Umuhimu wa Kumpunguzia Mtoto Shinikizo la Kufaulu

PICHA: Stressed Out Students



Ufaulu wa mitihani umepewa nafasi ya pekee katika mfumo wetu wa elimu. Shule zetu, kwa hakika, hazina namna nyingine ya kumwelimisha mtoto zaidi ya kumtaka akusanye, akumbuke na kutumia maarifa aliyonayo kujibu maswali ya mtihani.

Ingawa ustawi wa jumla wa mwanadamu hautegemei eneo hilo moja la ukusanyaji na utumiaji wa maarifa, shule zetu zinaonekana kuamini pasipo mtu kuwa na maarifa mengi hawezi kufanikiwa.

Kasumba hii imetuathiri na sisi wazai. Tunafikiri, kwa mfano, ni lazima mtoto afaulu masomo kwa kiwango cha juu ili afanikiwe. Matarajio haya makubwa yanatufanya tuwaweke watoto kwenye shinikizo kubwa mno la kufaulu tukiamini ufaulu huo ndio kigezo cha ustawi wao katika maisha.

Matokeo yake, tangu mtoto anapoingia shuleni kwa mara ya kwanza mpaka anamaliza, anajikuta katika mazingira ambayo kimsingi hana kazi nyingine zaidi ya kumridhisha mwalimu na mzazi wake kwamba, kama watoto wengine, na yeye anao uwezo wa kukusanya na kukumbuka maarifa. Mazoea haya yanaibua changamoto kadhaa kimalezi kwa watoto.

Kulea tabia ya ushindani

Shule zetu zinathamini wanafunzi wanaofanya vizuri na kudhihaki wale wanaoonekana dhaifu. Mtoto anayefanya vizuri darasani, kwa mfano, ndiye anayependwa na walimu, ndiye anakuwa maarufu, na ndiye anayepata zawadi ya kuwa bora kuliko wengine. Hili ni tatizo na nitaeleza kwa nini.

Kwa muda mrefu tuliamini kumzawadia mtoto mdogo aliyefanya vizuri kuliko wenzake ingekuwa si tu motisha kwake kuongeza jitihada za kufanya vizuri kwa mara mwingine tena, lakini pia ingewafanya watoto wengine kuweka bidii zaidi kwa matarajio ya kupata zawadi kama aliyopewa mwenzao.

Hata hivyo, tafiti nyingi, mfano za Prof. Carol Dweck wa Chuo Kikuu cha Stanford, zinaonyesha utamaduni huu wa kuwapongeza watoto kwa namna inayobagua uwezo wao una kasoro nyingi zinazoweza kukuza mitazamo mibovu kwa watoto.  

Kwa mfano, mtoto aliyezoea kuongoza darasani na kusifiwa anaweza kugeuka kuwa mtumwa wa sifa. Utumwa huu wa sifa unamweka kwenye hatari ya kuwa na tabia ya kuelekeza nguvu kwenye eneo linalomfanya ajione bora na hivyo kukwepa maeneo mengine ambayo, pengine, yanaweza kuwa muhimu katika maisha.

Ikiwa, mathalani, mtoto anajua walimu na wazazi humsifia kwa kufaulu vizuri, mtoto huyu anaweza kukwepa  kushiriki kazi za ndani ambazo anajua haziwezi kumgusa mzazi wake.

Pia, kupongezwa kwa kuwazidi wengine kunaweza kumkatisha tamaa mtoto hasa pale inapotokea ama anafanya vizuri lakini hakuna mtu anayejali au basi kuna mtoto mwingine anayeonekana kumzidi kinyume na vile alivyozoea.

Lakini vile vile, kwa upande wa watoto wanaoshuhudia mwenzao akizawadiwa kwa kuwazidi mara kwa mara, wengi wao hunyong’onyea na kuanza kujiona kama watu duni wasio na uwezo wa kufanya vizuri kama wenzao.

Tafsiri yake ni kwamba, kwa watoto wadogo, hakuna sababu ya msingi ya kuwawekea mazingira ya kuwashindanisha kiuwezo hali inayoweza kuwaingizia dhana ya kushindana hata katika mazingira ambayo hakuna sababu yoyote ya ushindani.

Kudumaza vipaji

Changamoto ya pili ya shinikizo hili kubwa la taaluma kwa watoto, ni kudumaza vipaji ambavyo kimsingi hakuna namna ya kuvipima kwa kutumia mitihani. Kwa kuwa shughuli karibu zote zinazoendelea darasani zinalenga kujenga eneo moja tu la kukusanya na kukumbuka maarifa, mtoto hawezi kuwa na motisha ya kufanya vitu vingine visivyohusiana na masomo.

Matokeo yake mtoto anapokuwa shuleni anakuwa hana kazi nyingine zaidi ya kusoma, kuandika na kuhesabu. Anaporudi nyumbani, hali kadhalika, anakutana na mzazi anayeamini kazi ya msingi ya kufanya kwa mwanae ni kuzingatia masomo.

Mtoto anayeishi kwenye shinikizo la namna hii anapojaribu ‘kuchepuka’ kidogo ili kukuza vipaji visivyotambuliwa na mitihani rasmi ya darasani, anajikuta kwenye mgogoro na mwalimu na mzazi.

Kwa sababu hii, watoto wetu wengi ambao pengine wangeweza kuwa na vipaji vya kila aina, wanaishia kufanya vitu ambavyo mara nyingine haviwafanani.

Kudumaza ukuaji

Shinikizo hili kubwa la kufaulu masomo pia linaathiri mtindo wa kawaida wa maisha ya mtoto. Shule inayotaka mtoto awe bora kitaaluma, kwa mfano, kwa kawaida, itamnyima fursa ya kushiriki shughuli zisizo na kimasomo lakini ambazo kimsingi zingeweza kuwa muhimu kimakuzi.

Mtoto huyu mdogo shauri ya kusoma kwenye shule inayotaka kuongoza kwenye mitihani, hatopata mtu wa kumfundisha kujifanyia usafi wake binafsi, kufagia, kushiriki kazi za mikono kwa sababu tu mitihani ambayo ndio kipimo cha ubora wa shule haina vipengele vinavyopima utu wa mtoto, ushiriki wake kwenye kazi za mikono.

Pamoja na uzuri wa kufaulu masomo, mtoto mdogo wa shule ya msingi, kwa kweli, anahitaji kufaulu pia hata kwenye maeneo mengine yenye nafasi muhimu ya kumsaidia kupata mafanikio katika maisha.

Mbali na kupata alama 95 darasani, kwa mfano, mtoto huyu anahitaji kujifunza umuhimu wa kujali hisia na mahitaji ya wengine, tabia ambayo angeweza kujifunza vizuri zaidi kupitia michezo kuliko vitabu vilivyotajwa kwenye mtalaa.

Kasoro hii ya mfumo wa elimu kutilia mkazo eneo la ufahamu na maarifa kuliko maeneo mengine, imefanya watoto wengi wakose fursa pana ya kujengwa kiroho, kimaadili na hata kupata stadi nyingine muhimu za kimaisha.

Ushauri

Natambua shauku kubwa waliyanayo wazazi kuona watoto wanashika nafasi ya kwanza darasani. Hata hivyo, kama tulivyoona kwa ufupi, shauku hiyo ya kuwa na watoto wenye ‘akili’ isiwafanye watoto wakajikuta wakibanwa mno na hivyo kukosa muda wa kujifunza stadi nyingine za maisha.

Aidha, tunazo sababu za kutosha kuvumilia hata pale tunapoona watoto wetu hawafanyi vizuri darasani. Hakuna ushahidi wa kitafiti unaothibitisha kuwa ufaulu wa sekondari na vyuoni unategemea na ufaulu mkubwa wa ngazi za chini.

Miaka ya awali ina umuhimu mkubwa katika kujenga sura ya maisha atakayoishi mtoto. Tunahitaji kuweka msisitizo mkubwa kwenye kujenga utu, kuwakuza kiroho na kuwafundisha stadi za maisha, kwa sababu hayo ndiyo maeneo yatakayoamua mustakabali wao.


Pia, utamaduni wa kuwashindanisha watoto wa ngazi za chini hauna tija. Tunaweza kuwafanya watoto wakajifunza vizuri bila kuwaambia wameshika nafasi ya ngapi darasani. 

Maoni

  1. Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
    * upendo
    inaelezea * inaelezea kivutio
    * kama unataka ex wako nyuma
    *acha talaka
    *kuvunja mawazo
    * huponya viharusi na magonjwa yote
    * uchawi wa kinga
    *Ugumba na matatizo ya ujauzito
    * bahati nasibu
    * bahati nzuri
    Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
    Whatsapp:+2349046229159

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia