Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2017

Umuhimu wa Kumpunguzia Mtoto Shinikizo la Kufaulu

Picha
PICHA: Stressed Out Students Ufaulu wa mitihani umepewa nafasi ya pekee katika mfumo wetu wa elimu. Shule zetu, kwa hakika, hazina namna nyingine ya kumwelimisha mtoto zaidi ya kumtaka akusanye, akumbuke na kutumia maarifa aliyonayo kujibu maswali ya mtihani. Ingawa ustawi wa jumla wa mwanadamu hautegemei eneo hilo moja la ukusanyaji na utumiaji wa maarifa, shule zetu zinaonekana kuamini pasipo mtu kuwa na maarifa mengi hawezi kufanikiwa.

Ufanyeje Kijana Chipukizi 'Anapokata' Mawasiliano na Wewe?

Picha
PICHA:  Parent Pump Radio Kama nilivyoeleza kwenye makala yaliyopita, tofauti za kimtazamo kati ya mzazi na kijana anayechipukia ni hali zinazotarajiwa. Wakati mwingine tofauti hizi zinaweza kuonekana kama mambo madogo yasiyo na msingi. Lakini tofauti hizi zinazoonekana kuwa ndogo zisiposhughulikiwa zinaweza kukomaa na hatimaye kusababisha matatizo makubwa. Wazazi, mara nyingi, hatupendi kuzipa uzito tofauti hizi mara zinazopoanza kujitokeza. Kijana wako anaweza kuanza kuwa mkimya bila sababu za msingi, anaanza kukukwepa na hata kupunguza mawasiliano na wewe, lakini ukachukulia ‘kawaida.’

‘Homework’ Zinavyodumaza Ukuaji wa Watoto Wadogo

Picha
PICHA:  PhillyVoice Ukiwauliza wazazi kitu gani wanafikiri kikisitizwa mapema zaidi kwa watoto kitawasaidia kufanikiwa, wengi  watakwambia elimu. Kwa sababu hiyo, wazazi hasa wasomi wanaharakisha kuwapeleka shule watoto wenye umri mdogo. Ninawafahamu watoto wengi wa miaka minne wanaosoma darasa la kwanza. Wazazi wa watoto hawa wanafanya hivyo wakiamini mtoto akisoma mapema, maana yake uwezekano wa kufanikiwa maishani unakuwa mkubwa.

Maswali Matano Yatakayokusaidia Kujua Thamani ya Kazi Yako

Picha
Nianze kwa kukuuliza swali rahisi. Kitu gani kinakupa motisha ya kuamka asubuhi na kwenda kazini? Unafikiri nini hasa kinaongeza thamani ya kazi yako? Kwa mujibu wa tafiti, takribani asilimia 80 ya watu wanaofanya kazi za kuajiriwa au kujiajiri hawapati utoshelevu. Kwa hakika mambo mengi yanachangia watu kutokupenda kazi zao. Kuna migororo kazini, kutokufikia matarajio waliyokuwa nayo na wakati mwingine mazingira hafifu ya kazi. Pia, sababu nyingine ni kutokuona namna gani kazi anayofanya mtu inakidhi makusudi mapana ya maisha yake. Katika mazingira haya, ni vigumu kuona thamani ya kazi yake na hivyo itakuwa vigumu kutosheka. Mtu anayependa kazi yake mara nyingi anakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuwa mbunifu, kuwa na bidii zaidi na hivyo kupata matokeo mazuri kuliko mtu anayesukumwa kufanya kitu asichoona thamani yake. Kwa kuzingatia ukweli huo, katika makala haya tunaangazia maeneo matano yanayoweza kukusaidia kuelewa kwanini kazi unayoifanya inaweza kuwa na

Hisia Zilizojeruhiwa Zinavyoweza Kujenga Ukatili Usiotarajiwa

Picha
PICHA: Pride News Magazine Baraka amekuwa akilalamikiwa kwa tabia yake ya udokozi tangu akiwa darasa la tatu. Ingawa alikuwa mdogo kwa umbo, jina lake maarufu lilikuwa ‘Baraka kibaka.’ Mbali ya kuwa kibaka, baraka alikuwa mgomvi aliyepambana na karibu kila mwanafunzi shuleni.

Mbinu za Kumshirikisha Mwanafunzi Katika Ujifunzaji

Picha
PICHA:  United Nations Majuzi niliwatembelea walimu wanafunzi waliokuwa wakiendelea na mazoezi ya ufundishaji. Mafunzo kwa vitendo yana umuhimu wa kipekee katika maandalizi ya walimu. Katika kipindi hiki, mwanafunzi anapewa fursa ya kutumia maarifa aliyojifunza darasani katika mazingira halisi ya kazi. Kwa mwalimu, kama mimi, hiki ni kipindi cha kutathmini uwezo wa mwanafunzi wa ualimu kumudu majukumu yake. Moja wapo ya vipindi vingi nilivyopata bahati ya kuhudhuria ni Baiolojia kidato cha III kilichokuwa kikifundishwa na mwanafunzi wangu wa mwaka wa II. Baada ya kufanya utangulizi wa somo lake, mwalimu huyu mwanafunzi aliwaelekeza wanafunzi wake kukaa katika makundi ya watu watano watano kusudi wafanye majadiliano. Majadiliano ni mbinu muhimu ya ufundishaji inayowawezesha wanafunzi kujifunza. Kama tulivyosema kwenye makala yaliyopita, kupitia majadiliano, mwanafunzi hupata fursa ya kusikiliza mtazamo tofauti kutoka kwa wenzake. Aidha, majadiliano ni mbinu