahada za awali waliingia kufanya mtihani wa muhula wa mwisho wa masomo. Wakati wanaingia, mmoja wao alijigamba kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kukanyaga maktaba tangu amejiunga na chuo hicho miaka mitatu iliyopita. Nilishangaa inawezekanaje mwanafunzi wa chuo kikuu kujisifia jambo la fedheha kama hilo.

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -2

Picha
PICHA: Shutterstock Katika makala yaliyopita tuliona mbinu tatu unazoweza kuzitumia kuelewa mambo unayojifunza. Kwanza, ni ‘njaa’ inayokusukuma kuelewa. Unapokuwa na ari ya kuelewa jambo, mara nyingi, utahamasika kulielewa bila kutumia nguvu nyingi. Pili, tuliona ni muhimu kutengeneza picha kubwa ya jambo unalojifunza kabla hujaanza kujifunza undani wa mambo madogo madogo ndani ya picha hiyo. Kwa mfano, unaposoma aina za vyakula, lazima kwanza uelewe vyakula. Uelewa wa jumla wa vyakula utakurahisishia kazi ya kuchanganua aina zake kwa sababu tayari unayo rejea utakayoitumia kuelewa zaidi. Mbinu ya tatu ni kukihusisha kitu unachokisoma na mambo unayoyafahamu tayari. Unaposoma aina za vyakula, kwa mfano, lazima uwe unafikiria vyakula mbalimbali unavyovifahamu katika mazingira yako. Unapojaribu kuhusianisha kile unachokisoma na maisha yako ya kila siku, unaurahisishia ubongo wako kazi ya kupokea kuliko kuingiza kitu kipya kisichohusiana kwa vyovyote vile na ...

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma

Picha
PICHA: Oxford Learning Kusoma kitu usichokielewa ni hasara. Mbali na kuongeza uwezekano wa ‘kupigwa chenga’ wakati wa mtihani, kutokuelewa kunaharibu dhima ya elimu. Mtu asiyeelewa kile alichojifunza, kwa mfano, hawezi kutumia maarifa aliyonayo kuleta tija kwa jamii.

Kinachofanya Wanafunzi Wasielewe Wanachokisoma

Picha
PICHA:  SciTech Daily Ujifunzaji (learning) ni mchakato wa kupata uzoefu mpya katika maeneo makubwa matatu. Kwanza, kubadili namna mtu anavyofikiri. Maarifa mapya huja na uzoefu mpya unaobadilisha uelewa wa mambo.

Unamsaidiaje Mtoto Asiyefanya Vyema Kimasomo?

Picha
PICHA: BBC News Kwa mzazi mwenye mtoto anayesoma shule, ni rahisi kuelewa inakuwaje pale unapokuwa na uhakika mwanao ana uwezo mzuri lakini matokeo anayoyapata shuleni hayalingani na uwezo wake. Kama mzazi unayejali unajaribu kufanya wajibu wako, unamsaidia kazi za shule, unamwekea mazingira mazuri yanayomhamasisha kujisomea akiwa nyumbani, unashirikiana na walimu wake, lakini bado matokeo yanakuwa kinyume.

Mwalimu Anavyoweza Kukuza Udadisi kwa Wanafunzi -2

Picha
PICHA: The East African MWALIMU anabeba wajibu muhimu wa kuhakikisha mwanafunzi anajenga ari ya kujifunza maudhui kama yaliyoainishwa kwenye mtalaa. Mwalimu aliyeandaliwa vyema na kufuzu kazi ya kutafsiri mtalaa katika maisha ya mwanafunzi, anaweza kuibua na kuchochea udadisi kwa mwanafunzi.  Katika makala ya kwanza tulitumia mfano wa mradi wa Next Generation Leaning (NGL) unaoendeshwa na Shirika la Opportunity Education kujifunza namna mwalimu anavyoweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi. Tuliona kanuni mbili. Kwanza, mwalimu anahitaji kumfanya mwanafunzi aone namna gani kile anachofundishwa darasani kinagusa maisha yake ya kawaida. Kujua uhusiano uliopo kati ya maudhui anayojifunza na maisha yake, kunamfanya athamini maudhui husika na hivyo kuwa na ari ya kujifunza. Pili, mwalimu anahitaji kumjengea mwanafunzi uwezo wa kujiuliza maswali ya msingi kuhusu maudhui anayojifunza. Kanuni hii inamsaidia mwanafunzi kupunguza utegemezi kwa mwalimu na hivyo kujenga hali ya kuji...