Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2012

Waholanzi na utamaduni wa baiskeli, sisi tunakimbilia magari binafsi

Picha
 Wakati sisi tunashindana kwenda kazini na magari ya bei mbaya, wenzetu wanakuja kazini na baiskeli. Hapa ni Ede, Uholanzi. Baiskeli ndio usafiri maarufu. Jambo hili si la kawaida. Fikiria, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu achilia Profesa wake, apande baiskeli kwenda chuoni. Kwa hakika ni jambo unaloweza kuliewa pale Dar es salaam. Waholanzi wakiwa wamepaki vyombo vyao vya usafiri. Picha:Jielewe Katika mazingira haya ambapo kila mtu anatafsiri maendeleo kwa kuangalia vitu, na katika mazingira ambayo kila mtu yuko tayari kuonekana naye yupo hata ikibidi kwa mkopo, almuradi aendeshe gari, ni vigumu kupata ufumbuzi wa 'kero' ya kudumu ya foleni jijini Dar es Salaam.  Kila mmoja anafikiri kutatua kero hii kwa kuongeza gari barabarani. Foleni itoke wapi kwa mazingira haya? Picha: Jielewe Kituo cha elimu MDF, Ede, Uholanzi. Picha: Jielewe Hebu fikiri kama watu wangeamua kutumia usafiri wa umma, huu huu uliopo, magari mangapi yangeondoka barabarani? Saa n